Mheshimiwa Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi akizungumza na Mbunge wa Iringa mjini Mh. Mchungaji P...
Mheshimiwa
Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi akizungumza na
Mbunge wa Iringa mjini Mh. Mchungaji Peter Msigwa katika Shule ya
Viziwi, kulia ni Mbunge Viti Maalum Mhe Zainab Mwamwindi akisikiliza na
katikati ni Mbunge wa viti Maalum Iringa Mh. Ritha Kabati.
|
Mheshimiwa
Profesa Joyce Ndalichako Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi alifanya
ziara ya ghafla katika shule Mkoani Iringa. Alitembelea shule
zinazofundisha watoto wenye mahitaji maalum za Makala Wilaya ya Mfundi,
Shule ya viziwi Mtwivila, Shule ya sekondari ya wasichana Mtwivila na
shule ya sekondari ya Lugalo. Nia ya ziara ni pamoja na kukagua vifaa
vya kufndishia ambvyo serikali imetoa. Pia alipta fursa ya kusalimia
wanafunzi na walimu. Katika ziara hiyo aliongzana na Mkuu wa Mkoa wa
Iringa Mhe Amina Masenza, Katibu Tawala wa mkoa wa Iringa, Wamoja
Ayoub, Wakuu wa wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Jamhuri David na Iringa
Mheshimiwa Richard Kasesela. Pia wabunge waheshimiwa, Ritta Kabati,
Zainab Mwamwindi na Mchungaji Peter Msigwa
Mheshimiwa Profesa
Joyce Ndalichako Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi akizungumza na
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela (wa pili kushoto) na Mbunge
wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa.
Mheshimiwa
Profesa Joyce Ndalichako Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi akizungumza
pamoja na viongozi mbalimbali mkoani Iringa wakifurahia jambo na
wanafunzi wa shule ya maalum ya viziwi mkoani humu
Mheshimiwa
Profesa Joyce Ndalichako Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi akizungumza na
Mh. Ritha Kabati akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi
Profesa Ndalichako na wanafunzi wa Iringa Girls.
COMMENTS