Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete wakisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa katika mazishi ya bilione...
Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete wakisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa katika mazishi ya bilionea Maleu Mrema Agosti 9 nje kidogo ya jiji la Arusha katika hoteli ya Ngurudoto
Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la Bilionea marehemu Maleu Mrema katika ibada ya mazishi yaliyofanyika jana katika hoteli yake ya Ngurudoto iliyopo nje kidogo ya jiji la Arusha.
Waziri Mkuu mstaafu,Edward Lowassa akiweka shada la maua pamoja na mke wake katika mazishi ya bilionea Maleu Mrema jana nje kidogo ya jiji la Arusha katika hoteli ya Ngurudoto
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Mrema katika ibada ya mazishi yaliyofanyika katika hoteli yake ya Ngurudoto iliyopo nje kidogo ya jiji la Arusha
Baadhi ya wake za marehemu wakiweka udongo katika kaburi la mpendwa wao
Waziri Mstaafu wa mambo ya nje Bernard Membe akiweka shada la maua katika kaburi la Bilionea Mrema
Meneja mahusiano Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) Pascal Shelutete akiweka shada la maua katika kaburi la Bilione Mrema
Watoto wa marehemu wakiwa wamebeba mashada ya maua
Baadhi ya wanakamati wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Mrema kuelekea katika eneo maalumu lililotengwa na familia kwaajili ya maziko.
Hapa watoto wakiwa wanaweka udongo katika kaburi la baba yao.
Wake wa marehemu wakiwa wanaingia katika eneo maalumu lililotengwa kwaajili ya maziko
Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo pamoja naAbdulrahman Omari Kinana wa Katibu Mkuu wa CCM (kushoto) katika msiba wa Mrema.
Wake wa marehemu Mrema wakiwa katika huzuni. Kulia ni baba mzazi wa Bilionea huyo.
Mh Abdulrahman Omari Kinana Katibu Mkuu wa CCM akitoa heshima zake.
Jeneza la marehe Bilionea Maleu Mrema likiwa linashushwa kaburini.
Wanafamilia wakiwa katika picha ya pamoja na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete. Pamoja nao ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
Mwonekano wa kaburi baada ya mazishi ya Maleu Mrema. (PICHA NA PAMELA MOLLEL)
COMMENTS