MHANDISI LWENGE: HAKUNA MUDA UTAKAO ONGEZWA MSIPOKAMILISHA MRADI KWA WAKATI

NA FRANK SHIJA – MAELEZO Mkandarasi anayejenga mradi wa ujenzi wa miundombinu ya ugawaji maji Dar es Salaam na Pwani atakiwa kukamilisha mra...







NA FRANK SHIJA – MAELEZO
Mkandarasi anayejenga mradi wa ujenzi wa miundombinu ya ugawaji maji Dar es Salaam na Pwani atakiwa kukamilisha mradi huo kwa wakati kulingana na makubaliano yaliyopo ndani ya mkataba.


Agizo hilo limetolewa jana na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo ambapo alitembelea kazi ya ulazaji wa mabomba katika eneo la Kibamba na Hondogo, Kituo cha kusukuma maji Makongo Juu, ujenzi wa matanki ya maji maeneo ya Changanyikeni, Mabwepande na Bagamoyo.


“ Nimeona mkandarasi sasa hivi anaenda vizuri, na niseme tu kazi hii ikamilike kama kama ilivyo katika mkataba sitaongeza muda, hivyo ifikapo tarehe 16, Novemba 2017 mradi huu uwe umekamilika” alisema Mhandisi Lwenge.


Mhandisi Lwenge amesema kuwa mradi huu ni muendelezo wa kuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma ambapo watu zaidi ya wakazi laki tano wa maeneo ya Jiji la Dar es Salaam na Pwani watanufaika baada ya mradi huu kukamilika.


Mhandisi Lwenge amesema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha Wananchi wake wanaondokana na adha ya ukosefu wa huduma ya maji katika maeneo wanayoishi ili waweze kujikitika katika kufanya kazi.


Aidha Mhandisi Lwenge aalisema kuwa ameridhishwa na kasi ya maendeleo ya ujenzi wa mradi huo na kumtaka Mkandarasi wa mradi huo kuhakikisha mradi huo unakamilika ifikapo tarehe 16 Novemba mwezi 2017 kama ilivyo katika makubaliano.


Awali akitoa maelezo ya mradi huo, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasa) Mhadisi Romanus Mwang’ingo amesema kuwa Mradi wa Usambazaji wa Maji Safi Dar es Salaam na Pwani unahusishaujenzi wa matenki tisa (9) ya kusambaza na kuhifadhi maji yenye ukubwa wa kuhifadhi lita milioni 3 hadi 6, ujenzi wa vituo vinne (4) vya kusukuma maji, ununuzi na ufungaji wa Pampu kubwa za kusukuma maji 16, ununuzi wa transfoma na ufungaji njia za umeme wa msongo mkubwa, ununuzi na ulazaji wa mabomba makubwa ya ugawaji maji na ulazaji maji wa mabomba ya usambazaji maji mtaani yatakayokuwa na urefu wa jumla ya kilometa zipatazo 477.


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majjid Mwanga ameipongeza Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasa) kwa jitihada zake za kutatua changamoto za upatikanaji wa maji safi kwa wananchi wa wilaya yake.
“ Kipekee kabisa kwa niaba ya wananchi wa Bagamoyo niseme tu mradi huu wa tenki la ujazo wa lita 6Milioni changamoto ya maji itabaki kuwa historia kwani tutaachana na utumiaji wa miundombinu ya zamani” alisema Majjid.
Naye Mhandisi Mkazi wa Kampuni ya Jane Construction ambao ndiyo mkandaarasi mkuu wa mradi huo Bw. Ashish Srivagtava amemshukuru Waziri kwa kutembelea na kujiongena mradi huo na kuahidi kuwa mradi huo utakamilika kwa wakati kama ambavyo Waziri ameelekeza.
Katika ziara hiyo ya kukagua mradi wa usambazaji maji safi Dar es Salaam na Pwani waziri alitembelea kazi ya ulazaji wa mabomba katika eneo la Kibamba na Hondogo, Kituo cha kusukuma maji Makongo Juu, ujenzi wa matanki ya maji maeneo ya Changanyikeni, Mabwepande na Bagamoyo.


Maeneo yatakayo nufaika na mradi huu ni pamoja na Salasala, Bunju, Wazo, Makongo, Changanyikeni, Bagamoyo, Mpiji, Zinga, Kitope, Ukuni, Kerenge, Buma, Mataya na ukanda maalum wa EPZA ambayo ni maeneo yanayo hudumiwa na mtambo wa Ruvu chini. Ambayo ni maeneo mengine yatakayo nufaika na mradi huu ni yale yaliyopo kati ya Mbezi luisi na kiluvya, ambayo ni Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Msakuzi, Makabe, Malamba mawili na Msigani. Maeneo haya huhudumiwa na mtambo wa ruvu juu ambao ulizinduliwa na mh,Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Juni 21,2017.
Mradi wa usambazaji wa maji safi Dar es Salaam na Pwani unatekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasa) ulianza tangu mwezi Machi 2016 na unatarajiwa kukamilika tarehe 16, Novemba, 2017 unathamani ya shilingi bilioni 72 ambazo ni mkopo nafuu kutoka India, nchi mshirika wa maendeleo.


Baadhi ya mafundi wakiwa wanalaza bomba la maji kama walivyokutwa na mpiga picha wetu wakati wa ziara ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa ugawaji wa maji safi Dar es Salaam na Pwani


Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Majjid Mwanga akielezea jambo mbele ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge (watatu kutoka kushoto) wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa ugawaji wa maji safi Dar es Salaam na Pwani jana. Kushoto kwa Waziri ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasa) Romanus Mwang’ingo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto).



Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasa) Romanus Mwang’ingo kuhusu ujenzi wa tanki la maji wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa ugawaji wa maji safi Dar es Salaam na Pwani jana. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Maji Safi Dar es Salaam (Dawasco) Mhandisi Cyprian Luhemeja.



Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge akipewa maelezo kuhusu ujenzi wa tanki la maji wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa ugawaji wa maji safi Dar es Salaam na Pwani.



Baadhi ya mafundi wakiwa wanalaza bomba la maji kama walivyokutwa na mpiga picha wetu wakati wa ziara ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa ugawaji wa maji safi Dar es Salaam na Pwani




Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge akiangalia mashine inayotumiwa katika ujenzi na ulazaji wa mabomba ya maji alipotembelea eneo la Kibamba na Hondogo ambapo ulazaji huo wa mabomba unaemndelea ikiwa ni utekelezaji wa mradi mkubwa wa ugawaji wa maji safi Dar es Salaam na Pwani.


.(PICHA ZOTE NA: FRANK SHIJA – MAELEZO)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MHANDISI LWENGE: HAKUNA MUDA UTAKAO ONGEZWA MSIPOKAMILISHA MRADI KWA WAKATI
MHANDISI LWENGE: HAKUNA MUDA UTAKAO ONGEZWA MSIPOKAMILISHA MRADI KWA WAKATI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjpbc2PCrHMf7gtIF9UiW9n6gJJPGOuzsAwCpYE2rU4v9FwCFlwThGcC2-FQX2MghT7IRZ9MSXhtoSqrqeb9IhuKIcuRTYGtokzt02_Li-_KNXPxvlGyLwN0WmpphI0empJUeHUDFVVPmE1/s640/PIX3b.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjpbc2PCrHMf7gtIF9UiW9n6gJJPGOuzsAwCpYE2rU4v9FwCFlwThGcC2-FQX2MghT7IRZ9MSXhtoSqrqeb9IhuKIcuRTYGtokzt02_Li-_KNXPxvlGyLwN0WmpphI0empJUeHUDFVVPmE1/s72-c/PIX3b.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/mhandisi-lwenge-hakuna-muda-utakao.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/mhandisi-lwenge-hakuna-muda-utakao.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy