ZIARA YA RAIS DK.SHEIN KASKAZINI B UNGUJA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini  Unguja...



DSC_4525
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini  Unguja Mhe.Vuai Mwinyi Khamis mara alipowasili katika viwanja vya Sea Cliff Hotel Shehia ya Kama Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja alipofanya ziara katika Wilaya  hiyo Agosti 12/2017.
DSC_4526
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa  Kaskazini  Unguja Mhe.Haji Juma Haji mara alipowasili katika viwanja vya Sea Cliff Hotel Shehia ya Kama Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja alipofanya ziara katika Wilaya  hiyo.
 
DSC_4533
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Makamanda wa vikosi vya ulinzi  mara alipowasili katika viwanja vya Sea Cliff Hotel Shehia ya Kama Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja alipofanya ziara katika Wilaya hiyo. 
DSC_4537
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini  Unguja Mhe.Vuai Mwinyi Khamis na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serkali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe.Haji Omar Kheir (kushoto) pamoja na Viongozi mbali mbali mara alipowasili katika  Hotel ya Sea Cliff Shehia ya Kama Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja alipofanya ziara katika Wilaya hiyo.

DSC_4547
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Viongozi mbali mbali katika ukumbi wa mikutano wa Hotel ya Sea Cliff   Shehia ya Kama Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja katika Mkutano wa Ziara maalum ya kutembelea miradi mbali mbali ya mendeleo kwa Mkoa wa Kaskazini  Unguja iliyoanza leo,kabla ya kupata taarifa ya mkoa katika ukumbi huo.

DSC_4552
Baadhi ya Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kaskazini “B”Unguja na Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi wakiwa katika mkutano wa utolewaji wa taarifa ya Mkoa wa Kaskazini Unguja iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe,Vuai Mwinyi Mohamed (hayupo pichani) katika ukumbi wa Sea Cliff Hotel Shehia ya Kama Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja.
 
DSC_4555
Baadhi ya Washauri wa Rais na Viongozi wengiine walipokuwa wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe,Vuai Mwinyi Mohamed (hayupo pichani) alipokuwa akitoa taarifa yakee ya utelezaji wa majukumu ya Mkoa wa Kaskazi Unguja katika mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Sea Cliff Hotel Shehia ya Kama Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.

DSC_4573
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohanmed Shein akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Vuai Mwinyi Mohamed (kushoto) wakati alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Tangi la Maji safi na Salama   katika Kijiji cha Kisongoni Upenja Wilaya Kaskazini “B” Unguja leo, akiwa katika ziara ya kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo,(wa pili kulia) Waziri wa Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira Mhe.Salama Aboud Twalib.

DSC_4578
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akipokea taarifa ya Utekelezaji Kazi ya Mkoa wa Kaskazini Unguja kutoka kwa Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Vuai Mwinyi Mohamed baada ya kuisoma katika mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Sea Cliff Hotel Kama Wilaya ya  Kaskazini “B”,Rais alipofanya ziara maalum katika Wilaya hiyo kuangalia Miradi mbali mbali ya Maendeleo,[Picha na Ikulu.] 12 /08/2017.
DSC_4605
Baadhi ya  Viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipozungumza nao akiwa katika ziara ya kuangalia Miradi mbali mbali ya Maendeleo katika mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Sea Cliff Hotel Kama Wilaya ya  Kaskazini “B”,Unguja.

DSC_4607
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali (hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Sea Cliff Hotel Kama Wilaya ya  Kaskazini “B”,Unguja,alipofanya ziara maalum  ya kuangalia Miradi mbali mbali ya Maendeleo katika Wilaya hiyo (Picha na Ikulu).
…………………………………………………………………..
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
MAKAMO Mwenyekiti wa CCM Zanzibar  Dkt. Ali Mohamed Shein  amewataka viongozi na watendaji wa chama hicho kufanya kazi za kuimarisha taasisi hiyo ya kisiasa ili ishinde na kuongoza dola katika uchaguzi mkuu ujao.
Rai hiyo ameitoa  wakati akizindua Tawi la CCM la Kitope ‘B’  jimbo la Mahonda kwenye ziara yake ya kukagua na kuzindua miradi mbali mbali ya maendeleo aliyoianza leo Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Dkt. Shein alisema viongozi na wanachama wa chama hicho wanatakiwa kutumia vyema ofisi za Tawi hilo ambalo ni la kisasa kwa lengo la kutekeleza kwa ufanisi kazi za kisisaa zitakazozaa matunda ya ushindi katika uchaguzi wa mwaka 2020.
“Kwanza nakupongezeni viongozi na wanachama wote wa jimbo la Mahonda mlioshiriki kujenga tawi hili la kisasa linaloendana na hadhi ya chama chetu kimaendeleo kwani lina ofisi zote ambazo ngazi zote kiutendaji ndani ya tawi mtafanya kazi zenu kwa utulivu.
Pia nasaha zangu kwenu ni kwamba uchaguzi mkuu unakaribia haupo mbali hivyo tumieni ofisi hii vizuri kuchapa kazi kwa bidii sambamba na kuongeza wanachama wapya ambao ndio mtaji wetu mkubwa wa kisiasa ili kuhakikisha 2020 tunashinda.”, alisisitiza Dkt. Shein.
Aidha alisema kuwa lengo la serikali ya mapinduzi ya Zanzibar inayotokana na CCM ni kuimarisha huduma zote za kijamii na kiuchumi ili wananchi wa mijini na vijijini waweze kunufaika na fursa hizo.
Dkt.Shein ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alitembelea ujenzi wa kituo kipya cha mashine za kutibia maji kinachojengwa katika eneo la Donge mbiji ambapo mradi huo uliofadhiliwa na serikali ya China utagharimu zaidi ya Dola za kimarekani milioni 5.5.
Katika ziara hiyo  Dkt. Shein alitembelea  shamba la  karafuu  na  kuzungumza  na mliki wa mradi wa kilimo cha karafuu huko Donge  Pwani, Haroun Abou Mbarouk alieleza kuwa shamba hilo lenye mikarafuu zaidi ya 170 limekuwa likizalisha zao hilo kwa wingi ambapo kwa mavuno ya mwaka wanapata zaidi ya gunia 25.
Sambamba na hayo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alitembelea mradi wa ujenzi wa tangi la Maji huko Donge Kisongo unaojengwa na mafundi  kutoka jamhuri ya watu wa China utakaowanufaisha  wananchi  wa Wilaya ya Kaskazini “B”  na maeneo jirani.
Ziara hiyo itaendelea kesho katika Wilaya ya Kaskazini  ‘’A” Unguja ambapo Dkt.Shein ataweka  mawe ya msingi katika miradi mbali mbali ya kijamii na kuhitimisha kwa hotuba ya majumuisho ndani ya Mkoa huo.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: ZIARA YA RAIS DK.SHEIN KASKAZINI B UNGUJA
ZIARA YA RAIS DK.SHEIN KASKAZINI B UNGUJA
http://fullshangweblog.com/home/wp-content/uploads/2017/08/DSC_4525.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/ziara-ya-rais-dkshein-kaskazini-b-unguja.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/ziara-ya-rais-dkshein-kaskazini-b-unguja.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy