WOTE SCHEME MKOMBOZI WA WANANCHI, ASEMA NAIBU WAZIRI WA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

NAIBU Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amesema " Wote scheme ni Mkombozi kwa wananchi wengi walio katika S...







NAIBU Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amesema " Wote scheme ni Mkombozi kwa wananchi wengi walio katika Sekta isiyo rasmi na ameushahuri Mfuko wa Pensheni wa PPF kushirikiana na Maafisa Maendeleo ya Jamii kupitia Ofisi za Halmashauri ili kuweza kuwafikia kwa urahisi jamii ambayo haipo kwenye ajira rasmi na kuweza kunufaika na Mfumo huo.

Mfuko wa Pensheni wa PPF unashiriki katika Maonesho ya Nane nane kitaifa Lindi kwa lengo la kuendelea kutoa elimu kwa wananchi hasa walio katika sekta isiyo rasmi kama vile wakulima, wafugaji, Wavuvi, wajasiriamali wakubwa na wadogo na wengine wote waliojiajiri wenyewe juu ya Mfumo wa " Wote scheme " ambao unawawezesha kujiwekea akiba wakati huo huo wakipata fursa za mafao ya Uzeeni, huduma za bima ya afya, mikopo ya maendeleo na mikopo ya kujiendeleza kielimu.


Vilevile kwa wale walioajiriwa wanaweza kumtumia Mfumo huu wa "Wote scheme" kama mfumo wa hiari wa kujiwekea akiba
Zaida Mahava, Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya kusini amesema kwa kutambua kundi kubwa la jamii ambalo halipo kwenye ajira rasmi wameona ipo haja ya kutoa elimu juu Mfumo wa Wote scheme ili waweze kunufaika na huduma zinazotolewa na PPF kupitia Mfumo wa Wote scheme.



Naibu Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Angelina Mabula (Mb) akiongea jambo na Meneja wa PPF Kanda ya Kusini Bi Zaida Mahava (kushoto) pamoja na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF baada ya kupewa maelezo ya namna ya Mfumo wa WOTE SCHEME unavyofanya kazi na faida zake kwa sekta isiyo rasmi wakati alipotembelea Banda la PPF lililopo chini ya banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Kilimo Nane Nane 2017 yanayofanyika Kitaifa Lindi katika Viwanja vya Ngongo Halmashauri ya Manispaa ya Lindi



Meneja wa PPF Kanda ya Kusini Bi Zaida Mahava akimuelekeza Mwananchi jinsi ya kujaza fomu ya kujiunga na mfumo wa hiari wa Wote scheme baada ya kupewa elimu alipofika katika Banda la PPF lililopo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika Kitaifa Lindi katika Viwanja vya Ngongo Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.


Naibu Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Angelina Mabula (Mb) akusaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la PPF lililopo chini ya banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Kilimo Nane Nane 2017 yanayofanyika Kitaifa Lindi katika Viwanja vya Ngongo Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WOTE SCHEME MKOMBOZI WA WANANCHI, ASEMA NAIBU WAZIRI WA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
WOTE SCHEME MKOMBOZI WA WANANCHI, ASEMA NAIBU WAZIRI WA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhXlL8rrVz2ZM5INn-BJ3DR8MOkro58ilKZbI8N0DD1bKizMLs-7Pdr87P-mVR8nDMSaqnPTEn8KL-3kWCeS8jRzDLA_n62SQ5M0eGZIG7X3dGBp1suErTc0KlaUfhkBR6c6jkEj3_DKh3t/s640/4.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhXlL8rrVz2ZM5INn-BJ3DR8MOkro58ilKZbI8N0DD1bKizMLs-7Pdr87P-mVR8nDMSaqnPTEn8KL-3kWCeS8jRzDLA_n62SQ5M0eGZIG7X3dGBp1suErTc0KlaUfhkBR6c6jkEj3_DKh3t/s72-c/4.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/wote-scheme-mkombozi-wa-wananchi-asema.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/wote-scheme-mkombozi-wa-wananchi-asema.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy