F BALOZI KAMALA ATEMBELEA KATA KITOBO NA KUZINDUA MRADI WA DARAJA LA KYANKOKO | RobertOkanda

Saturday, August 5, 2017

BALOZI KAMALA ATEMBELEA KATA KITOBO NA KUZINDUA MRADI WA DARAJA LA KYANKOKO

Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dkt. Diodorus Buberwa Kamala siku ya jana alitembelea Kata ya Kitobo Wilayani Missenyi na kuzindua Daraja la Kyankoko lenye sehemu tatu zilizowekewa Kalavati ,mrasdi uliopewa jina la la Novati Rutegaruka Memorial Bridge ambalo ni jina la muasisi na mwanasiasa mkongwe ambaye aliangaingia eneo hilo katika kipindi cha Uhai wake.

Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dkt. Diodorus Buberwa Kamala pichani wakati akizindua Daraja hilo lililogharimu kiasi cha shilingi milioni kumi na nne za kitanzania (Tsh 14,000,0000) kulia pichani ni Diwani wa Kata ya Kitobo Mh.Willy Mtayoba.Muonekano wa Daraja la Kyankoko lililopewa jina la Novati Rutegaruka Memorial Bridge Daraja linalovikutanisha Vijiji vya Msibuka na Kayanga katika Kata ya Kitobo Wilayani Missenyi.


Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dkt. Diodorus Buberwa Kamala (pichani) akiongea na wananchi wa Kijiji cha Kashasha kata Kitobo waliohudhuria katika mkutano wake wa hadhara,Balozi Dkt. Diodorus Buberwa Kamala ameweza kuchangia miradi ya maendeleo inayoendelea katika kata hiyo na pamoja na kuahidi kuzifanyia kazi kero mbalimbali kama Uhaba wa wauguzi katika Zahanati na vituo vya Afya,Utaratibu wa Bima ya Afya kwa Wazee na watu wenye Ulemavu kwa kuwapunguzia changamoto wanazokutana.


Sehemu ya wananchi wakifatilia kwa umakini wakati mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dkt. Diodorus Buberwa Kamala akiendelea kuwahutubia na kufanya majumuhisho ya changamoto alizozibaini katika ziara yake ya Siku 17 Jimboni Mwake.


Baadhi ya wananchi waliohudhurio mkutano wameweza kupata nafasi ya kuelezea Kero zinazowakabili licha ya kuwepo mafanikio katika utatuzi wa baadhi ya kero kupitia kwa Mbunge wao Balozi Dkt. Diodorus Buberwa Kamala

Baadhi ya wananchi waliohudhurio mkutano wameweza kupata nafasi ya kuelezea Kero zinazowakabili licha ya kuwepo mafanikio katika utatuzi wa baadhi ya kero kupitia kwa Mbunge wao Balozi Dkt. Diodorus Buberwa Kamala

Wananchi wakifurahia jambo katika mkutano huo uliofanyika Jana katika Kijiji cha Kashasha kata Kitobo Wilayani Missenyi.


Afisa Maendeleo Kata Kitobo Saudi Crispian wakati akisoma taarifa ya maendeleo ya kata kwa Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Balozi Dkt. Diodorus Buberwa alipotembelea kata hiyo, Balozi Dkt. Kamala amehitisha ziara yake kwa kutembelea maeneo mbalimbali kwa kukagua miradi ya maendeleo na kubaini namna miradi mingi ya Maji Wilayani Missenyi ilivyotekelezwa chini ya kiwango. (Picha kwa hisani ya bukobawadaumedia)

0 comments:

Post a Comment