Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ukielekea mkoani Tanga ambako katika ziara yake ya sik...
Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ukielekea mkoani Tanga ambako katika ziara yake ya siku tano ataungana na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda kesho Jumamosi katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la kuanza kwa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima hadi bandari ya Tanga
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Tanga pamoja na maelfu ya wananchi wa Mkata wakati akiwasili mkoani Tanga
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Tanga pamoja na maelfu ya wananchi wa Mkata wakati akiwasili mkoani Tanga.
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefuta umiliki wa mashamba matano yenye jumla ya hekari 14,000 yaliyoshindwa kuendelezwa na wamiliki wake katika Wilaya ya Muheza mkoani Tanga.
Hatua hiyo imechukuliwa na Rais Magufuli wakati akiwahutubia wananchi wa Wilaya hiyo alipokuwa anapita kuelekea Tanga kwa ajili ya shughuli ya uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirishia mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga,Tanzania.
Rais amefuta umiliki huo baada ya baadhi ya wananchi wa wilaya hiyo waliopewa mashamba hayo kwa ajili ya kuwekeza katika miradi mbalimbali ya kilimo ambacho kingeiingizia Serikali mapato, kuyaacha maeneo hayo bila kufanya uwekezaji tarajiwa.
“Tayari nimeshafuta umiliki wa mashamba matano yaliyokuwa yamechukuliwa bila kuendelezwa, nimeyarudisha kwa uongozi wa Mkoa ili wayapange maeneo hayo kwa ajili ya shughuli za Serikali pamoja na kuyagawa kwa wananchi. Nasisitiza wananchi wagaiwe mashamba hayo bure,” alisema Rais Magufuli.
Rais Magufuli ameongeza kuwa ardhi ya mkoa wa Tanga haikupangwa kwa ajili ya wawekezaji bali ni ardhi kwa ajili ya wananchi wote hivyo wana haki ya kupewa bure ardhi hiyo iliyoshindwa kuendelezwa.
Katika safari hiyo ya kuelekea Tanga mabapo alisimama maeneo mbalimbali kuwahutubia wananchi, Rais Magufuli alimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mhandisi Robert Gabriel kwa kutumia vizuri fedha za Serikali kuhamasisha vikundi vya wananchi kujenga madarasa kwa gharama ndogo na kuwataka viongozi wengine kuiga mfano wake.
Alipopewa nafasi ya kuwasalimia wananchi, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema kuwa utekelezaji wa maagizo mbalimbali ya Rais Magufuli unaonesha wazi dhamira yake ya kutaka kuifanya Tanzania kuwa mpya hivyo ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha hamkatishi tamaa Rais Magufuli kwa kufanya kazi kwa bidii.
“Tunampongeza Rais Magufuli kwa juhudi zake za kuibadilisha Tanzania, katika bajeti ya sekta ya afya ya mwaka huu, tumepewa shilingi milioni 650 kwa ajili ya kuimarisha kituo cha afya cha Mkuzi, kikubwa ninaomba mtusaidie kuwaibua wanaouza dawa za Serikali ili tukomeshe tabia hii,” alisisitiza Waziri Ummy.
Baadhi ya maeneo ambayo Rais alisimama kuongea na wananchi wakati akielekea Tanga ni pamoja na Mkata, Michungwani, Hale, Muheza na Mkanyageni.
Rais Magufuli pamoja na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wanatarajiwa kuweka Jiwe la Msingi katika mradi mkubwa wa ujenzi wa bomba la mafuta la kutoka Hoima nchini Uganda mpaka Tanga, Tanzania. Jiwe hilo la msingi litawekwa eneo la Chongoleani lililopo Barabara ya Horohoro kuelekea Mombasa nje kidogo ya jiji la Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia maelfu ya wananchi wa Mkata akiwasili mkoani Tanga
Sehemu ya umati wa wananchi wa Mkata wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Sehemu ya umati wa wananchi wa Mkata wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Sehemu ya umati wa wananchi wa Mkata wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Sehemu ya umati wa wananchi wa Mkata wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Sehemu ya umati wa wananchi wa Mkata wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Sehemu ya umati wa wananchi wa Mkata wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Sehemu ya umati wa wananchi wa Mkata wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Sehemu ya umati wa wananchi wa Mkata wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wananchi Mkata
Sehemu ya umati wa wananchi wa Mkata wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaga baada ya kuongea na wananchi wa Mkata
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa aliposimama kuongea na wananchi eneo la Komkonga
Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama kuongea nao eneo la Komkonga
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wananchi aliposimama eneo la Komkonga
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wananchi aliposimama eneo la Komkonga
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Godwin Gondwe akimshangilia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akiongea na wananchi aliposimama eneo la Komkonga
Wananchi wakiwa na furaha kumuona Rais wao
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza kwa kazi nzuri na ya mfano katika kuendeleza elimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mhe. Robet Gabriel
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza kwa kazi nzuri na ya mfano katika kuendeleza elimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mhe. Robet Gabriel
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Godwin Gondwe akiongea jambo na Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mhe. Robet Gabriel
Wananchi wa Hale wakimsikiliza Rais
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wananchi wa Michungwani
Wananchi wakimshangilia Rais Magufuli
Rais akisalimiana na wananchi wa Kabuku
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia vazi la mwananchi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia vazi la mwananchi
Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ukisimamishwa na maelfu ya wananchi kila alipopita
Wenyeji kwa wageni wakifurahia ujio wa Rais Magufuli
Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ukisimamishwa na maelfu ya wananchi kila alipopita
Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ukisimamishwa na maelfu ya wananchi kila alipopita
Rais Magufuli akiongea na wananchi eneo la Hale
Wananchi wenye furaha wakimsikiliza Rais Magufuli
Wengi walitumia simu zao za mkononi kumrekodi Rais Magufuli
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe January Makamba akiongea
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo alipowasili wilayani humo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Mbunge wa Muheza Mhe. Adadi Rajabu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa kwa shangwe na wananchi wa Muheza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisoma mabango alipowasili wailayani Muheza
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndg. Abdulrahmana Kinana akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Mhe. Henry Shekifu wakati wa mkutano wa hadhara wilayani Muheza
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndg. Abdulrahmana Kinana akiongea katika mkutano wa hadhara wilayani Muheza
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akitambulishwa kwa wananchi wakati wa mkutano wa hadhara wilayani Muheza
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimia wananchi wakati wa mkutano wa hadhara wilayani Muheza
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa meza kuu na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigella wakati wa mkutano wa hadhara wilayani Muheza
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndg. Abdulrahmana Kinana katika mkutano wa hadhara wilayani Muheza
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndg. Abdulrahmana Kinana akiongea na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe January Makamba katika mkutano wa hadhara wilayani Muheza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wananchi wa Muheza
Wananchi wa Muheza wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini Mhe. Stephen Ngonyani aka 'Profesa Maji Marefu' akisalimia wananchi
Mbunge wa Pangani Jumaa Aweso akisalimia wananchi
Mbunge wa Korogwe Mjini Mhe. Mary Chatanda akisalimia wananchi
Mbunge akisalimia wananchi
Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini Mhe Omari Kigoda akisalimia wananchi
Mbunge wa Muheza Mhe. Adadi Rajabu akisalimia wananchi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata picha na baadhi ya viongozi wa Muheza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Profesa Maji Marefu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata picha na baadhi ya watoto waliokuwepo kwenye mkutano wake wa hadhara Muheza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza diwani wa Pongwe Mhe. Mbaraka Saadi Mbaraka akimuelezea changamoto za eneo lake
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza diwani wa Pongwe Mhe. Mbaraka Saadi Mbaraka aliyemuelezea kwa ufasaha changamoto za eneo lake
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsifia diwani wa Pongwe Mhe. Mbaraka Saadi Mbaraka kwa kumuelezea changamoto za eneo lake.
Wananchi na diwani wa Pongwe Mhe. Mbaraka Saadi Mbaraka wakifurahia umauzi wa Rais wa kujengwa kituo cha mabasi eneo lao
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekeza eneo la Pongwe lijengwe kituo cha mabasi na kuitwa jina la diwani wa Pongwe Mhe. Mbaraka Saadi Mbaraka baada ya kufurahishwa na jinsi alivyomuelezea kwa ufasaha changamoto mbalimbali za eneo lake. (Picha zote na IKULU)
COMMENTS