NEC YAPONGEZWA KWA USIMAMIZI NA MATUMIZI BORA YA RASILIMALI ZA SERIKALI

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani (Kulia) akimweleza jamb...Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi

(NEC) Bw. Kailima Ramadhani (Kulia) akimweleza jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya

Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama

(kushoto) alipotembelea Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi eneo la kuhifadhia

Mashine za BVR. Katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na

Bunge), Maimuna Tarishi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,

Ajira na Watu Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama akitazama moja ya Daftari la Wapiga Kura

alipotembelea Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar es salaam. Katikati

ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani na Kushoto ni Afisa TEHAMA wa

Tume Bi. Mwamvita Solo.
Afisa TEHAMA wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw.

Julius Kobelsiki akitoa ufafanuzi kuhusu Mashine ya kuandikisha Wapiga Kura ya

BVR kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye

Ulemavu
Mhe.

Jenista Mhagama alipotembelea Ofisi za Tume jijini Dar es salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,

Ajira na Watu Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na baadhi ya watendaji na

watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi mara baada ya kuhitimisha ziara yake

katika Ofisi za Tume jijini Dar es salaam. Kulia kwake Katibu Mkuu Ofisi ya

Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Maimuna Tarishi na Mkurugenzi wa Uchaguzi

Bw. Kailima Ramadhani (kulia).
Na. Aron Msigwa - Dar es slaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira

na Watu Wenye Ulemavu


Mhe. Jenista Mhagama ameipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kuendelea kusimamia

matumizi bora ya rasilimali inazopewa na Serikali na kuzitaka taasisi nyingine

za Serikali kuiga mfano huo.

Mhe. Muhagama ameyasema

hayo leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kutembelea ofisi za Tume ya Taifa

ya Uchaguzi kuangalia utekelezaji wa maagizo ya Bunge kupitia Kamati ya Kudumu

ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala Bora iliyoridhia Bunge lipitishe fedha

kiasi cha shilingi bilioni 10 kuiwezesha Tume kufanya maandalizi ya Uboreshaji

wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura nchini .

Akizungumza na watendaji na

baadhi ya watumishi wa Tume amesema kuwa ameridhishwa na utendaji kazi wao na

namna Tume ilivyojipanga kutekeleza jukumu la uboreshaji wa Daftari la Kudumu

la Wapiga Kura kuelekea uchaguzi ujao wa mwaka 2020 kwa kuwa na mpango Kazi,

unaochambua na kubainisha mahitaji muhimu yanayotakiwa, lini na wapi ili kazi

hiyo iweze kufanyika kwa umakini. 

“ Naipongeza sana Tume kwa

kuendelea kufanya vizuri , nimegundua kuwa imejipanga vizuri kutekeleza

majukumu yake ambayo yameainishwa Katika Katiba,  kwa niaba ya Waziri Mkuu nimekuja hapa na timu

ya watendaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kuangalia utekelezaji wa maagizo ya

Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala Bora walioridhia Bunge lipitishe

fedha shilingi Bilioni 10 ili kuiwezesha kufanya maandalizi ya Uboreshaji wa

Daftari la Kudumu la Wapiga Kura” Amesema.

Mhe. Mhagama ameeleza  kuwa kazi hiyo kazi ya utekelezaji wa maagizo

hayo ya Bunge inazingatia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka

1977 Ibara ya 5 kifungu kidogo cha 3 (a) ambacho kimeweka uanzishwaji wa

Daftari la Kudumu la Wapiga Kura nchini na Ibara ya 74 kifungu kidogo cha 6 (a)

na (e) ambacho kinaipa Tume madaraka ya kuchukua jukumu la kuandikisha wapiga

Kura nchini Tanzania.

Aidha, ameongeza kuwa

Sheria ya Uchaguzi kifungu cha 15 (3) kinaipa madaraka Tume ya Uchaguzi  kutengeneza mfumo na utaratibu wa  uandikishaji wa wapiga Kura nchini na

uboreshaji wa daftari hilo mara mbili kati ya Uchaguzi mkuu mmoja na unaofuata.

“Tunaelekea Uchaguzi Mkuu

wa mwaka 2020 kwa hiyo ili tuzingatie takwa la Katiba na takwa la Sheria ya Uchaguzi

ambayo inasimamiwa na Tume ni lazima sasa Serikali ione kwamba inaisaidia Tume

ya Taifa ya Uchaguzi na wote tunajua kuwa utendaji wake ni huru lakini Serikali

tunaowajibu wa kuhakikisha kuwa Tume inafanya kazi yake vizuri” Amesisitiza.

Kwa Upande wake Katibu Mkuu

Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Maimuna Tarishi akizungumza mara

baada ya kumalizika kwa ziara hiyo ameipongeza uongozi wa Tume  kwa kuonyesha mfano katika kuondoa mazoea

katika utendaji kazi ikiwemo utunzaji wa mali na rasilimali za Serikali.

Amesema kuwa Serikali

itaendelea kuijengea uwezo Tume kwa kuipatia rasilimali na vitendea kazi

inavyohitaji ili iweze kutimiza majukumu yake kwa wakati.

Naye Mkurugenzi wa Uchaguzi

wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani akizungumza mara baada ya

kumalizika kwa ziara hiyo amemshukuru viongozi hao kwa kuzitembelea ofisi za

Tume kuangalia maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kuishukuru

Serikali kwa kutenga shilingi Bilioni 10 zitakazotumika kwa ajili ya uboreshaji

huo.COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: NEC YAPONGEZWA KWA USIMAMIZI NA MATUMIZI BORA YA RASILIMALI ZA SERIKALI
NEC YAPONGEZWA KWA USIMAMIZI NA MATUMIZI BORA YA RASILIMALI ZA SERIKALI
https://i.ytimg.com/vi/aGDdFZ6NMwE/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/aGDdFZ6NMwE/default.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/nec-yapongezwa-kwa-usimamizi-na.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/nec-yapongezwa-kwa-usimamizi-na.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy