F TAMKO LA JUMUIA YA WAZAZI YA CCM KUTENGUA MATOKEO YA UJUMBE WA NEC KUTOKA WAZAZI - BARA | RobertOkanda

Thursday, December 14, 2017

TAMKO LA JUMUIA YA WAZAZI YA CCM KUTENGUA MATOKEO YA UJUMBE WA NEC KUTOKA WAZAZI - BARAMwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi Dkt. Edmund Bernard Mndolwa ametengua ushindi wa Ndg. Ngingite Nassoro Mohamed ambaye alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa kupitia Jumuiya ya Wazazi (Bara) baada ya kubaini uwepo wa kasoro kubwa katika uhesabuji wa kura wakati wa uchaguzi.

Kufuatia uamuzi huo Dkt. Edmund Mohamed Mndolwa amemtangaza Ndg. Kitwala Erick Komanya kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa kupitia Jumuiya ya Wazazi (Bara).Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Edmund Benard Mndolwa akizungumzia kuhusu kutengua ushindi wa mjumbe mmoja aliyechaguliwa kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuiya ya Wazazi kwa upande wa Tanzania bara.

0 comments:

Post a Comment