KAMPUNI YA KILUA INDUSTRIAL GROUP YAANDAA KONGAMANO KUBWA LA UWEKEZAJI WA VIWANDA JIJINI BEIJING,NCHINI CHINA

Kampuni ya Kilua Industrial Group of Companies imeandaa kongamano kubwa la uwekezaji wa Viwanda kwa kuwaalika viongozi Waandamizi wa Ser...


Kampuni ya Kilua Industrial Group of Companies imeandaa
kongamano kubwa la uwekezaji wa Viwanda kwa
kuwaalika viongozi Waandamizi wa Serikali ya Mkoa wa
Pwani,wafanyabiashara wakubwa ambao ni wamiliki wa viwanda na makampuni
mbalimbali,litakalofanyika jijini Beijing,nchini China.

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo,Mohamed Said Kilua
amesema kuwa kongamano hilo linatarajia kufanyika Oktoba 25,2017 katika hoteli
kubwa yenye hadhi ya nyota tano jijini Beijing,litakalojumuisha wafanyashabiashara
wamiliki wa viwanda na makampuni  wapatao
200 kutoka majimbo mbalimbali nchini China.



“Sisi Kilua Industrial Group of Companies tumeamua  kuibeba dhana ya Tanzania ya Viwanda kwa
utekelezaji kwa vitendo,na pia kuunga mkono dhamira ya Rais Dkt John Pombe
Magufuli ya kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya Viwanda, na kwa njia moja ama
nyingine iweze kuzigeuza rasimali maliasili  kuwa bidhaa”alisema Kilua.



Tanzania iliyojaaliwa ardhi yenye rutuba kwa kilimo cha
mazao ya Chakula na Biashara,haiwezi kutafsiri maendeleo hayo ya Kilimo bila
kuzigeuza bidhaa zilizoandaliwa kwa soko la ndani na lile la Kimataifa bila
kuwepo na viwanda vidogo/vya kati na vikubwa vitakavyozalisha bidhaa zenye
viwango vyenye ubora katika ushindani wa soko”alisisitiza Kilua.


 Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni Kilua Industrial Group of Companies,Mohamed Said Kilua (pichani shoto) pamoja na viongozi waandamizi wa Serikali ya mkoa wa Pwani wakipatiwa maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Huateng Metalluargical Co.Ltd, Chunsheng Jiang (wa nne kulia) kuhusiana na michoro waliyopewa kama zawadi, ikionesha mandhari ya maeneo mbalimbali ya jiji la Beijing pamoja na shughuli zao nchini China.


Viongozi hao ni Mkurugenzi wa halmashauri Wilaya ya Kibaha, Bi. Tatu Selemani (kofia nyekundu), Mansouly Ally ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibaha, Afisa Biashara (M) Pwani Suleiman Sirindwa, Katibu Tawala Msaidizi - Uchumi na Uzalishaji -Mkoa wa Pwani,Shangwe Twamala, Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bi. Philomena Kasanga pamoja na Katibu Tawala mkoa wa Pwani, Zuberi Mhina. 


Viongozi hao wamekuja jijini Beijing nchini China kwa ziara iliyoratibiwa na Kampuni ya Kiluwa Group of Companies,chini ya Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wake Mohamed Said Kiluwa (mwenye koti la njano) kwa ajilia kushiriki Kongamano kubwa la Viwanda. 
Aidha baada ya kukutana leo viongozi hao pamoja na wadau wakuu wa mambo ya viwanda nchini China, ambapo Oktoba 25 kutakuwepo na Kongamano litakalohusu masuala ya viwanda,litakajumuisha wadau wapatao 200 kutoka maeneo mbalimbali nchini humo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani (pichani kati)Zuberi Mhina akikata kipande cha nyama ya Mbuzi,ikiwa ni ishara ya kuwakaribisha wageni na wenyeji kwenye chakula cha jioni kiliochoandaliwa na wenyeji wa Beijing,kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni Kilua Industrial Group of Companies,Mohamed Said Kilua,kulia ni Katibu Tawala Msaidizi - Uchumi na Uzalishaji -Mkoa wa Pwani,Shangwe Twamala pamoja na Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bi. Philomena Kasanga wakishuhudia tukio hilo usiku huu.

 Baadhi ya wenyeji ambao nao wanatarajiwa kushiriki kongamano la Viwanda linalotarajia kufanyika Octoba 25,2017 chini ya Uratibu mkubwa wa kampuni ya Kilua Industrial Group of Companies,jijini Beijing nchini China.

 Wageni wakipewa maelezo mafupi katika baadhi ya michoro ambayo walipewa kama zawadi kutoka kwa wenyeji wao,kabla ya kupata chakula cha jioni pamoja.


COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: KAMPUNI YA KILUA INDUSTRIAL GROUP YAANDAA KONGAMANO KUBWA LA UWEKEZAJI WA VIWANDA JIJINI BEIJING,NCHINI CHINA
KAMPUNI YA KILUA INDUSTRIAL GROUP YAANDAA KONGAMANO KUBWA LA UWEKEZAJI WA VIWANDA JIJINI BEIJING,NCHINI CHINA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhDWiVR8qAy8URor3wM7jq9SvnHItV8rOwgOc1FUPmz0DSdpj-qIaWPMc_fUEtQ26r_8GW2YBm91eCSUTUj_h7uGpkALp5blzIrALqldTMW8ekHDnMkUOHNy6Wxu1dIDhG0FquPGLv0RNGC/s640/IMG-20171022-WA0005.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhDWiVR8qAy8URor3wM7jq9SvnHItV8rOwgOc1FUPmz0DSdpj-qIaWPMc_fUEtQ26r_8GW2YBm91eCSUTUj_h7uGpkALp5blzIrALqldTMW8ekHDnMkUOHNy6Wxu1dIDhG0FquPGLv0RNGC/s72-c/IMG-20171022-WA0005.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/10/kampuni-ya-kilua-industrial-group.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/10/kampuni-ya-kilua-industrial-group.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy