F RC MAKONDA AAGIZA CV ZA WATENDAJI KATA DAR KUPITIWA UPYA. | RobertOkanda

Wednesday, August 9, 2017

RC MAKONDA AAGIZA CV ZA WATENDAJI KATA DAR KUPITIWA UPYA.
RC Makonda aagiza CV za watendaji kata za jiji la Dar es Salaam kupitiwa upya hatua hiyo imefuata baada ya Mkuu huyo wa Mkoa D ar es Salaam kufika katika eneo la Bunju B jijini humo kwa maelekezo ya Rais Magufuli aliyetoa siku 4 kutatuliwa kero za eneo hilo.


Katika mkutano na wananchi wa eneo hilo, RC Makonda alilazimika kumuinua mtendaji wa kata hiyo na ndipo alipogundua wengi wao hawaelewi vizuri majukumu yao na ndipo alipomuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kindondoni, Ally Happi kukagua CV za watendaji wake mara moja.


RC Makonda amedai Watendaji hao kutoelewa majukumu yao ndio imekuwa sababu kubwa ya wananchi kushindwa kutatuliwa kero ndogondogo na hatimaye Wanasubiri Rais akipita wanamsimamisha kwa matatizo madogodogo yakiwemo ya Vyoo, Umeme na masoko.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wananchi wa Bunju B juu ya Watendaji wa Kata kutoelewa majukumu yao imekuwa ni sababu kubwa ya wananchi kushindwa kutatuliwa kero zao.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Allya Hapi akizungumza na wanachi wa Bunju B akifafanua jambo katika mkutano huo.

Sehemu ya wanchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii.

0 comments:

Post a Comment