JAFO: HILI NI DAMPO LA MFANO

Kazi ya utupaji taka na ushindiliaji taka ikifanyika ndani ya Dampo la kisasa la Chidaye.  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisem...


Kazi ya utupaji taka na ushindiliaji taka ikifanyika ndani ya Dampo la kisasa la Chidaye. 



Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua eneo la Dampo la Chidaye 
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza mara baada ya kukagua Dampo la Chidaye.

……………………. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo ameipongeza Manispaa ya Dodoma kwa usimamizi mzuri wa miradi inayo tekelezwa na Ofisi ya Rais Tamisemi katika Manispaa hiyo ikiwemo kufanikisha ujenzi wa miundombinu ya barabara za lami pamoja na ujenzi wa Dampo la kisasa. 

Naibu Waziri Jafo aliimwagia sifa Halmashauri hiyo kwa usimamizi mzuri uliofanikisha ujenzi huo licha ya kuanza kutumika tangu mwezi Februari mwaka huu. 

“Pamoja na kutumika tangu mwezi Februari lakini hakuna chembe ya harufu wala inzi ukilinganisha na madampo mengine hapa nchini,”amesema Jafo 

Amependezwa na mfumo mzima uliotumika katika ujenzi wa Dampo hilo ambalo ni miongoni mwa madampo kadhaa yanayo jengwa na Tamisemi katika miji mbalimbali hapa nchini kwa fedha kutoka Benki ya dunia. 

Jafo amewataka wataalam wengine kutoka miji mbalimbali kuja kujifunza ili maeneo yote yanapojengwa madampo hayo waige mfano mzuri wa Dodoma. 

Jafo ameutaka uongozi wa jiji la Dar es salaam pamoja na manispaa zake kuja Dodoma kujiongezea maarifa wakati wanajiandaa kujenga miradi kama hiyo katika jiji hilo kupitia mradi wa Dar es salaam Metro Politant Development Project (DMDP) ulio chini ya Ofisi ya Rais Tamisemi. 

Naibu Waziri Jafo amewataka wanadodoma kutunza miundombinu hiyo ambayo serikali inaingia gharama kubwa kuijenga. 

Dampo hilo linatarajiwa kutumika kwa zaidi ya miaka 19 kuanzia sasa.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: JAFO: HILI NI DAMPO LA MFANO
JAFO: HILI NI DAMPO LA MFANO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiYkxISvlvgQobqKXJoocKndBi-I0Nqld-Qgwgfjgl0J-7ITm1yJ2pat7-yTFhakWxBR_NAf472qa6fTSiMtqRv1AwbX0wxZszVPI5m8-q7EaSurggDeXP5PSbX1D0SWHHvlctt_TtIe7Y/s640/dampo-2.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiYkxISvlvgQobqKXJoocKndBi-I0Nqld-Qgwgfjgl0J-7ITm1yJ2pat7-yTFhakWxBR_NAf472qa6fTSiMtqRv1AwbX0wxZszVPI5m8-q7EaSurggDeXP5PSbX1D0SWHHvlctt_TtIe7Y/s72-c/dampo-2.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/jafo-hili-ni-dampo-la-mfano.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/jafo-hili-ni-dampo-la-mfano.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy