KAMPUNI YA NETWORK LTD YAZINDUA DROO KUBWA YA MILIONI 60

Mratibu wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Sebastian Maganga akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo Pichani) kuhusiana na mchezo...Mratibu wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Sebastian Maganga akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo Pichani) kuhusiana na mchezo wa bahati nasibu ya Tatu Mzuka, wakati wa uzinduzi wa mchezo huo wa kubahatisha nchini mapema jijini Dar es Salaam (Picha na Imma Matukio Blog)

Na Mwandishi Wetu

Tatu Mzuka ni mchezo mpya wa jackpot uliobuniwa mahsusi kubadilisha maisha ya watu. Tatu Mzuka ni rahisi kucheza kwa kutumia simu ya mkononi, na kushinda ni baada ya kila lisaa limoja baada ya kucheza.Kucheza Tatu Mzuka unahitaji kuchagua namba zako tatu za bahati, kati ya 0 na 9 kwa kufanya muhamala kwenye simu ya mkononi, linganisha namba mbili ili kujiongezea nafasi ya kushinda mara mbili, au linganisha namba tatu na ushinde mara 200.Akieleza sababu ya kutumia namba tatu, Mratibu wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Sebastian Maganga alisema, “tumezungukwa na namba,, inaweza kuwa siku yako ya kuzaliwa, namba ya jezi ya mchezaji unayempenda au kumbukumbu yoyote hivyo tunaamini kila mtu anazo namba angalau tatu za bahati, sasa fikiria kutumia namba yako ya bahati kujishindia mamilioni ya fedha.”

Balozi wa Tatu Mzuka, Mussa Hussein akitambulisha Tatu mzuka kwa waandishi wa habariUnaweza kubeti kuanzania Tsh 500 mpaka Tzsh 30,000 na kujiwekea
nafasi ya kushinda mpaka Tzsh milioni 6 ndani ya lisaa. Kubeti na Tatu
Mzuka ni kupitia huduma za fedha kwa njia ya mtandao, hivyo hutahitaji
kufanya usajili wowote. Fedha utakazoshinda pia zitatumwa moja kwa moja
kwenye simu yako.“Kila unapobeti unaingia moja kwa
moja kwenye droo ya wiki iitwayo Mzuka Jackpot, na droo hii inakupa
nafasi ya kuwa milionea, hivyo basi kwa kila Tzsh 500 unayobeti kwenye
Tatu Mzuka, unapata nafasi moja ya kuingia kwenye droo ya Mzuka
Jackpot,” alieleza Maganga.Aliongeza kuwa, kila
ticket ya Tatu Mzuka inakuwa na viashiria vyenye herefu 6 zanazokuingiza
kwenye droo ya Jackpot, hivyo ukibeti Tzsh 500, herufi zako zinaingizwa
kwenye droo mara tatu, hivyo kukuongezea nafasi ya kushinda.Muwakilishi
kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Daniel Wilson amewasihi
watanzania kushiriki kwenye Tatu Mzuka na kuwa na nafasi ya kubadilisha
na kuboresha maisha yako. Sera ya Tatu Mzuka ni uwazi, hivyo kila
ushindi wa washiriki utachapishwa kwenye tovuti ya Tatu Mzuka (www.tatumzuka.co.tz).Droo
ya Jackpot itafanyika kila Jumapili na kurushwa moja kwa moja na vituo
vya televisheni vya TV1 na Clouds TV saa 3 kamili usiku na kutangazwa na
mtanganzaji mashuhuri Mussa Hussein akiambatana na Antu Mandoza. Kila
mshindi atakua na uhakika wa kushinda kati ya Tzsh milioni 2 na milioni
6, pamoja na kupata nafasi ya kujishindia milioni 30. Iwapo hakuna
atakayeshinda milioni 30, basi wiki inayofata, kitita cha Mzuka Jackpot
kitaongezeka mara mbili yake na kuwa milioni 60.Ndani
ya wiki moja tu tangu kuanza kwa Tatu Mzuka, wameshapatikana washindi
zaidi ya 40,000, na kulipwa kiasi cha Tzsh milioni 100 kwa pamoja. Beti
na Tatu Mzuka sasa upate nafasi ya kushinda Tzsh milioni 60 Jumapili
hii.

 Mmoja wa waandishi wa habari akishiriki katika droo ya Tatu Mzuka wakati wa uzinduzi

 Balozi wa Tatu Mzuka, Shilole akishiriki katika mchezo huo wa kubahatisha mapema leo

 Baadhi ya Waandishi wa Habari waliokuwepo katika shughuli ya uzinduzi wa mchezo wa kubahatisha wa Tatu Mzuka mapema leo katika hoteli ya SerenaOn Thursday, May 18, 2017 12:11 PM, khalfan said wrote:


Habari ya saa wadau, pokeeni codes

MWALIMU COMMERCIAL BANK PLC (MCB), YAZINDUA KAMPENI YA WEKA AKIBA NA USHINDE, WATEJA KUONDOKA NA IPADS Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank PLC, Bw. Ronald Manongi, (katikati), akiwa na Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko, Bw. Valence Luteganya, (kulia) na Meneja Masoko, Bi. Rahma Ngassa, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 18, 2017.NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
MWALIMU
Commercial Bank PLC imezindua kampeni  ya
“Weka Akiba na Ushinde” kwa Wateja wake na wananchi kwa ujumla.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam leo Mei 18, 2017 wakati akizindua kampeni hiyo, Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank PLC, Bw. Ronald Manongi alisema, “Draw
hiyo ipo wazi kwa wateja wote waliopo na watakaojiunga na sifa kubwa ya kuingia
kwenye draw hiyo ni kwa mteja aliyepo au anayejiunga, kuweka akiba ya Shilingi
50, 000 au zaidi.” Alisema Bw. Manongi.
Akifafanua
zaidi Afisa huyo Mtendaji Mkuu wa benki hiyo alisema, kampeni hiyo ambayo
itawawezesha wateja kupata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali kila mwezi
kwa kipindi cha miezi miwili.
“Mteja
anapoweka akiba (fedha), kiasi cha Shilingi 50,000 au zaidi, atapata alama,
(Point) moja itakayomuwezesha kushiriki kwenye draw.” Alisema.
Alisema,
kadiri Mteja anapoweka akiba zaidi ndivyo Anavyojiwekea nafasi nzuri ya
kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo IPADS na vocha za manunuzi zenye thamani ya
Shilingi 100,000 na kwamba kila itakapochezeshwa draw hiyo, washindi wanane (4)
na kujishindia zawadi mbalimbali.
Akielezea hudma za benki hiyo, Bw.Manongi alifafanua
kuwa  Mwalimu Commercial Bank inatoa
gharama nafuu na rafiki za kibenki na ni suluhisho la kifedha kwa walimu,
watumishi wa serikali na wananchi kwa ujumla na kutoa wito kwa Wateja wapya kuja
kufungua Akaunti na kuweka akiba ili wapate nafasi ya kuingia kwenye draw hiyo.
Naye Mkuu wa kitengo cha Biashara na Masoko wa Benki
hiyo, Bw. Valence Luteganya alisema, “Huduma za kibenki za MCB ni bora na  nafuu, tunawahakikishia wateja wetu waje
kufanya maamuzi ya kifedha yaliyo sahihi kwani tunatoa huduma mbalimbali za
kibenki zilizo nafuu.” Alisema na kuongeza kuwa MCB pia inatoa huduma za ATM
zilizounganishwa na mtandao wa Umoja switch ambao una ATM zaidi ya 200 nchi
nzima.
“Lakini si hivyo tu pia huduma bora za kibenki kupitia
simu za mkononi (Mobile Banking), huduma ya bure ya ujumbe wa SMS ukiwa na
usalama na kuwawezesha wateja kupata taarifa za mara kwa mara kuhusiana na
Akaunti zao. Hivyo natoa wito kwa wananchi kwa ujumla kuja na kujiunga na Benki
yetu kwa huduma bora na za uhakika.” Alisema.
   
 Bw. Manongi akizungumzia kampeni hiyo
 Mkuu wa kitengo cha Biashara na Masoko wa Benki
hiyo, Bw. Valence Luteganya, akifafanua jinsi kampeni hiyo itakavyofanyika


 Meneja Masoko wa benki hiyo, Bi. Rahma Ngassa,(kushoto), akizungumzia ubora wa huduma za kibenki kwenye benki hiyo. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa MCB, Bw. Manongi
 Mkutano ukiendelea
 Waandishi wa habari wakiwa kazini
 Bw. Manongi akisikiliza maswali ya waandishi
 Bw. Manongi, (kushoto), akiwa na Bw.Luteganya

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: KAMPUNI YA NETWORK LTD YAZINDUA DROO KUBWA YA MILIONI 60
KAMPUNI YA NETWORK LTD YAZINDUA DROO KUBWA YA MILIONI 60
https://1.bp.blogspot.com/-4FmTU1UF4s8/WYweLhqJ5uI/AAAAAAAAQew/x_lXat9aPFQy5bhipBdHCcL6uuSArnfXACLcBGAs/s400/_MG_3694.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-4FmTU1UF4s8/WYweLhqJ5uI/AAAAAAAAQew/x_lXat9aPFQy5bhipBdHCcL6uuSArnfXACLcBGAs/s72-c/_MG_3694.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/kampuni-ya-network-ltd-yazindua-droo.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/kampuni-ya-network-ltd-yazindua-droo.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy