MUGABE AKOMAA: LICHA YA KUVULIWA UENYEKITI WA ZANU-PF ASISITIZA YEYE BADO NI AMIRI JESHI MKUU

NA K-VIS BLOG/Mashirika ya Habari RAIS wa Zimbabwe ambaye sasa yuko matatani, anakabiliwa na ukomo (deadline) uliowekwa na ch...





NA K-VIS BLOG/Mashirika ya Habari

RAIS wa Zimbabwe ambaye sasa yuko matatani, anakabiliwa na ukomo (deadline) uliowekwa na chama chake kujiuzulu, baada ya kutoa hotuba ya kushangaza ambapo amekataa kuachia madaraka.

Mugabe mwenye umri wa miaka 93, anatakiwa kujiuzulu ifikapo saa 6 mchana leo Novemba 20, 2017, vinginevyo bunge la nchi hiuyo ambalo lina wafuasi wengi kutoka chama chake cha ZANU-PF litapiga kura ya kutokuwa na imani nae na hivyo kumuondoa madarakani.

Emmerson Mnangagwa, ambaye alitimuliwa na Mugabe hivi karibuni kwenye nafasi ya umakamu wa Rais, ametangazwa kuwa kiongozi wa ZANU-PF baada ya wanachama wa chama hicho kumng’oa madarakani Mugabe ambaye ndiye alikuwa Mwenyekiti wa taifa wa ZANU-PF.

Katika hotuba yake ya maandishi aliyoisoma kwa dakika 20 kwenye televisheni ya taifa, hakuna mahala alipotaja, msukosuko wa sasa kutoka kwenye chama chake au raia wa nchi hiyo ambao majuzi walijitokeza barabarani na kuhanikiza jiji la Harare huku wakimtaka Mugabe aondoke madarakani.

Badala yake Mugabe alisema jeshi la nchi hiyo halijafanya makosa kutwaa madaraka na kumuweka kwenye kizuizi cha nyumbani.

“Kwa vyovyote vile ambavyo jeshi lilitekeleza operesheni zake, mimi kama Amirijeshi Mkuu, ninatambua kuguswa kwao” Alisema Mugabe akirejea jinsi jeshi la nchi hiyo lilivyozingira Shirika la Utangazaji la Taifa jijini Harare.

Mugabe pia alisema, “Mkutano Mkuu wa ZANU-PF unatarajiwa kufanyika wiki chache zijazo na mimi nitauongoza mkutano huo hatua kwa hatua”. Alisema


Kabla ya hotuba hiyo ya Mugabe, Zanu-PF tayari ilimtangaza Mnangagwa kuwa kiongozi mpya wa chama hicho na pia mgombea wake wa kiti cha urais kwenye uchaguzi mkuu ujao huku mke wa Mugabe, Grace, akitimuliwa chamani.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MUGABE AKOMAA: LICHA YA KUVULIWA UENYEKITI WA ZANU-PF ASISITIZA YEYE BADO NI AMIRI JESHI MKUU
MUGABE AKOMAA: LICHA YA KUVULIWA UENYEKITI WA ZANU-PF ASISITIZA YEYE BADO NI AMIRI JESHI MKUU
https://1.bp.blogspot.com/-F7CjnPgZ0Yo/WhJydtTsFMI/AAAAAAAA-Og/D_60AjMJFagRzKiVQ-Rc7OI6wt93KMZbQCLcBGAs/s640/mugabe.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-F7CjnPgZ0Yo/WhJydtTsFMI/AAAAAAAA-Og/D_60AjMJFagRzKiVQ-Rc7OI6wt93KMZbQCLcBGAs/s72-c/mugabe.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/11/mugabe-akomaa-licha-ya-kuvuliwa.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/11/mugabe-akomaa-licha-ya-kuvuliwa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy