DAWASCO YARAHISISHA HUDUMA KWA WATEJA WA MAJI, SASA KUUNGANISHWA KWA NJIA YA SIMU

KATIKA kuhakikisha inarahisisha upatikanaji wa  huduma ya majisafi na kwenda na mfumo wa kisasa wa mawasiliano ya kiteknolojia, Shiri...





KATIKA kuhakikisha inarahisisha upatikanaji wa  huduma ya majisafi na kwenda na mfumo wa kisasa wa mawasiliano ya kiteknolojia, Shirika la MajiSafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) limezindua mfumo mpya wa mawasiliano ambao unalenga kumrahisishia mteja kupata na kutoa taarifa zinazohusu huduma hiyo kwa haraka zaidi jijini humo leo.
Huduma hiyo mpya sasa itapatikana kwa wakazi wote wa jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Teknolojia (TEHAMA) wa
DAWASCO, Bw. Kiula Kingu amesema lengo kuu la mfumo huu ni kumweka mteja karibu kihuduma na kila mwananchi ana uwezo wa kutumia mfumo huo katika simu yake kupitia mitandao yote ya simu za mikononi nchini.
Kingu ameongeza kuwa ili mteja kunufaika na mfumo huu anatakiwa kuhakikisha ana simu ya mkononi ya “Smartphone” ambayo itamwezesha kupakua mfumo huo mpya wa DAWASCO, kisha kujisajili kwa kuingiza akaunti namba yake ya DAWASCO ambapo baada ya kufuata hatua zote za kujisajili mteja atatumiwa neno la siri ambalo litamwezesha kuingia na kupata taarifa husika. “Sisi Dawasco tumeona haja ya kujiboresha na kwenda sawa na teknolojia kwa kumletea mteja wetu mfumo rahisi ambao utamwezesha kupata taarifa zetu kupitia simu yake ya mkononi muda wowote,”alisema Bw. Kingu.
Naye, Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Bi. Everlasting Lyaro, amewataka wananchi wa Dar es Salaam na Pwani kupakua mfumo huu kwani ni rahisi kuutumia na hauna gharama zozote. Anasema ni mfumo ambao utamrahisishia mteja kupata taarifa muhimu zinazohusu huduma ya maji zikiwamo ankara ya mwezi, taarifa za lini mteja alifungiwa huduma ya maji, muda ambao alifanya malipo, lini mita yake ya maji  ilisomwa na taarifa nyingine nyingi.
“Nawasihi wateja wetu na wananchi wote kupakua mfumo huu mpya katika simu zenu za mkononi ili kuweza kufurahia huduma zetu, hakuna gharama zozote ambazo utatozwa. Kupitia mfumo huu utaweza kupata taarifa zote muhimu za huduma ya majisafi zikiwemo taarifa za mivujo ya maji na ankara za maji za kila mwezi,”amefafanua Bi. Lyaro.
Anasema kwa sasa wateja hawana haja ya kutumia muda mrefu katika ufuatiliaji wa kuunganishwa huduma ya maji, bali kilichorahisishwa ni mteja kuweka taarifa zake sahihi kwenye mfumo huo na DAWASCO itatumia taarifa hizo kumtafuta mteja na kukamilisha taratibu nyingine hadi kuhakikisha mteja anapata huduma ya maji.

Meneja wa Tehama wa Shirika la Maji Safi na Maji Taka jijini Dar es Salaam (DAWASCO), Kiula Kingu akiongea na waandishi wa habari kuhusu faida za mfumo wa huduma mpya wa mawasiliano kwenye simu ya mkononi unaowezesha wateja wa shirika hilo kupata taarifa, kutoa taarifa, kupata ankara za maji za mwezi wakati wa uzinduzi wa mfumo huo jijini Dar es Salaam leo. 

Meneja wa Tehama wa Shirika la Maji Safi na Maji Taka jijini Dar es Salaam (DAWASCO), Kiula Kingu akifafanua utendaji wa mfumo wa huduma mpya wa mawasiliano kwenye simu ya mkononi unaowezesha wateja wa shirika hilo kupata taarifa, kutoa taarifa, kupata ankara za maji za mwezi wakati wa uzinduzi wa mfumo huo jijini Dar es Salaam leo. Wanaoshuhudia (kutoka kulia) ni Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Everlasting Lyaro, Afisa Tehama Chales Kayuza na Msimamizi wa kituo cha huduma wateja Vivian Shayo

Meneja wa Tehama wa Shirika la Maji Safi na Maji Taka jijini Dar es Salaam (DAWASCO), Kiula Kingu akifafanua jambo kwa wanahabari wakati wa uzinduzi wa mfumo mpya wa mawasiliano katika simu za mikononi inayowawezesha kupata taarifa zote muhimu za shirika hil kwenye simu. Pamoja naye ni Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Everlasting Lyaro. (Picha na Robert Okanda blogspot)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: DAWASCO YARAHISISHA HUDUMA KWA WATEJA WA MAJI, SASA KUUNGANISHWA KWA NJIA YA SIMU
DAWASCO YARAHISISHA HUDUMA KWA WATEJA WA MAJI, SASA KUUNGANISHWA KWA NJIA YA SIMU
https://i.ytimg.com/vi/CCe2T7kNZP8/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/CCe2T7kNZP8/default.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/dawasco-yarahisisha-huduma-kwa-wateja.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/dawasco-yarahisisha-huduma-kwa-wateja.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy