IAWRT YAVITAKA VYOMBO VYA HABARI NCHINI KUWA NA SERA YA JINSIA

Mwenyekiti wa Chama cha Kimataifa cha Wanawake Wanaofanyakazi kwenye Vituo vya Runinga na Redio (IAWRT) imevitaka vyombo vya habari kuwa...





Mwenyekiti wa Chama cha Kimataifa cha Wanawake Wanaofanyakazi kwenye Vituo vya Runinga na Redio (IAWRT) imevitaka vyombo vya habari kuwa na sera ya jinsia kwani kwa kufanya hivyo kutaongeza ufanisi wa kazi katika vyombo hivyo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa IAWRT nchini, Rose Mwalimu katika mafunzo yaliyotolewa na chama hicho kwa waandishi wa habari wa vituo vya runinga, redio na mtandaoni kuhusu sera ya jinsia katika vituo vyao vya kazi.

Mwalimu alisema katika kusaidia kuwepo na sera ya jinsia wameandaa mafunzo hayo ambayo yanalenga kusaidia kukuza sera ya jinsia katika maeneo ya kazi kwa wanahabari jambo ambalo litasaidia kuboresha vipindi vinavyorushwa kwani hata uandaaji wake utakuwa unahusisha jinsia zote.

Mwenyekiti wa Chama cha Kimataifa cha Wanawake Wanaofanyakazi kwenye Vituo vya Runinga na Redio (IAWRT) nchini, Rose Mwalimu akizungumza katika mafunzo ya waandishi wa habari yaliyoandaliwa na chama hicho.

"Haya mafunzo ya leo ni njia mojawapo ya kukuza sera ya ujinsia katika vyombo vya habari, utekelezaji wake huwa ni katika kutafuta watu ambao ni watangazaji ambao wao ndiyo watakuwa kama wasimamizi ambapo kupitia wao watatengeza vipindi ambavyo vitakidhi sera ya jinsia inavyotaka ili na wengine waige,

"Lengo ni kuwa na vipindi bora na sio tu vipindi bora lakini vipindi bora ambavyo vitakuwa na tija katika jamii ... tatizo wafanyakazi wengi hawajui haya madhara kama hakuna utekelezaji wa sera ya jinsia, madhara yapo kwa namna mbili, kwa wafanyakazi wao wenyewe na kwa wasikilizaji na watazamani, kwako kutokuwa na sera kama hushirikihi hizi jinsi mbili hata huo uhuru wa kupeana habari unakuwa haupo," alisema Mwalimu.



Alisema kuwa takwimu za utafiti walioufanya mwaka 2014 zinaonyesha kuwa ni vyombo vya habari vichache ambavyo vina sera ya jinsia hivyo hata uwiano wa madaraka katika vyombo hivyo unakuwa upande mmoja wa wanaume.

“Utakuta hata vyombo vya habari wakurugenzi na wahariri wakuu ni wanaume sasa wanawake wapo wapo na wanafanya nini?, wanawake wengi watangazaji wanapewa habari zinazowahusu wao wenyewe lakini hawashirikishwi vya kutosha katika habari za maendeleo," alisema Mwalimu.
Gladness Munuo akiwasilisha mada mbalimbali katika mafunzo kwa wanahabari kuhusu sera ya jinsia.
Baadhi waandishi wa habari walioshiriki mafunzo kuhusu sera ya jinsia.

Mwenyekiti wa IART akiwa katika picha ya picha ya pamoja washiriki na wakufunzi wa mafunzo hayo.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: IAWRT YAVITAKA VYOMBO VYA HABARI NCHINI KUWA NA SERA YA JINSIA
IAWRT YAVITAKA VYOMBO VYA HABARI NCHINI KUWA NA SERA YA JINSIA
http://www.thebeauty.co.tz/wp-content/uploads/2017/10/DSC_0077.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/10/iawrt-yavitaka-vyombo-vya-habari-nchini.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/10/iawrt-yavitaka-vyombo-vya-habari-nchini.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy