TIGO YATOA MSAADA WA KOMPUTA 47 KWA CHUO KIKUU CHA DODOMA

Makamu  M kuu wa  C huo  K ikuu Dodoma,  Prof. Idris Kikula akipokea moja  kati ya komputa 47 za thamani ya shilingi milioni 71/- toka k...


Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Dodoma,  Prof. Idris Kikula akipokea moja  kati ya komputa 47 za thamani ya shilingi milioni 71/- toka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Simon Karikari.Wengine kutoka kushoto Makamu Msaidizi Mkuu wa Chuo, Utawala, Mipango na Fedha, Prof. Ahmed Amme, Makamu Mkuu Msaidizi Chuo Kikuu Udom, Prof. Peter Msofe, Meneja huduma kwa jamii Tigo, Halima Okash(mwenye kilemba) na Meneja mawasiliano Tigo, Woinde Shisael. Hafla iliyofanyika jana chuoni hapo.


Meneja Mawasiliano Tigo, Woinde Shisael akizungumza na waandishi wa habari kwenye hafla ya kukabidhi komputa .


Baadhi ya wafanyakazi wa chuo kikuu Dodoma (UDOM)wakifutilia makabidhiano

Dodoma, Agosti 1, 2017- Kampuni inayoongoza kwa mtindo wa  maisha ya kidijitali, Tigo Tanzania leo  imetoa msaada wa kompyuta 47 za thamani ya  shilingi milioni 71 kwa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ili kuimarisha juhudi za taasisi hiyo  za kutoa elimu ya juu nchini.
Wakati akikabidhi kompyuta hizo kwa chuo hicho Kaimu  Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari alisema kuwa kupitia sera ya kampuni ya uwajibikaji kampuni hiyo imejikita katika kuwawezesha vijana na jamii kwa ujumla kufikia taarifa za  kimataifa na uelewa, ambapo watajifunza, kupanua ubunifu wao na kushirikiana na wenzao duniani kote.
Alifafanua zaidi  kuwa kupitia mchango huo, Tigo imeunga mkono Serikali ya Tanzania katika mtazamo wake wa kubadilisha nchi kuwa na uchumi unaoegemea katika uelewa ifikapo mwaka   2025 na kuthibitisha kujitoa kwa kampuni hiyo katika  kuunga mkono jitihada za wizara husika ya kubadilisha elimu nchini kwa kupitia kujumuishwa kwake katika uwanja wa kidijitali.

"Kupitia uwekezaji wetu wa kijamii, Tigo imekuwa mstari wa mbele katika kukuza sekta ya elimu nchini. Hatufanyi kazi tu na taasisi za elimu ya juu, bali pia tumeshatoa kompyuta na kuunganisha zaidi ya shule 60 za sekondari kwa mtandao wa intaneti wenye  kasi kupitia Mradi wetu wa Shule-elektroniki. Hali kadhalika, Tigo imetoa msaada wa  madawati zaidi ya 7,100 ambayo yamewanufaisha wanafunzi wa shule za msingi zaidi ya  21,000 kote nchini ", alisema Karikari.


Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Makamu Mkuu wa Chuo cha UDOM, Prof. Idriss Kikula  alishukuru Tigo kwa mchango huo akisema; "Ni kupitia ushirikiano huu kwamba tutaweza kutoa stadi za kisasa za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) pamoja na maarifa kwa kizazi cha wataalamu, ili nchi iweze kukidhi mahitaji ya taarifa zinazovbadilika na mtiririko wa kidijitali katika jamii na uchumi wa dunia."
"Ninashukuru Tigo kwa utayari wake katika kushirikiana na chuo chetu ili kuongeza kiwango cha ueledi katika elimu ya kidijitali.  Nakaribisha ushiriki wa wadau wengine katika utengemano wa teknolojia katika kujifunza, " alisema Kikula.
Msaada huo unafuatia mkataba wa makubaliano  uliosainiwa kati ya Tigo na Chuo Kikuu cha Dodoma mwanzoni mwa  mwaka huu, ambapo kampuni hiyo pia imejitolea kutoa kompyuta kwa taasisi hiyo ili iweze kutoa urahisi wa kufikiwa kwa  bidhaa za mtindo wa maisha ya kidijitali za kampuni hiyo.
Mwisho



COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TIGO YATOA MSAADA WA KOMPUTA 47 KWA CHUO KIKUU CHA DODOMA
TIGO YATOA MSAADA WA KOMPUTA 47 KWA CHUO KIKUU CHA DODOMA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEibjpz3ao_Qj61zZmCsHqEW9Zk7514YAGK-5J-f12id08ssM13gO2Mam_i5Ea2ZZ5P69U89XkNQbvRNt8MKj4Dz560JfOHbVOp940DuRsywow8j3aLiaqq2lBrFbCkO62y8EhpVipUWfLk/s640/l-r+UDOM+Deputy+Vice+Chancellor+++DVC-PFA+Prof+Ahmed+Ame%252C+UDOM++DVC-ARC+Prof+Peter+Msoffe%252C+%252C+UDOM+VC+-+Prof+++Idris+Kikula%252C+Tigo+Acting+MD%252C+Mr.+Simon+Karikari%252C+CSR+Mngr+Halima+Okash%252C+++Coprt+Comms+Mngr+Woinde+Shisael.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEibjpz3ao_Qj61zZmCsHqEW9Zk7514YAGK-5J-f12id08ssM13gO2Mam_i5Ea2ZZ5P69U89XkNQbvRNt8MKj4Dz560JfOHbVOp940DuRsywow8j3aLiaqq2lBrFbCkO62y8EhpVipUWfLk/s72-c/l-r+UDOM+Deputy+Vice+Chancellor+++DVC-PFA+Prof+Ahmed+Ame%252C+UDOM++DVC-ARC+Prof+Peter+Msoffe%252C+%252C+UDOM+VC+-+Prof+++Idris+Kikula%252C+Tigo+Acting+MD%252C+Mr.+Simon+Karikari%252C+CSR+Mngr+Halima+Okash%252C+++Coprt+Comms+Mngr+Woinde+Shisael.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/tigo-yatoa-msaada-wa-komputa-47-kwa.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/tigo-yatoa-msaada-wa-komputa-47-kwa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy