NAIBU SPIKA AFUNGUA MASHIDANO YA MBIO ZA BAISKELI MKOANI SIMIYU

Mshindi wa tatu mbio za baiskeli kilometa 80 (wanawake), Vumilia Mwinakila kutoka Mkoa wa Simiyu akicheza wimbo wa Kisukuma pam...


PICHA EIGHT
Mshindi wa tatu mbio za baiskeli kilometa 80 (wanawake), Vumilia Mwinakila kutoka Mkoa wa Simiyu akicheza wimbo wa Kisukuma pamoja na  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson baada ya kupokea kitita cha shilingi laki tatu.

PICHA ONE
Naibu Spika wa Bunge la  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson (wa pili kushoto) akimkabidhi ufunguo wa pikipiki mshindi wa kwanza kilometa 200 (wanaume), Hamisi Hussein kutoka Arusha katika mashindano ya Baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi (kulia) ni Mkurugenzi Kampuni ya Jambo Food Products ambayo ni mdhamini, Mhe.Salum Khamis akimpongeza Mshindi huyo
PICHA TWO
Naibu Spika wa Bunge la  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson (mwenye bendera nyeupe kulia) akifungua mashindano ya Mbio za Baiskeli Mkoa wa Simiyu(Simiyu Jambo Festival) kwa kuruhusu washiri kuanza mashindano hayo Mjini Bariadi.
PICHA THREE
Naibu Spika wa Bunge la  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson (mwenye baiskeli wa pili kulia) akiwa na viongozi wa Mkoa na baadhi ya Wabunge wa Mkoa wa Simiyu na Viti Maalum kutoka nje ya Mkoa kwa ajili ya kufungua mashindano ya baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi.
PICHA FOUR
Mkurugenzi Kampuni ya Jambo Food Products, Mhe.Salum Hamis ambaye ndio mdhamini wa mashindano ya baiskeli na ngoma za asili akimkabidhi Mshindi wa kwanza mbio za Kilometa 80 (wanawake) Raulensia Luzuba kutoka mkoani Mwanza zawadi ya shilingi laki tano taslimu.
PICHA FIVE
Rais wa Chama cha Baiskeli Taifa, Godfrey Mhagama akimkabidhi mshindi wa kwanza katika mbio za kilometa 10 (walemavu) katika mashindano ya Baiskeli na ngoma za asili (Simiyu Jambo Festival) yaliyofanyika Mjini Bariadi Simiyu.
PICHA SIX
Naibu Spika wa Bunge la  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akimkabidhi ufunguo wa pikipiki mshindi wa kwanza (wanaume) katika mashindano ya Baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi kilometa 200, Hamisi Hussein kutoka Arusha
PICHA SEVEN
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na washindi watatu wa mbio za Kilometa 10 (walemavu) na viongozi wa Mkoa wa Simiyu na baadhi kutoka nje ya mkoa wa Simiyu, mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya baiskeli na Ngoma za Asili(Simiyu Jambo Festival) Mjini Bariadi.
PICHA NINE
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na washindi watatu wa mbio za Kilometa 80(wanawake) na viongozi wa Mkoa wa Simiyu na baadhi kutoka nje ya mkoa wa Simiyu, mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya baiskeli na Ngoma za Asili(Simiyu Jambo Festival) Mjini Bariadi.
PICHA TEN
Washiriki wa mashindano ya mbio za Baiskeli kilometa 200(wanaume) wakiendelea kuchuana vikali kushindania pikipiki na fedha taslimu
PICHA ELEVEN
Mshindi wa kwanza kilometa 200 (wanaume), Hamisi Hussein kutoka Arusha akipanda kwenye pikipiki yake aliyokabidhiwa baada ya kuibuka mshindi dhidi ya wenzake katika mashindano ya Baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
PICHA TWELVE
Wa pili kutoka kushoto Katibu Tawala mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini, Mbunge wa Busega, Mhe.Raphael Chegeni , Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson wakiwa wamembeba nyoka wa kikundi cha wasanii wa ngoma ya asili ya Kisukuma.
PICHA THIRTEEN
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akimpongeza Bibi.Tatu Malulu kutoka Mwanza kwa kuwa mshindi wa pili mbio za kilometa 80 (wanawake) katika mashindano ya Baiskeli yaliyofanyika Mkoani Simiyu.
PICHA FOURTEEN
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akizungumza na waandishi wa habari katika mahojiano maalum mara baada ya kuwapokea washiriki wa mashindano ya mbio za baiskeli wa makundi yote(wanaume, wanawake na walemavu) yaliyofanyika Bariadi Mkoani Simiyu.
PICHA FIFTEEN
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthny Mtaka akizungumza na waandishi wa habari katika mahojiano maalum mara baada ya kuwapokea washiriki wa mashindano ya mbio za baiskeli wa makundi yote(wanaume, wanawake na walemavu) yaliyofanyika Bariadi Mkoani Simiyu.
PICHA SIXTEEN
Mshindi wa kwanza mbio za baiskeli kilometa 200 (wanaume), Hamisi Hussein kutoka Arusha(mwenye pikipiki) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi  na washindi wenzake, mshindi wa pili Masunga Duba kutoa Simiyu(wa tatu kushoto mstari wa pili) na wa tatu Richard Laizer (wa pili kulia mstari wa pili).
PICHA SEVENTEEN
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson(wa nne kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(wa tatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na mamanju wa vikundi viwili vya ngoma za asili kimoja kinachochocheza na fisi na kingine knacheza na fisi mara baada ya mashindano ya baiskeli na ngoma za asili kumalizika Mjini Bariadi.
PICHA EIGHTEEN
Kikundi cha ngoma ya asili cha Wagalu kikitoa burudani kwa wananchi na viongozi waliofika kushuhudia mashindano ya baiskeli na ngoma za asili (Simiyu Jambo Festival) Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
PICHA NINETEEN
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali pamoja na mamanju wa vikundi vya Wagika na Wagalu Mkoani Simiyu, mara baada ya mashindano ya baiskeli na ngoma za asili kumalizika Mjini Bariadi.
PICHA TWENTHY
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson(kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Kushoto wakiteta jambo wakati wakiwasubiri washiriki wa mashindano ya mbio za baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi, kufika katika kituo cha mwisho.
PICHA TWENTHY TWO
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson(wa tatu kushoto) akicheza pamoja na baadhi ya  viongozi wa Mkoa wa Simiyu na waimbaji kutoka Kata ya Bumela Wilayani Itilima wakati wa kuhitimisha mashindano ya baiskeli na ngoma za asili (Simiyu Jambo Festival) Mjini Bariadi.
PICHA TWENTHY THREE
Baadhi ya wasanii wa Kikundi cha ngoma ya asili cha Wagika wakitoa burudani kwa wananchi na viongozi waliofika kushuhudia mashindano ya baiskeli na ngoma za asili (Simiyu Jambo Festival) Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
PICHA TWENTHY FOUR
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson(wa nne kulia) akicheza pamoja na baadhi ya  viongozi wa Mkoa wa Simiyu na Msanii Elizabeth Maliganya(wa tatu kulia) kutoka Bariadi wakati wa kuhitimisha mashindano ya baiskeli na ngoma za asili (Simiyu Jambo Festival) Mjini Bariadi.
PICHA TWENTHY SIX
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kuhitimishwa kwa mashindano ya mbio za  baiskeli na ngoma za asili (Simiyu Jambo Festival) Mjini Bariadi.
PICHA TWENTHY SEVEN
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akisalimia na Katibu Tawala Wilaya ya Bariadi, Albert Rutaihwa ara baada ya kuwasilis kwa ajili ya kufungua mashindano ya baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi mkoani Simiyu.
…………………………
Na Stella Kalinga, Simiyu
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson amefungua Mashindano ya Mbio za Baiskeli na Ngoma za Asili Mjini Bariadi(Simiyu Jambo Festival) ambayo yamehudhuriwa na Maelfu ya Wananchi wa Mkoa wa Simiyu.
Mashindano hayo ya mbio za baiskeli yamehusisha kilometa 200 wanaume, kilomita 80 wanawake ambapo pia  walemavu waliweza kushindania katika umbali wa kilomita tano.
Akizungumza baada ya kufungua mashindano hayo Dkt.Tulia pamoja na kuupongeza Mkoa wa Simiyu kuandaa mashindano hayo amesema, ipo michezo nchini haijapewa kipaumbele lakini ikitumiwa vizuri inaweza kutoa ajira ukiwemo mchezo wa mbio za baiskeli; ambapo ametoa wito kwa viongozi wa mikoa mingine pia kuwekeza katika michezo mbalimbali ili kuwasaidia wananchi kupata kipato.
“Lililofanyika Simiyu ni jambo jema sasa watu watakuwa wanajua kuwa wakijifua vizuri kwenye baiskeli na ngoma za jadi wanakuja kushiriki mashindano ya Baiskeli Simiyu, nitoe wito kwa viongozi wengine kufikiria mambo mengine yanayoweza kuwasaidia wananchi katika maeneo yao kupata ajira na kujipatia kipato” alisema.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema mkakati wa mkoa huo ni kurasimisha tamaduni zote za Mkoa wa Simiyu na kuhusianisha na shughuli za Utalii ndani ya mkoa huo.
“Position(Nafasi) ya Mkoa wa Simiyu kwenye nchi ni kukuza tamaduni na sanaa zetu kama moja ya eneo litakalotuunganisha na sekta ya Utalii, tumezungukwa na mapori ya akiba na mbuga za wanyama, tungehitaji watalii wanapokuja kwenye maeneo hayo wapate ladha ya tofauti kiwemo utamaduni wa Mtanzania”
Mtaka ameongeza kuwa wasanii wote watatambuliwa na baadae kujengewa uwezo  kupitia watalaam wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(Kitivo cha sanaa),Chuo cha Sanaa Bagamoyo na vyuo vya michezo ili waweze kufanya kazi zao kibiashara na kuimarisha uchumi wao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products,Mhe.Salum Khamis ambaye ndio Mdhamini wa mashindano ya Baiskeli na ngoma za Asili (Simiyu Jambo Festival) amesema ataendelea kudhamini mashindano kama hayo Mkoani Simiyu ili kuwaweseha wananchi kuinua kipato kupitia vipaji vyao.
 Naye mshindi wa kwanza mbio za kilometa 80 (wanawake) Raulensia Luzuba kutoka Mwanza ameomba mashirika na makampuni mbalimbali kuwadhamini ili waweze  kujengewa uwezo na kuandaliwa kushiriki katika mashindano ya Kimataifa.
Masunga Duba mshindi wa mbio za kilometa 200(wanaume)kutoka Simiyu amesema pamoja na wafadhili kudhamini mashindano ameomba pia wawasaidie  wachezaji kupata baiskeli za kisasa zitakazowasaidia kwenda kwa kasi inayotakiwa.
Mashindano ya baiskeli Mkoani Simiyu yameshirikisha wachezaji kutoka mikoa ya Simiyu, Mwanza, Shinyanga,Arusha na Mbeya ambapo ushindi kwa upande wa wanaume umechukuliwa na Hamisi Hussein(Arusha) ambaye amejishindia pikipiki, wa pili ni Masunga Duba(Simiyu) kitita cha shilingi 1,000,000/= wa tatu Richard Laizer .shilingi 500,000/= na zawadi nyingine zimetolewa kwa mshindi wa nne mpaka wa 15.
Kwa upande wa wanawake mshindi wa kwanza  Raulensia Luzuba kutoka Mwanza amejipatia shilingi 500,000/=, mshindi wa pili Tatu Malulu(Mwanza) shilingi 400,000/= na wa tatu ni Vumilia Mwinamila(Simiyu) shilingi 300,000/= na zawadi nyingine zimetolewa kwa mshindi wa nne mpaka wa 10.
Walemavu mshindi wa kwanza Emmanuel Mtemi amejipatia shilingi 200,000/= wa pili Masunga Sendama shilingi 150,000/= na wa tatu Saguda Sospeter shilingi 100,000/=wote kutoka mkoa wa Simiyu na zawadi nyingine zimetolewa kwa mshindi wa nne na wa tano.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: NAIBU SPIKA AFUNGUA MASHIDANO YA MBIO ZA BAISKELI MKOANI SIMIYU
NAIBU SPIKA AFUNGUA MASHIDANO YA MBIO ZA BAISKELI MKOANI SIMIYU
http://fullshangweblog.com/home/wp-content/uploads/2017/08/PICHA-EIGHT.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/naibu-spika-afungua-mashidano-ya-mbio.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/naibu-spika-afungua-mashidano-ya-mbio.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy