F MAKAMU WA RAIS MHESHIMIWA SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI MKOANI LINDIMAKAMU WA RAIS, MAMA SAMIA AWASILI MKOANI LINDI; KUFUNGA MAONESHO YA NANE NANE KUSHO AGOSTI 8 | RobertOkanda

Monday, August 7, 2017

MAKAMU WA RAIS MHESHIMIWA SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI MKOANI LINDIMAKAMU WA RAIS, MAMA SAMIA AWASILI MKOANI LINDI; KUFUNGA MAONESHO YA NANE NANE KUSHO AGOSTI 8NA OMR, LINDI
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Lindi na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambi.
Makamu wa Rais amewasili mkoani Lindi tayari kwa kuhudhuria kilele cha sherehe za  siku ya Wakulima (Nane Nane) ambapo kitaifa zinaadhimishwa mkoani Lindi.
Katika Uwanja wa ndege wa kikwetu Lindi, Makamu wa Rais pia alipokelewa na Viongozi wa Chama na Serikali pamoja na Vikundi vya ngoma ambavyo vilimlaki kwa nyimbo mbali mbali.
Kesho siku ya Kilele cha sikukuu ya Wakulima (Nane Nane), Makamu wa Rais  atapata fursa ya kutembelea mabanda yakiwemo ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi katika maonesho hayo kwenye viwanja vya Ngongo kisha kuhitimisha kwa kuhutubia Wananchi  kwenye maonesho hayo.

 Makamu wa Rais akisalimiana na Mbunge wa Mtama, Mhe. Nape Nnauye


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea taarifa ya mkoa wa Lindi inayosomwa naMkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambi mara baada ya kuwasili mkoani Lindi tayari kwa kuhudhuria kilele cha sherehe za wakulima (Nane Nane). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi, alipowasili mjini humo leo Agosti 7, 2017.

0 comments:

Post a Comment