TUME YA TAIFA YA MIPANGO YA MATUMIZI YA ARDH I(NLUPC) YATOA TATHIMINI YA UTAFITI WALIOFANYA KORIDO YA MNGETA NA UKANDA WA UDZUNGWA-MGOMBELA-SELOUS,KILOMBERO-MOROGORO

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero (DAS)  Mh. Robert Selasela akifungua mkutano huo kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Kilombero uliohusu ...


Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero (DAS)  Mh. Robert Selasela akifungua mkutano huo kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Kilombero uliohusu uhifadhi wa Mazingira, Matumizi bora ya Ardhi, Hati  miliki za Kimira na Bioanuai katika Korido ya Mngeta na ukanda wa  Udzungwa-Mgombela-Selous.


 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) Dkt.  Stephen Nindi (aliyesimama) akitoa maneno ya utangulizi kwa wadau wa  Korido ya Mngeta na ukanda wa Magombela-Selous-Udzungwa wilayani  Kilombero juu ya utafiti uliofanywa na wataalam kutoka Tume hiyo  wakishirikiana na Asasi ya kiraia ya African Wildlife Foundation  uliolenga maeneo ya uhifadhi wa Mazingira, Matumizi bora ya Ardhi, Hati miliki za Kimira na Bioanuai  katika Korido ya Mngeta na ukanda wa Udzungwa-Mgombela-Selous, iliyofanyika Wilayani Kilombero.


 
Bw. Eugine Cylilo mtaalam kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi akitoa tathimini ya tafiti iliyofanywa na wataalamu kutoka Tume wakishirikiana na African Wildlife Foundation (AWF) ambayo ilionesha hali halisi ya usimamizi wa mipango ya Ardhi katika Korido ya Mngeta na ukanda wa Udzungwa-Mgombela-Selous juu ya utunzaji wa Mazingira na Bioanuai, Mipango ya matumizi
ya Ardhi na hati miliki za kimila na migogoro ya ardhi.


 Wadau wakimsikiliza Bw. Eugine Cylilo mtaalam
kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi akiwasilisha utafiti huo.


 Bi. Jane Mkinga Afisa mradi wa jumuiko la maliasili Tanzania akichangia maswala juu ya maliasili
 Diwani wa kata ya Mngeta Mh. Flora Kigawa akitaka kupata ufafanuzi  wa
changamoto za kutatua migogoro kati ya vijiji na pia kutaka kufahamu
idadi ya wanawake wangapi wanamiliki ardhi katika wilayani Kilombero.


 Diwani wa Kata ya Chita Mh. Chelele John akiuliza maswala mbalimbali yahusuyo Ardhi.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Bi.
Albina Burra akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali yaliyoulizwa na wadau
kuhusu utunzaji wa Mazingira na Bioanuai,Mipango ya matumizi
ya Ardhi na hati miliki za kimila na migogoro ya ardhi.
 Bw. Pastor Magingi Meneja wa Programu wa  asasi yakiraia ya African
Wildlife Foundation akieleza namna walivyoshirikiana  NLUPC katika
utafiti wa uhifadhi wa Mazingira, Matumizi bora ya Ardhi, Hati miliki za
Kimira na  Bioanuai katika Korido ya Mngeta na ukanda wa Udzungwa-Mgombela-Selous.


 Muwezeshaji wa Mkutano huo Bw. Geofrey Siima akiendelea kutoa Muongozo wakati wa warsha hiyo.

 Afisa Miradi kutoka asasi ya Kiraia ya Solidardad Bi. Maria Sengelela akitoa
maelezo ya namna wanavyoshirikiana na NLUPC katika swala zima la  matumizi bora ya Ardhi.


Afisa Sheria wa Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi ya Ardhi Bi. Devotha Salukele akijibu Maswala mbali mbali yahusuyo sheria yaliyoulizwa na wananchi kuhusu Ardhi.



 Afisa Ardhi Mteule kutoka Wilaya  Kilombero Bi. Syabumi Mwaipopo akifafanua na  kujibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wadau wakati wa mkutano huo.




 Afisa Mipango wa Wilaya ya Kilombero Bw. Ludwing Ngakoka akizungumza jambo wakati wa Mkutano huo.

 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero Mh. David Lugazio akitoa neno la Shukurani baada ya Mkutano huo kumalizika.

Wajumbe mbalimbali wakiendelea kufuatilia mkutano huo.

Picha ya pamoja 

Katika kuhakikisha kuwa kuna mipango na matumizi bora ya ardhi nchini Tanzania, Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi ya Ardhi kwa kushirikiana na Asasi ya Kiraia ya African Wildlife Foundation (AWF) walifanya utafiti wa uhifadhi wa Mazingira, Matumizi bora ya Ardhi, Hati miliki za Kimila na Bioanuai katika korido ya Mngeta na ukanda wa
Udzungwa-Mgombela-Selous Wilayani Kilombero.

Akizungumza wakati wa kuwasilisha utafiti huo kwa Madiwani, Watendaji Wilaya, Tarafa na Kata, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya matumizi ya Ardhi (NLUPC) Dkt. Stephen Nindi alisema kuwa Tume ilifanya utafiti katika ushoroba wa Mngeta pamoja na ukanda wa Udzungwa-Magombela-Selous lengo likiwa ni kuangalia mambo mbalimbali yanayohusu matumizi bora ya Ardhi, umiliki wa ardhi, uhifadhi ya mazingira na Bioanoai katika maeneo hayo.

Mkurugenzi Mkuu alidokeza kuwa Wilaya ya Kilombero ni moja ya Wilaya tajiri katika nchi ya Tanzania ambayo ina ardhi yenye rotuba kubwa inayofaa kwa kilimo cha aina mbalimbali pamoja na uoto wa aina mbalimbali “Kuna matumizi ya aina mbalimbali ya ardhi katika Wilaya hii, tuna wakulima, wawekezaji wakubwa katika kilimo, wawekezaji wakubwa katika misitu, hifadhi ya wanyama pori, kilomo cha kati na kilimo cha wakulima wadogo wadogo, wafugaji, wavuvi, wafanya biashara ambao kwa umoja wanatengeneza ubia mbalimbali katika matumizi ya Ardhi” alisema Dkt. Nindi.

Aliongeza kuwa lengo la utafiti huu ilikuwa kuangalia wadau mbalimbali katika utumiaji, upangaji na usimamizi wa ardhi wanatekelezaje, kuangalia changamoto za mipango ya matumizi ya Ardhi, umiliki wa ardhi, uhifadhi wa mazingira na Bioanoai.

“Tupo hapa kwa ajili ya kuwasilisha utafiti wetu kwamba namna gani mambo haya yanafanyika shughuli hizi za uhifadhi wa mazingira na Bioanoai, Shughuli za upangaji na matumizi ya Ardhi, umiliki wa Adhi pamoja na utekelezaji wake na usimamizi zinavyofanyika katika kanda hizi mbili” alisema Dkt. Nindi.

Akiwasilisha matokeo ya utafiti huo, mtaalamu wa mazingira kutoka Tume bwana Eugen Cyrilo, alibainisha changamoto kadhaa matumizi ya ardhi, umiliki pamoja na uhifadhi wa mazingira. “Changamoto kubwa iliyobainika katika utafiti huu, ni utekelezaji wa maipango ya matumizi ya ardhi. Vijiji vingi tulivyopitia vimeandaliwa mipango ya matumizi ya ardhi, ila kwa kuwa hakuna usimamizi wa mipango hiyo kwa ngazi ya vijiji, kunakuwa hakuna utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi waliojitengea” alieleza bwana Cyrilo.

Aidha, katika upande wa mazingira, ilibainika kuwa kumekuwa usimamizi usioridhisha hasa kwenye misitu na vyanzo vya maji kwa baadhi wanavijiji wenyewe au watu kutoka nje ya vijiji kuvamia na kuweka makazi kwenye misitu ikiwa pamoja na kukata miti bila utaratibu. “Kwenye baadhi ya maeneo, kumekuwa na uvamizi wa misitu ambapo hapo awali ilikuwa imetengwa kwa ajili ya uhifadhi, na sehemu zingine tulikuta wanavijiji wakifanya shughuli ambazo si rafiki kwa mazingira pembezoni mwa mito, hii ni tishio kubwa katika utunzaji wa mazingira” alisema bwana Cyrilo.

Akichangia katika matokeo ya utafiti huo, Meneja wa Programu kutoka AWF bwana Pastor Magingi aliwasihi uongozi wa Wilaya kuja na suluhisho la kusimamia mipango ya matumizi ya ardhi ili kufanya kazi nguvu kubwa inayofanywa na na Tume, Wadau pamoja na Halmashauri yenyewe isipotee bure.

Hatua hii iliwapelekea Madiwani wa Kata zilizohusika kwenye utafiti huu kupendekeza kuwapo kwa mtaalamu wa Wilaya atakayehusika moja moja na kusimamia utekelezakji  wa mipango ya matumizi ya ardhi katika Wilaya
ili kutoa ripoti ya mara kwa mara juu ya usimamaizi na utekelezaji wa mipango
ya matumizi ya ardhi ili kuwa endelevu na yenye manufaa kwa wananchi.

Utafiti huo ulihusisha Kata nne za ukanda wa Udzungwa-Magombera-Selous, ambazo ni Msolwa Stesheni, Mkula, Mang'ula B na Sanje pia kulikuwa na vijiji nane vya Msolwa Stesheni, Mkula, Sonjo, Msufini,Katurukila, Kanyenja, Magombera na Sanje. Aidha katika korido ya Mngeta utafiti huo ulihusisha kata sita za Namawala, Igima, Mbingu, Mngeta, Chita na Mofu pamoja na Vijiji  vya Mofu, Ihenga, Kisegese, Vigaeni, Makutano, Igima, Mbingu, Njage, Mngeta, Mchombe na Lukolongo.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TUME YA TAIFA YA MIPANGO YA MATUMIZI YA ARDH I(NLUPC) YATOA TATHIMINI YA UTAFITI WALIOFANYA KORIDO YA MNGETA NA UKANDA WA UDZUNGWA-MGOMBELA-SELOUS,KILOMBERO-MOROGORO
TUME YA TAIFA YA MIPANGO YA MATUMIZI YA ARDH I(NLUPC) YATOA TATHIMINI YA UTAFITI WALIOFANYA KORIDO YA MNGETA NA UKANDA WA UDZUNGWA-MGOMBELA-SELOUS,KILOMBERO-MOROGORO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhwhjS1u-JJpOtEj9oObAa0m2EiIXYLB01nEQZr1i7kcDKTtjSViByqQSzwnWrloiB0b8IgC7TOcmZiiK7XGbaHZkk2wgtiyWWMRVcwti1Vctuxy7zKdJ5XgDx73LUI7hlqZfsMDvU_i5wq/s640/4.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhwhjS1u-JJpOtEj9oObAa0m2EiIXYLB01nEQZr1i7kcDKTtjSViByqQSzwnWrloiB0b8IgC7TOcmZiiK7XGbaHZkk2wgtiyWWMRVcwti1Vctuxy7zKdJ5XgDx73LUI7hlqZfsMDvU_i5wq/s72-c/4.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/09/tume-ya-taifa-ya-mipango-ya-matumizi-ya.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/09/tume-ya-taifa-ya-mipango-ya-matumizi-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy