WAKULIMA WAASWA KUJENGA MAHUSIANO MAZURI NA WAFANYABIASHARA

Na Mathias Canal, Lindi Baada ya kuimarisha umoja na ushirikiano wa wakulima wenyewe ni vema wakulima wakajenga mahusiano mazur...

Na Mathias Canal, Lindi

Baada ya kuimarisha umoja na ushirikiano wa wakulima wenyewe ni vema wakulima wakajenga mahusiano mazuri na wafanyabiashara ili kutokutoa mianya kwa madalali ambao mara nyingi wamekuwa wakilalamikiwa kuwa wananunua mazao ya wakulima kwa bei ya chini huku wao wakiyauza kwa bei ya juu.

Hayo yameelezwa na baadhi ya wadau wa kilimo waliozuru katika sherehe za maonesho ya Wakulima Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

Wamesema kuwa Ni vema kukatengenezwa mfumo mzuri utakaowasaidia wakulima kupata taarifa sahihi za masoko na bei halisi ya bidhaa kupitia umoja wao, kuliko kuendelea kusherehekea kila mwaka wakati wakulima bado wanateseka na bei kandamizi za madalali.

Suala hili linaenda sambamba na kaulimbiu ya sherehe za Nane Nane mwaka huu ambayo ni “Zalisha kwa Tija Mazao na Bidhaa za Kilimo Mifugo na Uvuvi ili kufikia Uchumi wa Kati”  
Juma Msembi ni moja ya washiriki wa Maonesho ya Nanenane anasema serikali inapaswa kuzidi kuwa kiunganishi kizuri kati ya wakulima na soko, ili wakulima wasikate tamaa katika kuzalisha chakula kingi.

Anasema kuwa anaamini Sherehe hizi zitakuwa chachu ya kujadili na kutathmini maendeleo ya sekta ya kilimo na changamoto zinazowakabili wakulima na kuangalia namna ya kuzitatua.

Katika Maonesho haya wakulima watajifunza mbinu bora za kisasa za kilimo zitakazowawezesha kupata mazao mengi na kuinua kipato chao.

Msembi anatoa wito kwa wakulima na mashirika kujitokeza katika maonesho hayo kwa sababu watapata fursa ya kujifunza mambo mengi na kubadilishana uzoefu na wataalamu mbalimbali wa kilimo.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAKULIMA WAASWA KUJENGA MAHUSIANO MAZURI NA WAFANYABIASHARA
WAKULIMA WAASWA KUJENGA MAHUSIANO MAZURI NA WAFANYABIASHARA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiYev1YwXS5kxWhUlklkixisNaeBDZz9sZ1tCiQ71VX2CRd9W1-4ZiJp-nUtWdXe4FkhhwCRf0tvI3ALNh-v4_Wdx4SsjyE2rCIczALn-LAdhdgwxW02m1nY4SNJwA9Hk1ZPv_7_jOvptg/s640/DSC_0622.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiYev1YwXS5kxWhUlklkixisNaeBDZz9sZ1tCiQ71VX2CRd9W1-4ZiJp-nUtWdXe4FkhhwCRf0tvI3ALNh-v4_Wdx4SsjyE2rCIczALn-LAdhdgwxW02m1nY4SNJwA9Hk1ZPv_7_jOvptg/s72-c/DSC_0622.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/wakulima-waaswa-kujenga-mahusiano.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/wakulima-waaswa-kujenga-mahusiano.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy