F WAZIRI MAKAMBA AELEZA MOJA YA KERO KUBWA YA MUUNGANO ILIYOSALIA NI KODI | Okandablogs

Thursday, October 19, 2017

WAZIRI MAKAMBA AELEZA MOJA YA KERO KUBWA YA MUUNGANO ILIYOSALIA NI KODINA K-VIS BLOG, ZANZIBAR
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe.January Makamba amesema moja kati ya changamoto za muungano zilizobakia kwa sasa ni masuala ya kodi, ikiwemo taratibu za kodi ya VAT na usimikaji wa mitambo inayoshahabiana kwenye vituo vya forodha vya pande mbili za muungano.
Pia amesema, kuwepo kwa bandari zisizo rasmi “bubu” ni tatizo linguine na kuziagiza mamlaka kuhakikisha linasimamia mambo hayo ili kukomesha.
“kumekuwepo na manung’uniko kwenye eneo hili la ulipaji kodi stahiki na yapo mambo mengi yanayochangia manung’uniko hayo, nitoe wito tu kwamba lazima tujitahidi kuhakikisha kero hizo zinaondoka kabisa” alisema Mhe. Makamba
Ameeleza kwamba amelipokea suala hilo na kwamba tayari linashughulikiwa na mamlaka husika kwa uratibu wa Ofisi ya Makamu wa Rais. Hata hivyo, ameahidi kusukuma ukamilishaji wà utekelezaji wà masuala haya kupitia kwenye vikao vya ngazi ya juu kwa maamuzi. Hii ni baada ya kutembelea Shirika La Bandari Zanzibar (ZPC), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB).
Waziri Makamba leo ni siku ya pili ya ziara yake ya wiki moja kufatilia utekelezaji wa hatua za kutatua changamoto za Muungano. Ziara ya leo imelenga kubaini changamoto za kiforodha na kikodi zinazosababisha changamoto katika fursa za kiuchumi na biashara kati ya wananchi wa pande mbili za Muungano.0 comments:

Post a Comment