COKE STUDIO AFRIKA YACHANGIA KUPAISHA KAZI ZA WASANII NCHINI TANZANIA

Baadhi ya wasanii wa Tanzania waliowahi kushiriki Coke Studio. *Imetangaza pia muziki wa Bongo Fleva Onyesho maarufu la muziki la Coke...



Baadhi ya wasanii wa Tanzania waliowahi kushiriki Coke Studio.

*Imetangaza pia muziki wa Bongo Fleva

Onyesho maarufu la muziki la Coke Studio Africa, ambalo hivi sasa limeingia katika awamu ya tano chini ya udhamini wa kampuni ya Coca-Cola, limechangia kwa kiasi kikubwa kutangaza wasanii wa Tanzania waliofanikiwa kushiriki na kazi zao nje ya nchi hususani wanaopiga muziki wa Bongo Flava.

Kazi za wasanii zimejulikana kutokana na mtindo unaotumika katika onyesho hili la kuwakutanisha wasanii nguli kutoka nchi mbalimbali za Afrika ambapo hufanya kolabo za pamoja ambazo zinarushwa kupitia vituo vya luninga na kufuatiliwa na wapenzi wengi wa muziki kupitia mitandao ya kijamii.

Baadhi ya wasanii kutoka Tanzania ambao wameshiriki onyesho hili tangu lianzishwe ni Lady Jaydee, Diamond Platnumz, Vanessa Mdee, Alikiba, Joh Makini, Shaa, Fid Q, Ben Pol, John Makini, Shaa, Nahreel na msimu huu wa tano wapo Rayvanny, Izzo Bizness na Nandy.

Misimu minne iliyopita ya Coke Studio Africa imekuwa na mafanikio makubwa katika kuutangaza muziki wa Bongo Flava barani Afrika. Wamejiongezea mashabiki, wamejifunza mambo mbalimbali kuhusu muziki kama burudani, muziki kama taaluma na muziki kama biashara na tena si tu kutoka kwa wasanii wenzao wa Afrika na Marekani pia.

Vilevile wasanii wote ambao wamepita kwenye onyesho hili wameendelea kupata mafanikio makubwa ya kimuziki kutokana na kazi zao kuendelea kutamba na kukubalika kwa wengi ndani na nje ya Tanzania.

Taarifa kutoka kampuni ya Coca-Cola iliyotolewa hivi karibuni imeeleza kuwa onyesho la Coke Studio Africa, ambalo umaarufu wake umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka msimu huu utakuwa na burudani za aina yake kutoka kolabo za wasanii nguli barani Afrika kuanzia Afrika Magharibi mpaka Afrika ya Kusini na litarushwa na vituo vya luninga kwenye nchi zaidi ya 30 barani Afrika.

Tangia onyesho hili lianzishwe limekuwa kiungo kikubwa cha kuwakutanisha wanamuziki wa Afrika kufanya kazi kwa pamoja na kupiga muziki wenye vionjo kutoka sehemu mbalimbali za Afrika ikiwemo kuleta burudani kubwa kwa washabiki wa muziki wa kiafrika na kuwaunganisha waafrika hususani vijana kupitia muziki.

Katika msimu wa Coke Studio Africa unaotarajia kuanza kurushwa kwenye luninga mapema mwezi ujao unashirikisha wasanii kutoka katika nchi za Kenya, Afrika ya Kusini, Uganda, Tanzania, Rwanda, Ethiopia, Nigeria, Ghana, Angola, Zimbabwe, Togo, Cote d’Ivoire, Madagascar, Mauritius, Msumbiji, DRC na Cameroon.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: COKE STUDIO AFRIKA YACHANGIA KUPAISHA KAZI ZA WASANII NCHINI TANZANIA
COKE STUDIO AFRIKA YACHANGIA KUPAISHA KAZI ZA WASANII NCHINI TANZANIA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjMue6bEVNf7S_oBPK86Sg_BSZ1lDg5LxzKlmTPQ5cNIHNRSGyCELR0RWhzZQ3xB7VS1UqSQo824jonr0mV2SUGZuXlad7CtGFHXSUfGnBf5CbKnENqS3QwhXuRSSshOezYjrLJqd134Z4/s640/Lady+Jay+Dee+2.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjMue6bEVNf7S_oBPK86Sg_BSZ1lDg5LxzKlmTPQ5cNIHNRSGyCELR0RWhzZQ3xB7VS1UqSQo824jonr0mV2SUGZuXlad7CtGFHXSUfGnBf5CbKnENqS3QwhXuRSSshOezYjrLJqd134Z4/s72-c/Lady+Jay+Dee+2.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/coke-studio-afrika-yachangia-kupaisha.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/coke-studio-afrika-yachangia-kupaisha.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy