DKT. MWAKYEMBE: MCL ENDELEENI KUSIMAMIA MAADILI NA KUHABARISHA JAMII.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uchap...



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uchapishaji Magazeti ya Mwananchi Communications Ltd (MCL), Bw. Francis Nanai (kulia) wakiwaonyesha Waandishi wa habari muonekano mpya wa gazeti la michezo la Mwanaspoti mara baada ya uzinduzi Jijini Dar es Salaam.


NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ameipongeza Kampuni ya Uchapishaji Magazeti ya Mwananchi Communications Limited (MCL) kwa jitihada kubwa wanazozifanya katika kusimamia maadili kwa kuhabarisha na kuielimisha jamii ya Kitanzania
Pongezi hizo amezitoa jana wakati wa Uzinduzi wa Muonekano Mpya wa gazeti pendwa la michezo la Mwanaspoti linalochapishwa na Kampuni hiyo
Dkt. Mwakyembe amesema kuwa, mara kwa mara MCL imekuwa ikiisaidia jamii kwa kujihusisha katika masuala mbalimbali ya kijamii kama vile wakati wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera imeweza kutoa mchango wake mkubwa kwa jamii na daima imekuwa ikilinda maadili na weledi wa kazi ya uandishi kwa wafanyakazi wake jambo ambalo linaonyesha ushirikiano mzuri baina ya Serikali, Kampuni na jamii.
“Mimi nawapongeza na kuwashukuru sana MCL kwakuwa mstari wa mbele katika kulinda maadili katika kazi zenu, endeleeni kulinda maadili kwa kuhabarisha na kuielimisha jamii, sijaona mkivunja maadili ya kazi zenu na hakika mnajijengea sifa nzuri kwa wengine”, alisema Dkt. Mwakyembe.

Aliongeza kuwa, kwa sasa kumeibuka wimbi kubwa la Waandishi wa habari (Makanjanja) ambao hawana vyeti wala weledi wa kufanya kazi ya uandishi wa habari na hao wamekuwa kila wakati wakirusha taarifa zisizo sahihi hususani katika mitandao ya kijamii jambo ambalo Serikali haiwezi kulifumbia macho.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Bw. Francis Nanai amesema kwamba lengo la kampuni hiyo kuja na muonekano mpya wa gazeti hilo ni kuwapa ladha mpya wasomaji wake nchini kote, na hiyo ni mara ya sita kwa gazeti hilo kubadilishwa muonekano wake tangu kuanzishwa kwake mwaka 2001.
“Sisi kama wadau wa michezo tumewasikiliza wasomaji wa gazeti letu na tukayafanyia kazi mawazo yao na ndiyo maana tukaamua kuja na muonekano mpya wa gazeti hili ambao uko kimataifa zaidi”, alisema Nanai.
Aliongeza kuwa, gazeti hilo lilianzishwa na waandishi wa tatu mwaka 2001 na lilikuwa likitoa nakala 3,000 kwa siku ambapo kwa sasa kuja kwa muonekano mpya wa gazeti hilo kutaongeza idadi ya wasomaji tofauti ilivyokuwa mwanzo na idadi ya uchapishaji imeongezeka hadi kufikia nakala 60,000 kwa siku.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akichomoa gazeti jipya la Michezoa la Mwanaspoti ambalo lina muonekano mpya wa kisasa zaidi mara baada ya kulizindua Jijini Dar es Salaam.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: DKT. MWAKYEMBE: MCL ENDELEENI KUSIMAMIA MAADILI NA KUHABARISHA JAMII.
DKT. MWAKYEMBE: MCL ENDELEENI KUSIMAMIA MAADILI NA KUHABARISHA JAMII.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjd7Tj9POTPjBekznsmMh2AcIEI-hLuBQx1DGL4B-6CF0UNCdiuTKt2gsEh31K7koot247PRgQRmxCl-qwilIR9milWaSJCm7lUZtyZWSREl5ZZDs4hxok80r-kHj_jFJvmnIz3BFkYT_mH/s640/PICHA+5.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjd7Tj9POTPjBekznsmMh2AcIEI-hLuBQx1DGL4B-6CF0UNCdiuTKt2gsEh31K7koot247PRgQRmxCl-qwilIR9milWaSJCm7lUZtyZWSREl5ZZDs4hxok80r-kHj_jFJvmnIz3BFkYT_mH/s72-c/PICHA+5.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/dkt-mwakyembe-mcl-endeleeni-kusimamia.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/dkt-mwakyembe-mcl-endeleeni-kusimamia.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy