MAMENEJA, WATUNGA SERA UHIFADHI WANYAMAPORI WAPEWA KIBARUA KIZITO.

Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi akimkabidhi kitabu Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Wanyamapori cha Serengeti, Dk...


Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi akimkabidhi kitabu Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Wanyamapori cha Serengeti, Dkt.Robert Fyumagwa mara baada ya hafla iliyofanyika jana jijini Arusha ya uzinduzi wa kitabu kinachoelezea hali ya bioanuwai kabla ya ujenzi wa barabara itakayoanzia Mto wa Mbu kwenda Natron hadi Loliondo itakayoruka kipande katika hifadhi ya Serengeti hadi Mugumu. Wengine ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti ya Wanyamapori (TAWIRI), Prof. Apolinaria Pereka (kushoto) na Mkurugenzi wa Mipango na Sera wa Wizara Dkt. Iddi Mfunda.

Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi amewataka Mameneja pamoja na Watunga sera za uhifadhi wa Wanyamapori waanze kuyafanyia kazi matokeo ya tafiti 186 zilizowasilishwa na wanasayansi watafiti wa uhifadhi ili zilete tija kwa taifa

Amewataka Mameneja na Watunga sera hao kuacha tabia ya kuzifungia tafiti hizo kwenye makabati badala yake wazisome ili waweze kuzitumia katika kujibu changamoto zilizojitokeza kwenye uhifadhi.

Milanzi amesema kuwa masuala yaliyoibuliwa kwenye tafiti hizo yaanze kutafutiwa ufumbuzi yasisubili hadi matatizo yatokee.
Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti ya Wanyamapori (TAWIRI), Prof. Apolinaria Pereka pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TAWIRI, Simon Mduma (wa pili kulia) mara baada ya kufunga mkutano wa kumi na moja wa wanasayansi watafiti wa wanyamapori wa kutoka ndani na nje ya nchi uliofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano AICC wa jijini Arusha.

Alibainisha hayo jana mjini Arusha wakati alipokuwa akifunga Mkutano wa kimataifa wa kumi na moja wa wanasayansi watafiti wa uhifadhi wa wanyamapori, mazingira pamoja na mabadiliko ya tabianchi.

Mkutano huo ulioandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) umefanyika kwa muda wa siku tatu ambapo wanasayansi watafiti wa kutoka ndani na nje ya nchi waliwasilisha na kujadili tafiti 186 katika maeneo hayo.

Aidha, Milanzi amezitaka Taasisi na Mashirika binafsi kuiga mfano wa TAWIRI ya kuandaa mikutano inayowakutanisha watu kutoka sehemu mbalimbali Duniani hali inayopelekea kuvitangaza vivutio vya utalii pamoja na kukua kwa utalii wa mikutano.Amesema azma ya Serikali ni kuhakikisha Utalii wa mikutano inaanza kuchukua nafasi kwa kulingiizia Taifa mapato yatokanayo na wageni wanaokuja kwa ajili ya kuhudhuria mikutano ya kimataifa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya TAWIRI, Prof. Apolinaria Peleka amesema mkutano huo umetoa fursa kwa wahifadhi pamoja na watunga sera kuziona changamoto zinazoikabili nchi katika masuala ya uhifadhi.

Aliongeza kuwa, tafiti hizo zilizowasilishwa zitaisaidia Serikali kupanga mipango yake ya muda mrefu na muda mfupi kulingana na matokeo ya tafiti zilivyojitokeza.

Aidha, amezitaka taasisi na mashirika binafsi kuzitumia tafiti hizo kwa ajili ya kujiletea maendeleo.

Mkutano huo ulifunguliwa juzi na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ambapo alizitaka taasisi za Serikali pamoja na mashirika binafsi ziisaidie TAWIRI ili iweze kufanya tafiti tofauti na inavyofanya sasa.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAMENEJA, WATUNGA SERA UHIFADHI WANYAMAPORI WAPEWA KIBARUA KIZITO.
MAMENEJA, WATUNGA SERA UHIFADHI WANYAMAPORI WAPEWA KIBARUA KIZITO.
http://blog.maelezo.go.tz/wp-content/uploads/2017/12/2-11-1024x678.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/12/mameneja-watunga-sera-uhifadhi.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/12/mameneja-watunga-sera-uhifadhi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy