WAZIRI MKUU AWASILI NCHINI CUBA KWA ZIARA YA KIKAZI

TUTAENDELEZA MAHUSIANO YA KIDIPLOMASIA YALIYOJENGWA NA AWAMU ZILIZOTANGULIA-MAJALIWA WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali y...



TUTAENDELEZA MAHUSIANO YA KIDIPLOMASIA YALIYOJENGWA NA AWAMU ZILIZOTANGULIA-MAJALIWA



WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli inayatambua na kuyathamini mahusiano mazuri ya kidiplomasia yaliyojengwa na awamu zilizotangulia baina ya Tanzania na mataifa mbalimbali ikiwemo Jamuhuri ya Cuba na kwamba itayaendelea.

Ametoa kauli hiyo jana jioni (Alhamisi, Agosti 17, 2017), alipozungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, Bi Anna Teressa mara baada ya kuwasili nchini Cuba kwa ajili ya ziara ya kikazi yenye lengo la kudumisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

“Tanzania na Cuba zina historia ya kutosha. Tunatambua mahusiano mazuri yaliyopo kati nchi zote mbili, ambayo yalikuwepo kuanzia Serikali ya Awamu ya kwanza chini ya uongozi wa Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Nyerere.”

Amesema katika ziara yake hiyo anatarajia kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali ya Cuba kwa lengo la kukuza ushirikiano katika sekta za Afya, Elimu, Utalii na Kilimo.

Waziri Mkuu amesema Cuba ni mojawapo kati ya nchi zenye ushirikano wa muda mrefu na Tanzania kisiasa, kijamii, kiafya na kiuchumi.”Mfano katika Sekta ya Afya, madaktari wengi kutoka Cuba walikuwa wanakuja Tanzania kutibu wagonja waliokuwa na maradhi makubwa.”

Pia Waziri Mkuu amesema katika ziara hiyo anatarajia kukutana na Jumuya ya Wafanyabiashara wa Cuba ili kuwaelezea fursa za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania hususan  katika Sekta ya Viwanda pamoja na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Kwa upande wake Bi. Anna ambaye alimpokea Waziri Mkuu kwa niaba ya Serikali ya Cuba alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea ushirikiano mzuri baina ya nchi hizo mbili, hivyo alimuhakikishia kwamba wataendelea kuudumisha.

Pia Bi. Anna ametumia fursa hiyo kuupongeza uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli kwa namna inavyopambana na rushwa, ufisadi, kuhimiza uwajibikaji pamoja na kutetea wanyonge.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
IJUMAA, AGOSTI 18, 2017.


COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI MKUU AWASILI NCHINI CUBA KWA ZIARA YA KIKAZI
WAZIRI MKUU AWASILI NCHINI CUBA KWA ZIARA YA KIKAZI
https://i.ytimg.com/vi/Yum_OIuB888/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/Yum_OIuB888/default.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/waziri-mkuu-awasili-nchini-cuba-kwa.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/waziri-mkuu-awasili-nchini-cuba-kwa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy