AIRTEL YATOA VITABU VYA SAYANSI KWA SEKONDARI SUMBAWANGA

Na Mwandishi Wetu Ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha kila mtoto kuanzia chekechekea mpaka ...



Na Mwandishi Wetu
Ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha kila mtoto kuanzia chekechekea mpaka kidato cha nne wanapata elimu bure, kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania leo imetoa vitabu vya sayansi kwa shule za mkoa wa Rukwa Wialyani Sumbawanga vyenye thamani ya shilingi milioni kumi TZS 10,000,000
Vitabu hivyo vimepokelewa na Mbunge wa Jimbo la kalambo Mhe. Josephat Kandege na kugaiwa kwa shule zenye uhabu wa vitabu jimboni humo.
 Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi vitabu, Mbunge wa Jimbo la kalambo Mh, Josephat Kandege alisema “ muhimu kutambua mchango wa makampuni binafsi kama Airtel Tanzania kwa juhudi za dhati za kuunga mkononi serikali yetu katika kuninua sekta ya elimu hapa nchini. sote tunajua ya kwamba serikali yetu inaongozwa na sera ya serikali ya viwanda. Kwa maana hiyo hatuwezi kuwa na viwanda bila ya kuwa na wanasayansi, hiyo basi vitabu hivi vitaongeza chachu kwa wanafunzi wetu wa kuendelea kufanya vizuri katika masomo ya sayansi na hatimaye kufanikisha ndoto zao pamoja na serikali”.
Mh Kandege aliendelea kusema kwamba “nawaomba Airtel na wadau wengine waendelee kutusaidia kwenye nyaja zingine mbali mbali ili kuendelea kutengeneza mazingira bora kwa wanafunzi kujifunza na hivyo kuongeza uelewa na kuwa na taifa lenye ueledi”.
Kwa upande wake Meneja Mauzo wa Airtel Rukwa na Katavi Bw, Hapson Kamanya  alisema “Airtel tunaamini jamii iliyoelimika inajengwa kutoka katika shule zenye vifaa vya kufundishia vya kutosha hususani vitabu,  ili kuwa na maendeleo endelevu ni muhimu kuwekeza kwenye elimu na leo tunathibitisha dhamira yetu kwa kutoa msaada wa vitabu katika shule hizi”.
Tunaamini ya kwamba msaada wa vitabu utachochea ufaulu mzuri katika masomo ya sayansi katika mkoa na  pia utaongeza idadi ya wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi” Aliongeza Kamenya.
Kwa upande Mkuu wa shule ya Mwazye Bw, Haron Mwaibabu akiongea kwa niaba ya shule zilizofaidika na msaada wa vitabu hivyo alisema “Msaada huu umekuja wakati muafaka wakati shule zetu zimekuwa na upungufu wa vitabu na tunaahidi kuvitunza na kuvitumia ipasavyo".
Aliongeza, ni ukweli kuwa shule zetu zina uhaba wa vitabu vya sayansi kitu ambacho kilikuwa kinatupa ugumu kwenye kufundisha na hata kupelekea baadhi ya wanafunzi wetu kutotamani kuchukua masomo ya sayansi. Tunashukuru sana Airtel kwa kuwa mkombozi kwenye hili’.
 
 Diwani wa Kata ya Mambo Nkose Kanowalya Siwale (kushoto), Meneja Mauzo Airtel Tanzania Kanda ya Rukwa Hudson Kamenya (wa pili kushoto), Jimbo la Kalambo mkoani Rukwa Wilaya ya Sumbawanga Josephat Kandege wakimkabidhi vitabu vya sayansi Makamu wa shule ya Sekondari ya Kalambe Charles Mnkonya (kulia). Vitabu hivyo vyenye thamani ya TZS 10,000,000 vimetolewa na Airtel Tanzania kwa shule za sekondari zenye uhaba wa vitabu vya sayansi kwenye Jimbo la Kalambo.

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kalembe wakiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja Mauzo Airtel Tanzania kanda ya Rukwa Hudson Kamenya baada ya kampuni ya Airtel Tanzania kukabidhi vitabu vya sayansi vyenye thamani ya Tzs10,000,000/- mwishoni mwa wiki kwa jimbo la Kalambo mkoani Sumbawanga


Meneja Mauzo Airtel Tanzania kanda ya Rukwa Hudson Kamenya (katikati) na Mbunge wa Jimbo la Kalambo mkoani Rukwa Wilaya ya Sumbawanga wakimkabidhi Mwalimu wa somo la Kemia kwenye shule ya sekondari ya Mwazye Aidin Mwaibabu baadhi ya vitabu vilivyotolewa na kampuni ya Airtel Tanzania kwa shule za sekondari zenye uhaba wa vitabu vya sayansi kwenye Jimbo la Kalambo.





COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: AIRTEL YATOA VITABU VYA SAYANSI KWA SEKONDARI SUMBAWANGA
AIRTEL YATOA VITABU VYA SAYANSI KWA SEKONDARI SUMBAWANGA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhJNcwESE82BRnj8BT4SHql93gkUjDeh9KTv7tsckDecAt6Io-AASmwwWQHYCQetgAfoXL1bRNEMMnkU3fS7gyrLFZoLns27ILXfUn0z2meeAvG8rNDQhit9NMT95BgemJiYDIsMK7_cqY/s640/IMGM0105.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhJNcwESE82BRnj8BT4SHql93gkUjDeh9KTv7tsckDecAt6Io-AASmwwWQHYCQetgAfoXL1bRNEMMnkU3fS7gyrLFZoLns27ILXfUn0z2meeAvG8rNDQhit9NMT95BgemJiYDIsMK7_cqY/s72-c/IMGM0105.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/airtel-yatoa-vitabu-vya-sayansi-kwa.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/airtel-yatoa-vitabu-vya-sayansi-kwa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy