WANANCHI WAENDELEA KUNUFAIKA NA MAONESHO YA NANENANE LINDI

Na Mathias Canal, Lindi   Maonyesho ya Nanenane Kanda ya Kusini ambayo yalianza tokea tarehe 1/8/2017 katika viwanja vya...


Na Mathias Canal, Lindi 

Maonyesho ya Nanenane Kanda ya Kusini ambayo yalianza tokea tarehe 1/8/2017 katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi yanaendela kushika kasi huku kivutio kikubwa ikiwa ni baaada ya bidhaa mbalimbali zinazoonyeshwa kwenye mabanda na Halmashauri mbalimbali kutoka mikoa yote miwili inayounda kanda ya kusini ambayo ni Lindi na Mtwara.

Kwa ujumla wake maonyesho ni mazuri kwani yamehusisha shughuli nyingi za Kilimo, Uvuvi na mifugo kama kauli mbiu inavyosema “Zalisha kwa Tija Mazao na Bidhaa za Kilimo Mifugo na Uvuvi ili kufikia Uchumi wa Kati” kauli mbiu hii ikiwa na msisitizo na hamasa zaidi kwa wananchi kutambua mbinu bora za Kilimo Mifugo na Uvuvi ili kuwa na kipato kikubwa kitakachopelekea wananchi kwa ujumla wao kufikia uchumi wa kati.

Pia kumekua na wajasiriamali wengi sana ambao wamefika katika Maonesho hayo wakiwa na bidhaa mbalimali zikiwemo bidhaa za ngozi, mikoba, viungo, asali, vyakula vya asili, mashine Ndogondogo na vingine vingi vya kuvutia.

Maonyesho ya mwaka huu yamekua chachu na kuwa na mvuto mkubwa kwani tangu kufunguliwa kwake kumekuwa na mgeni rasmi anayetembelea kila siku ambao ni mwaaziri, ama wakuu wa mikoa kutoka katika mikoa husika jambo ambalo limefanya maandalizi kuwa makubwa na mazuri zaidi.

Kanda ya kusini ina fursa nyingi za kiuchumi kama vile Hali ya hewa nzuri, na Uzalishaji mazao mbalimbali hususani zao kubwa la Korosho, Jambo la msingi ni kujipanga vizuri  na kuhakikisha tunatumia fursa hizi  kikamilifu ili kupunguza umasikini na kuleta utajirisho.

Katika hotuba nyingi zinazotolewa na wageni mbalimbali wanaozuru katika Maonesho hayo ni kuhusu Tatizo kubwa linalokabili sekta ya kilimo na ufugaji nchini kwa wahusika kutozingatia kanuni bora na za kisasa za kilimo na Ufugaji.

Hivyo katika maonesho haya kuwapo kwa Taasisi za utafiti zinazozalisha mbegu za kisasa, Kuwapo kwa teknolojia na zana za kilimo za kisasa ni njia mojawapo ya kuongeza tija kwa jambo ambalo litawasaidia wananchi kufahamu zaidi kanuni bora za kilimo.

Ufugaji nyuki ni fursa mpya ambayo endapo Watanzania wataichangamkia itawaletea kipato na kuwaondolea umasikini. Fursa haihitaji gharama kubwa kuazisha gharama kubwa ni kununua mizinga na kuweka maeneo rafiki ya nyuki ili waweze kuingia.

Baada ya hatua hiyo hakuna gharama yeyote zaidi ya kuvuna na kuchakata asali ili iwe na ubora wa kimataifa.

Nyuki wanatoa mazao mengi ikiwa ni pamoja na nta ambayo inatumika kutengeneza mishumaa na bidhaa nyingine.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WANANCHI WAENDELEA KUNUFAIKA NA MAONESHO YA NANENANE LINDI
WANANCHI WAENDELEA KUNUFAIKA NA MAONESHO YA NANENANE LINDI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi_e9z12X_ZUfghRUT60dGecESkILSQ5j9-z1n2xAg58FUftzDqTUztIEnU_1wyMPtDOB_zg8fQgab9sp0XOEVf_ZdRTdLwk4IXVf1VQ-q4dEm0Qf0RKY4x7BK8Qe4SvWpjwjkeEtkSLJ8/s640/DSC_0961_New1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi_e9z12X_ZUfghRUT60dGecESkILSQ5j9-z1n2xAg58FUftzDqTUztIEnU_1wyMPtDOB_zg8fQgab9sp0XOEVf_ZdRTdLwk4IXVf1VQ-q4dEm0Qf0RKY4x7BK8Qe4SvWpjwjkeEtkSLJ8/s72-c/DSC_0961_New1.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/wananchi-waendelea-kunufaika-na.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/wananchi-waendelea-kunufaika-na.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy