VIJANA ZAIDI YA 60 WAMLALAMIKIA MWEKEZAJI KWA KUWARUSHA FEDHA ZAO

 wamama wa kijiji cha Sambaru wakiendelea kutwanga mawe kwa ajili ya kuweka tayari kwa kupatikana madini ya  ya zahabu. baadhi ...





 wamama wa kijiji cha Sambaru wakiendelea kutwanga mawe kwa ajili ya kuweka tayari kwa kupatikana madini ya  ya zahabu.

baadhi ya vijana wa kijiji cha sambaru
Na Woinde Shizza,Singida



Zaidi ya vijana 60 wa kijiji cha
Sambaru kata ya Ikungi  wilayani Igungi
mkoani Singinda wamemlalamikia mwekezaji wa kampuni ya  Sambaru
Gold Mining kwa kitendo cha kuwarusha fedha za malipo  ya kazi walikuwa wakimfanyia mgodini kwake



 Wakiongea na waandishi wa habari kijijini hapo
baadhi ya vijana hao walisema kuwa wamefanya kazi katika kampuni hiyo kwa
kipindi cha mda mrefu lakini muwekezaji huyo ajawalipa ela zao  na badala yake amewafukuza kazini hapo bila
kuwalipa malipo yoyote .









Mmoja wa vijana hao aliyejitambulisha
kwa jina la Saidi Hassan alisema kuwa walishapeleka malalamiko yao kwa viongozi
wa kijiji  lakini hakuna hatua  yeyote iliyochukuliwa hivyo wameiomba serikali
iwasaidie ili wapate mafao yao kwani fedha hizo walikuwa wanazitegemea katika
kuwasaidia katika majukumu mbalimbali ya kifamilia.









“tumekuwa tunamfata muwekezaji huyu
na kumuomba  atulipe fedha zetu lakini
amekuwa anatukana na kusema atudai ,mbaya zaidi kunawakati alifikia hatua ya
kukamata baadhi ya wenzetu ambao wanamdai na kuwapeleka polisi,”alisema Saidi









Kwa upande wake kijana mungine
aliyejitambulisha kwa jina la Fredy John alisema kuwa kunakipindi walishawahi
kumpeleka polisi alipofika na kuulizwa kama vijana hao wanamdai alikuabali na
akahaidi kuwalipa na aliomba mda na akapewa kimaandishi lakini ,muda huo
umepita na hadi leo vijana hao awajalipwa na amefikia hatua ya kuwakana kabisa









Gazeti hili lilimtafuta mwenyekiti wa
kijiji hicho cha Sambaru Mfaume Hassan  ili kubainisha kama anataarifa za vijana hawa
nae alisema kuwa ni kweli anataarifa za vijana hawa na alishamtumia mmiliki wa
kampuni hiyo taarifa za kuwalipa vijana hawa lakini hajateleza   hivyo ameamua kupeleka swala hili katika
ngazi za juu ili  wamsaidie









“sisi kama kijiji tumekuwa tuna
utaratibu wa  kuwapa vijana wawekezaji
hawa nah ii inatokana na uhitaji wa muwekezaji ,unakuta muwekezaji anataka
vijana wa kumsaidia kazi uko mgodini kwake analeta barua katika ofisi ya
kijiji  na sisi tunampa  vijana na ndio utaratibu uliofanywa sasa
muwekezaji huyu kaja kuchukuwa vijana lakini cha kushangaza wamefanya kazi
mgodini kwake lakini ajawalipa mpaka leo na mbaya zaidi akifatwa anasema kuwa
adaiwi kitu ambacho sio cha kweli mimi kama kiongozi wa kijiji nikishirikiana
na wenzangu tutajitaidi kufuata sheria ili vijana hawa walipwe ela zao na hadi
sasa navyoongea nilishampa taarifa mkuu wa wilaya”alisem Mwenyekiti wa kijiji
Mfaume Hassan









Gazeti hili lilimtafuta  mmiliki wa kampuni ya Sambaru  Gold Mining Ahamed Magoma  kujibu
tuhuma hizi nae alisema kuwa yeye kama yeye adaiwi na kijana yeyote Yule
wa kijiji cha Sambaru ,na kama kuna mtu anae mdai afuate  vyombo husika vya sheria akamdai









“mimi sidaiwi na kijana yeyote Yule vijana
wangu wote ambao nawaajiri  nawalipa
vizuri na wengine wapo kazini hadi sasa,pia mimi sijawai kwenda kijijini
kutafuta kijana wa kunifanyia kazi na napenda kusema ivi kama kuna mtu ambae
ananidai afuate sheria  ,aje na vielelezo
anidai  na kama ni kweli nitamlipa ila
sidaiwi na mtu yeyote “alisema Magoma









Akiongelea swala hilo mkuu wa wilaya
ya Ikungi
Miraji Mtaturu alisema kuwa swala hilo
alishalipokea kutoka kwa mwenyekiti wa kijiji cha Sambaru  na alimuagiza aandike idadi ya vijana hao
pamoja na majina yao ili ayafanyie kazi ,aidha pia alisema kuwa atamuandikia
barua  ya kumuita ofisini kwake  mmiliki wa mgodi huo wa Sambaru Gold Mining .









COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: VIJANA ZAIDI YA 60 WAMLALAMIKIA MWEKEZAJI KWA KUWARUSHA FEDHA ZAO
VIJANA ZAIDI YA 60 WAMLALAMIKIA MWEKEZAJI KWA KUWARUSHA FEDHA ZAO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgpgwU3emXRV8SyJJrCNZivsvlPh-dYY0hVLnLNrKhQ2MmOQtebEkcUZzCwLdMBZrBWQWNpAQG1A6nSFDRXRyuLoh123iapRd-SJ97FuqPMnNWpiwmfDaWf9BfKfbfBZwVIkuWmLhNWryfE/s640/DSC00597.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgpgwU3emXRV8SyJJrCNZivsvlPh-dYY0hVLnLNrKhQ2MmOQtebEkcUZzCwLdMBZrBWQWNpAQG1A6nSFDRXRyuLoh123iapRd-SJ97FuqPMnNWpiwmfDaWf9BfKfbfBZwVIkuWmLhNWryfE/s72-c/DSC00597.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/vijana-zaidi-ya-60-wamlalamikia.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/vijana-zaidi-ya-60-wamlalamikia.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy