MTANDAO WA BARABARA KUU NA MIKOA UMEFUNGUA FURSA ZA UWEKEZAJI NCHINI

Na Ismail Ngayonga MAELEZO DAR ES SALAAM 13.8.2017 TANGU uhuru mwaka 1961 Serikali imeendelea kufanya juhudi za kuimarisha miundo...


Na Ismail Ngayonga
MAELEZO
DAR ES SALAAM
13.8.2017
TANGU uhuru mwaka 1961 Serikali imeendelea kufanya juhudi za kuimarisha miundombinu ya barabara nchini kutokana na umuhimu wa sekta hiyo katika kuchochea ukuaji wa uchumi na maendeleo ya watu.
Jitihada hizo za kuimarisha miundombinu ya barabara zinalenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii, usafirishaji wa pembejeo za kilimo na mazao ya wakulima kufika kwenye masoko kwa wakati.

Barabara ya lami nchini Tanzania

Katika kipindi cha miaka ya 1980-2000 hali ya mtandao wa barabara nchini ilikua mbaya kutokana na barabara nyingi kukosa fedha za ukarabati na matengenezo na hivyo kuwa kikwazo katika juhudi za Serikali za kuvutia wawekezaji nchini.
Barabara zilizokuwa zinajengwa zilikuwa hazifanyiwi matengenezo inavyopaswa na hivyo kufikia kuharibika na kuhitaji ukarabati ili kuzirejesha kwenye hali nzuri. 
Hali hiyo ilipelekea Serikali kupitia ya Wizara ya Ujenzi kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kubuni mikakati ya pamoja itakayowezesha kuboresha sera  za taifa katika sekta ya barabara hususani katika mfumo wa kutoa fedha za matengenezo ya barabara.
Kutokana na umuhimu wa sekta ya barabara katika kuchochea maendeleo ya nchi, mwaka 2000 Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi ilianzisha Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) 
TANROAD ilianzishwa na Serikali ili ikiboresha na kuongeza mtandao wa barabara kwa kuweka mkazo katika ujenzi na ukarabati wa barabara na madaraja ili kuleta uhakika na nafuu ya usafiri na usafirishaji.
Akiwasilisha hotuba ya makadirio ya bajeti ya mapato na matumizi yam waka 2017/18, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa anasema Serikali imeendelea kutekeleza sera ya kuunganisha mikoa yote na nchi zote jirani kwa barabara za lami ambapo jumla ya kilometa 987 na madaraja makubwa mawili yalikamilika kujengwa na kukarabatiwa kwa kiwango cha lami.
Anaitaja miradi iliyokamilika ni pamoja na ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara ya Namtumbo – Kilimansera – Matemanga - Tunduru (km 187.9); Tunduru – Nakapanya – Mangaka (km 137.3) na Mangaka – Mtambaswala (km 65.5) katika Ukanda wa Kusini.
Anasema kuwa kwa upande wa kwa upande wa ukanda wa Kati, Magharibi na Ukanda wa Ziwa miradi iliyokamilika ni ujenzi wa barabara ya Mbeya – Lwanjilo – Chunya (km 72), barabara ya Mwigumbi – Maswa – Bariadi – Lamadi (sehemu ya Bariadi – Lamadi - km 71.8), .
Miradi mingine ni barabara ya Nzega – Puge (km 58.8), barabara ya Sitalike – Mpanda (km 36.9), barabara ya Tabora – Urambo - Ndono (km 94) na barabara ya Kyaka – Bugene – Kasulo (sehemu ya Kyaka - Bugene (km 59.1).
Anaongeza kuwa katika mwaka wa fedha 2016/2017, Serikali kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS) ilipanga kusimamia kazi za ujenzi, ukarabati na matengenezo ya mtandao wa barabara kuu na za mikoa wenye urefu wa kilometa 35,000.
Anaongeza kuwa hadi kufikia Machi 2017 jumla ya kilometa 433 za barabara kuu zilikamilika kujengwa kwa kiwango cha lami, sawa na asilimia 72 ya lengo la kilometa 592 kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
“Aidha, ukarabati wa jumla ya kilometa 77 za barabara kuu kwa kiwango cha lami ulikuwa umekamilika ni sawa na asilimia 52.56 ya lengo la kilometa 146.5 kwa mwaka wa fedha 2016/2017” anasema Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa anasema kwa upande wa barabara za mikoa, jumla ya kilometa 45.52 zilikuwa zimejengwa kwa kiwango cha lami, pamoja na kufanya ukarabati wa kilometa 520.2 za barabara za mikoa kwa kiwango cha changarawe.
Aidha Profesa Mbarawa anasema kwa upande wa matengenezo ya barabara, hadi kufikia Machi 2017 katika barabara kuu, jumla ya kilometa 5,895.31 zilifanyiwa matengenezo ya kawaida, kilometa 1,074.5 zilifanyiwa matengenezo ya muda maalum na sehemu korofi na madaraja 998 yalifanyiwa matengenezo.
Kuhusu udhibiti wa ubora wa barabara nchini, Profesa Mbarawa anasema katika mwaka 2016/17 Serikali iliendelea na kazi ya kudhibiti uzito wa magari ambapo hadi kufikia Machi 2017 jumla ya magari 2,602,400 yalipimwa ambapo kati ya hayo 684,952, sawa na asilimia 30.84, yalikuwa yamezidisha uzito.
“Jumla ya fedha iliyokusanywa kutokana na tozo ya uharibifu wa barabara na malipo ya kupitisha mizigo mipana na isiyo ya kawaida hadi Machi, 2017 ilikuwa ni Tsh Bilioni 4.1” anasema Profesa Mbarawa.

Uimarishaji wa mtandao wa barabara unafanyika wakati tunaimarisha ushirikiano wa nchi zetu za Afrika Mashariki, hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kulinda miundombinu ya barabara hizo ili ziendelee kutengeza ajira na kipato, uboreshaji wa maisha na kupunguza umaskini.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MTANDAO WA BARABARA KUU NA MIKOA UMEFUNGUA FURSA ZA UWEKEZAJI NCHINI
MTANDAO WA BARABARA KUU NA MIKOA UMEFUNGUA FURSA ZA UWEKEZAJI NCHINI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiUF5KgmiSQ03QhpPFHv6cRTlrCtVjhJhjrDG5lG6Y24OSS9bWwA6PWn6KiWvoyI1WEtRjWWrt9WkApzA7CA9d8AnJFk-HzNRN3TZ8SckBlKQUv2gq6fIudg2-JZN0OMBANx6CS2iMJnRI/s640/Road-contractors-Tanzania.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiUF5KgmiSQ03QhpPFHv6cRTlrCtVjhJhjrDG5lG6Y24OSS9bWwA6PWn6KiWvoyI1WEtRjWWrt9WkApzA7CA9d8AnJFk-HzNRN3TZ8SckBlKQUv2gq6fIudg2-JZN0OMBANx6CS2iMJnRI/s72-c/Road-contractors-Tanzania.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/mtandao-wa-barabara-kuu-na-mikoa.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/mtandao-wa-barabara-kuu-na-mikoa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy