Mama lishe na madereva wa Bodaboda wakizoa mafuta ya kupikia yaliyomwagika kwenye barabara ya mchepuko kando ya Barabara ya Nyerer...
Mama lishe na madereva wa Bodaboda wakizoa mafuta ya kupikia yaliyomwagika kwenye barabara ya mchepuko kando ya Barabara ya Nyerere mkabala na Kiwanda cha Pepsi Cola jijini Dar es Salaam leo alfajiri baada ya gari lililokuwa limebeba mafuta hayo kugongana na gari la mizigo. Wakazi hao wa jijini waliona hiyo ni fursa na kutafuta vyombo mbalimbali huku wakichota mafuta hayo kwa ajili ya matumizi licha ya kuelewa kwamba wanahatarisha afya zao na walaji wao pia. Baadhi yao walikutwa wakichota mafuta yaliyochanganyika na maji kwenye mtaro jambo ambalo ni hatari sana kwa afya. Chini ni picha mbalimbali pamoja na video inayoonesha hali ilivyokuwa. (Picha na Robert Okanda) |
COMMENTS