WAKULIMA WILAYANI KILWA MKOANI LINDI WAUFANANISHA UGONJWA WA MIHOGO NA UKIMWI

 Mwenyekiti wa Kijiji cha Ruyaya kilichopo Kata ya Lihmalyao wilayani Kilwa Mkoa wa Lindi, Hassan Amanzi, akizungumza wakati wa ufu...
 Mwenyekiti wa Kijiji cha Ruyaya kilichopo Kata ya Lihmalyao wilayani Kilwa Mkoa wa Lindi, Hassan Amanzi, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kilimo kwa wakulima wa Kijiji hicho yaliyofanyika wilayani humo jana. Wengine ni viongozi na wajumbe wa kijiji hicho. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).
Wazee na vijana wakiwa kwenye mafunzo hayo.  Mkulima Athuman Hassan akizungumzia kukosekana kwa dawa ya salfa ya kuua wadudu kwenye mikorosho.
 Mkulima Mohamed Sadiki akichangia jambo kuhusu zao la mhogo.
 Selemani Mbanga, akizungumzia jinsi wanyama waharibifu tembo na nguruwe wanavyo haribu mazao yao.
 Mkulima Mohamed Dege akielezea ugonjwa unaofanana na Ukimwi unavyoshambulia mihogo yao.
 Wakina mama wa kijiji hicho wakiwa kwenye mafunzo hayo.
 Mwezesha wa mafunzo hayo kutoka Jukwaa la Bioteknolojia (OFAB), Dk.Hamalord Mneney, akitoa mafunzo ya kilimo cha kisayansi na Bioteknolojia kwa wakulima hao.
 Wakulima wakiwa kwenye moja ya shamba la mihogo katika kijiji hicho kwa mafunzo.
 Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia, OFAB, ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Morogoro, SUA, Philbert Nyinondi akiangalia mhogo katika moja ya mashamba ya kijiji hicho wakati akipatiwa maelezo ya ugonjwa unaoshambulia mihogo kutoka kwa mkulima, Mohamed Maundu.
Majadiliano yakiendelea katika shama hilo.

Na Dotto Mwaibale, Kilwa-Lindi

WAKULIMA  wa mihogo katika Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi wamefananisha ugonjwa unaoshambulia mihogo yao kuwa kama  ukimwi uliokosa dawa kutokana na mihogo kuooza na kunyauka majani yake ambapo wameomba wataalamu wa kilimo na serikali kuwasaidia ili waondokane na changamoto hiyo.

Hayo yamebainika katika ziara ya watafiti wa kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ya kutoa mafunzo ya kilimo bora cha mihogo kwa wakulima wa Kijiji cha Ruyaya kilichopo Kata ya Lihmalyao wilayani Kilwa mkoani Lindi jana.

Akizungumza katika mafunzo hayo mkulima Mohamed Rashid Dege alisema changamoto kubwa waliyonayo ni ugonjwa wa ukimwi wa mihogo ambao unawasumbua kwa muda mrefu ambao unashambulia mihogo yao na hauna dawa.

"Ugonjwa huu wa ukimwi wa mihogo unaifanya mihogo kuliwa au kuoza na majani yake kukauka hatujui ni ugonjwa gani ni ugonjwa ambao unatusumbua sana tunaomba wataalamu na serikali watusaidi kutuondolea  kero hii" alisema Dege.

Mkulima Athuman Mwamba alisema changamoto nyingine waliyonayo ni kukosekana kwa mbegu bora zilizozalishwa kitaalamu hivyo waliwaomba watafiti kuwapelekea mbegu bora.

Selemani Mbanga ambaye ni mkulima wa kijiji hicho alisema changamoto nyingine waliyo nayo ni kukosekana kwa soko la uhakiki la kuuza mihogo yao na wanyama waharibifu kama tembo na nguruwe kushambulia mihogo yao.

Mkulima Hamisi Mohamed alisisitiza kukosekana kwa soko la mihogo na barabara ya ambayo haipitiki vizuri wakati wa mvua.

Athumani Hassan alililamikia changamoto ya kutopatika dawa ya salfa kwa ajili ya kupulizia mikorosho ambayo katika msimu huu wa kilimo hawajapata ya kutosha  na kusabibisha mashamba ya mikorosho kushambuliwa na wadudu.

Ofisa Ugani kutoka Ofisi ya Kilimo ya Halmshauri ya Wilaya ya Kilwa, Manyusi  Ngilangwa alisema dawa ya salfa kwa ajili ya kupulizia mihogo ya wakulima hao haikuweza kutosheleza kwa sababu ya kukosekana kwa idadi halisi ya wakulima kutokana na kuuza korosho zao maeneo ya mbali ya kijiji hicho.

"Dawa ya salfa imetolewa kidogo kwa kuwa hakukuwa na taarifa ya idadi ya wakulima ambayo hupatikana wakati wakiuza korosho zao kwa walanguzi bila ya kutumia ghala lao ambalo lipo kijijini hapo jambo lililosabisha kuto kuwa na idadi kamili ya wakulima" alisema Ngilangwa.

Alisema wakulima wanapotumia kuuza korosho zao katika ghala hilo inakuwa rahisi kupata idadi yao hivyo kuletewa pembejeo zao kwa urahisi.

Mwezesha wa mafunzo hayo kutoka Jukwaa la Bioteknolojia (OFAB), Dk.Hamalord Mneney aliwaambia wakulima hao ugonjwa wa mihogo wanaoufananisha na ukimwi kuwa ni ugonjwa batoto na michirizi ya kahawia ambapo aliwata wakulima hao kufuata ushauri wa wataalamu wa kilimo na kutumia mbegu bora zenye zisizo na magonjwa.

Dk. Mneney aliwaambia wakulima hao kuwa waongeze bidii katika kilimo chao na kuwa waondoe dhana ya kudai soko la mihogo halipo ambapo aliwahakikishia kuwa soko lipo iwapo watalima na kuvuna mihogo isiyo na magonjwa.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Hassan Amanzi aliishukuru COSTECH kwa kuwapelekea mafunzo hayo ambayo yameongeza mori kwa wakulima hao.(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAKULIMA WILAYANI KILWA MKOANI LINDI WAUFANANISHA UGONJWA WA MIHOGO NA UKIMWI
WAKULIMA WILAYANI KILWA MKOANI LINDI WAUFANANISHA UGONJWA WA MIHOGO NA UKIMWI
https://1.bp.blogspot.com/-lToGWgXVg0c/WYi_f_Z2eTI/AAAAAAAAbrU/8Lj2_PHLmgQSEZ73PMnqL9gRHtiBgVb3wCLcBGAs/s640/IMG_2845.JPG
https://1.bp.blogspot.com/-lToGWgXVg0c/WYi_f_Z2eTI/AAAAAAAAbrU/8Lj2_PHLmgQSEZ73PMnqL9gRHtiBgVb3wCLcBGAs/s72-c/IMG_2845.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/wakulima-wilayani-kilwa-mkoani-lindi.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/wakulima-wilayani-kilwa-mkoani-lindi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy