MPINA AKUTANA NA KATIBU MKUU WA JUMUIYA YA MADOLA , WAZUNGUMZIA MASUALA YA HIFADHI YA MAZINGIRA NA SULALA LA MABADILIKO YA TABIANCHI YAPEWA KIPAUMBELE

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland akizungumza na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhag...



Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland akizungumza na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Nje ya Ofisi ya Makamu wa Rais Baada ya kumaliza mkutano ulohusu suala zima la usimamizi na Utunzaji wa Mazingira.


Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland akiongea jambo na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, baada ya mkutano uliofanyika katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaan Leo.

Mhe. Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza AshaRose Migiro, akizungumza baada ya kikao na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland alipofanya mazungumzo na Naibu Waziri Mpina na wataalaam kuhusu masuala ya Mazingira, Ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.
Picha ya Pamoja, ikimuonyesha Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina na wajumbe walioshiriki mkutano wa masuala ya hifadhi ya mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam leo.

Picha ya Pamoja, ikimuonyesha Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina.


Kushoto Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akiongea na Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Mhe. AshaRose Migiro baada ya kumaliza mazungumzo yaliyoohusu masuala ya mazingira.

………………………………………………………………..

Katibu wa Jumuiya ya madola Mhe. Patricia Scotland amefanya mazungumzo na Naibu Waziri Ofisi ya Mkamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga kuhusu suala zima la Hifadhi na usimamizi wa Mazingira huku eneo la mabadiliko ya Tabianchi likipewa kipaumbele.

Katika mazungumzo hayo Bi. Scotland alisema kuwa kuna kila sababu ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kuelewa zaidi suala zima la mabadiliko ya tabianchi akieleza kuwa wanasayansi wanasema ifikapo mwaka 2050 dunia inaweza kabisa kuepukana na suala la athari kubwa za mabadiliko ya tabianchi endapo itawezekana kulifanyia kazi kwa pamoja.

Kwa upande wake Naibu Waziri Mpina alieleza kuwa Tanzania imeathiriwa na mabadiliko ya tabianchi katika sekta mbalimbali na jitihada zimefanyika katika kuwezesha jamii kuhimili na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Alisema serikali inatekeleza Mkakati wa Mabadiliko ya Tabianchi (2012) ambapo sekta za kilimo, mifugo, uvuvi, nishati zimeandaa na zinatekeleza mpango kazi wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi katika maeneo yao.

Aidha, Mhe. Mpina alipokumbushwa kuhusu jitihada zake zinazoonekana wazi katika suala zima la utunzaji wa mazingira hususan katika oparasheni zake za viwandani, na Balozi Migiro; Mpina alisema kuwa viwanda vingi nchini alivyovipitia havina mifumo ya kisasa ya kutibu majitaka akitolea mfano wa jiji la Dar es Salaam Mpina lisema mfumo wa majitaka katika jiji hilo kwa sasa ni asilimia 13% tuu ndiyo yenye mfumo mzuri na kuongeza kuwa asilimia iliyobakia haijakaa vizuri, jambo ambalo si salama kwa viumbe hai na mazingira.

Awali, akiongea katika mkutano huo, Balozi wa Tanzania nchini Uingerea Mhe. Asharose Migiro akitolea mfano wa athari za mabadiliko ya tabia nchi katika maeneo ya ufukwe ya ocean road ambayo imelika, alisema wakati umefika sasa kwa Tanzania kuonyesha ushirikiano katika suala hili na wananchi kuelewa shughuli za kibinadamu zinazochangia kuongeza athari za mabadiliko ya tabianchi.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Amefanya mazungumzo hayo leo na Naibu waziri Mpina na Team ya wataalam baada ya kutembelea kisiwa cha Zanzibar.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MPINA AKUTANA NA KATIBU MKUU WA JUMUIYA YA MADOLA , WAZUNGUMZIA MASUALA YA HIFADHI YA MAZINGIRA NA SULALA LA MABADILIKO YA TABIANCHI YAPEWA KIPAUMBELE
MPINA AKUTANA NA KATIBU MKUU WA JUMUIYA YA MADOLA , WAZUNGUMZIA MASUALA YA HIFADHI YA MAZINGIRA NA SULALA LA MABADILIKO YA TABIANCHI YAPEWA KIPAUMBELE
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjBLhfvQJmLBjVigwU9SQDHwius0uhlPpXFV3dlhWb_i6mcNQ2A6gYYH-HDOaTEIf9dSMCBwRKZFgkGRQqv19RPcufM5i3-dHiAaXq8ung7-qgrW8mrq_CrrihVVepg7tidekvhD6aVcdw/s640/DSC_0052-1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjBLhfvQJmLBjVigwU9SQDHwius0uhlPpXFV3dlhWb_i6mcNQ2A6gYYH-HDOaTEIf9dSMCBwRKZFgkGRQqv19RPcufM5i3-dHiAaXq8ung7-qgrW8mrq_CrrihVVepg7tidekvhD6aVcdw/s72-c/DSC_0052-1.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/mpina-akutana-na-katibu-mkuu-wa-jumuiya.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/mpina-akutana-na-katibu-mkuu-wa-jumuiya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy