MAKAMU WA RAIS AWATAKA WAKAZI WA KIZIMKAZI KUWA NA BIMA YA AFYA

 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa mkono wa pongezi kijana aliyeshinda kwenye mashindano ya Ngalawa Bw. Ali Khami...


 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa mkono wa pongezi kijana aliyeshinda kwenye mashindano ya Ngalawa Bw. Ali Khamisi Mgeni akiwa na chombo chenye jina la Sea Never Dry.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria ufunguzi wa jingo la Mkombozi Saccos lililpo Kizimkazi Dimbani wakati wa Sherehe za Siku ya Wakizimkazi.

 Viongozi na Wageni mbali mbali walijumuika kula chakula cha asili cha Wakizimkazi wakati wa shrehe ya Siku ya Wakizimkazi.
 Mashindano ya kukuna nazi yawa kizutio wakati wa Sherehe za Siku ya Wakizimkazi.
 Mashindano ya kusokota kamba 
Vijana kutoka Kusini mwa Kizimkazi wakivuta kamba wakishindana na vijana wa kaskazini wakati wa sherehe za Siku ya Wakizimkazi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa Sherehe za Siku ya Wakizimkazi iliyofanyika kwenye uwanja wa Maulid, Kizimkazi, Wilaya ya Kusini mkoa wa Kusini, Unguja. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Bw. Sudi Simba ambaye alifika Kizimkazi kutambulisha huduma ya bima ya Afya ya Afya Wote wakati wa Sherehe za Siku ya Wakizimkazi iliyofanyika kwenye uwanja wa Maulid, Kizimkazi, Wilaya ya Kusini mkoa wa Kusini, Unguja.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia vipeperushi vyenye taarifa ya huduma ya bima ya Afya ya Afya Wote wakati wa Sherehe za Siku ya Wakizimkazi iliyofanyika kwenye uwanja wa Maulid, Kizimkazi, Wilaya ya Kusini mkoa wa Kusini, Unguja

 Wakazi wa Kizimkazi wakiangalia ngalawa 15 zikichuznz vikali ikiwa sehemu ya sherehe ya siku ya Wakizimkazi
 Wananchi wakimpokea mshindi wa pili katika mashindano ya Ngalawa kijana Ahmed Yusufu Hassan ambaye ngalawa yake ameipa jina la Ndio Mambo


                           NA MWANDISHI MAALUM
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewahimiza wakazi wa Kizimkazi  kujiandikisha Bima ya Afya kwani ndio mfumo ambao utawawezesha kupata matibabu haraka na kwa gharama ndogo.
Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati  wa Sherehe ya  Siku ya Wakizimkazi ambapo siku hiyo wakazi hao hukutana na kupeana taarifa za maendeleo na kupanga mipango ya baadae kasha kula chakula cha asili pamoja na michezo ya asili.
Mhe. Samia aliwaeleza wananchi hao kuwa hakutokuwa na mjomba atakayekuja kuwaletea maendeleo na alihimiza kwa kusema “Maendeleo ya Kizimkazi yataletwa na Wakizimkazi wenyewe”.
Katika Sherehe hizo Makamu wa Rais alifungua jengo la Ofisi ya Saccos ya Mkombozi lililopo Kizimkazi Dimbani na Kukagua maendeleo ya Ukumbi wa Skuli ya Sekondari Kizimkazi.
Mchezo wa Kuvuta ,kusokota kamba, kukuna nazi na mbio za Ngalawa zilionekana kuvutia watu wengi.
Makamu wa Rais alihimiza wanamichezo kujitokeza kwa wingi mwakani kwani michezo hudumisha umoja  na kuleta mshikamano katika jamii.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAKAMU WA RAIS AWATAKA WAKAZI WA KIZIMKAZI KUWA NA BIMA YA AFYA
MAKAMU WA RAIS AWATAKA WAKAZI WA KIZIMKAZI KUWA NA BIMA YA AFYA
https://4.bp.blogspot.com/-MxJisfyMO-g/WY8Y0dXsLbI/AAAAAAAA2rA/_XVn8_sOojIsOWECNDChsleRLjC8QDRRwCLcBGAs/s640/63.jpg
https://4.bp.blogspot.com/-MxJisfyMO-g/WY8Y0dXsLbI/AAAAAAAA2rA/_XVn8_sOojIsOWECNDChsleRLjC8QDRRwCLcBGAs/s72-c/63.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/makamu-wa-rais-awataka-wakazi-wa.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/makamu-wa-rais-awataka-wakazi-wa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy