WAZIRI DKT. MWAKYEMBE AWA MGENI RASMI FAINALI ZA SHINDANO LA BONGO STYLE, AKARIBISHA SHINDANO HILO KUFANYIKA BUNGENI DODOMA 2018

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.  Dkt. Harrison Mwakyembe akitoa hotuba yake wakati wa fainali za shindano la Bongo Style...


Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.  Dkt. Harrison Mwakyembe akitoa hotuba yake wakati wa fainali za shindano la Bongo Style, lililofanyika makumbusho ya Taifa Jijini Dar ,linalohusisha fani za ubunifu wa mavazi,upigaji picha na uandishi wa miswada ya filamu ambapo aliipongeza Taasisi isiyo ya kiserikali ya Faru Arts and Development Organization(FASDO) kwa kuandaa mashindano hayo, alisema kuwa Serikali inalojukumu la kusaidia Asasi kama FASDO ambazo zinaingia katika maswala ambayo Serikali hawakuyawekea msingi mkubwa. "Naomba niagize na kuwa kuna watendaji wetu wa wizara katika sherehe hii mkae chini na watu wa FASDO ili mwaka kesho zoezi hili lifanyikie Bungeni Dodoma" Alisema Dkt. Mwakyembe.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.  Dkt. Harrison Mwakyembe (wa tatu kutoka kulia) akimkabidhi Agnes Nyahonga  tuzo na zawadi ya mfano wa Hundi yenye thamani ya Tsh 1,000,000 aliyeshinda   shindano la Bongo Style katika kipengele cha ubunifu wa mavazi.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.  Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili
kutoka kulia) akimkabidhi Goodhope Elieskia maarufu kwa jina la Zagamba  tuzo na zawadi ya mfano wa Hundi yenye thamani ya Tsh 1,000,000 aliyeshinda shindano la Bongo
Style katika kipengele cha uandishi wa miswada ya Filamu.

 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe (wa
kutoka kulia) akimkabidhi Masoud Masoud  tuzo na zawadi ya mfano wa Hundi yenye thamani ya Tsh 1,000,000 aliyeshinda   shindano la Bongo Style katika kipengele cha ubunifu wa mavazi.



 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili
kutoka kulia) akimkabidhi Philip Florian  tuzo ya Best Personality aliyopokea kwa niaba ya Kelvin Mwanasoko ambaye hakuweza fika katika Mashindano hayo.

 Msanii Dullah Aka DY akitumbuiza wakati wa Fainali hizo.
 Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Godfrey Mngereza akizungumza wakati wa fainali za Shindano la Bongo Style na kuipongeza Asasi ya Kiraia ya FASDO kwa ubunifu mkubwa.
 Mratibu wa FASDO Nchini Tanzania Bi. Joyce Msigwa akizungumza wakati mambo mbalimbali yanayohusu Asasi hiyo ikiwa ni pamoja na mafanikio waliyoyapata kama kuendesha shindano la Na mimi nipo pamoja na FASDO CUP na mengine mengi yahusuyo asasi hiyo.
Ilikuwa ni 'Surprise' Kati kati ya Sherehe za Shindano la Bongo Style ambapo Mratibu Mkuu wa FASDO na Muasisi wa Asasi hiyo isiyo ya kiserikali Bi. Lilian Nabora(Aliyevaa Gauni Jekundu) alipofanyiwa Hafra fupi ya siku yake ya Kuzaliwa ambapo alitimiza miaka 50. Waliomsindikiza ni 'Team' ya FASDO pamoja na washiriki wa shindano hilo kwa mwaka 2017.
Mratibu Mkuu na Muasisi wa FASDO Lilian Nabora akiongea wakati wa fainali za Bongo Style, alisema kuwa wamewekeza sana katika mitandao ya kijamii na hasa tovuti ya www.fasdo.org ili kuwafikia vijana wengi zaidi Tanzania nzima ambao wanauwezo na wanajiamini kuwa wanavipaji katika mambo mbalimbali wapate kujiunga katika taasisi hiyo,aliongeza kuwa mchakato wa kuwapata washindi ulipitia mchujo mpaka kuwapata washiriki bora 30,kisha 15, mpaka kufikia washindi watatu(3) "Mpaka sasa tumeweza kuwafikia vijana wanaokadiliwa kuwa 1,500 na mpaka sasa bado tunawahimiza wapate kujiunga nasi" alisema Bi. Lilian.
 Waliokaa katika Meza ni Majaji Upande wa ubunifu wa mavazi, na walio mstari wa mbele ni Majaji upande wa Miswada ya Filamu na upigaji picha.
Baadhi ya washiriki upande wa Ubunifu wa Mavazi wakiwa wanaonesha Mavazi yao waliyo yabuni wao wenyewe
 Wageni waalikwa  wakifuatilia sherehe za Fainali za shindano la Bongo Style

 Mwenyekiti wa FASDO Bw. Stanley Kamana akitoa neno la Shukurani wakati wa Fainali za Bongo Style

 Washiriki wa Shindano la Bongo Style kwa Mwaka 2017 wakiwa wanafuatilia mambo mbali mbali wakati wa Shindano hilo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Kiraia ya FASDO Bw. Tedvan Nabora akitoa neno la Shukurani kwa wote waliohudhuria katika Fainali za shindano la Bongo Style

Picha ya pamoja ya  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.  Dkt. Harrison Mwakyembe,Uongozi na Team ya FASDO,Majaji na washindi wa Bongo Style Competition kwa mwaka 2017.

Picha zote na Laden Tedvan Nabora.






COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI DKT. MWAKYEMBE AWA MGENI RASMI FAINALI ZA SHINDANO LA BONGO STYLE, AKARIBISHA SHINDANO HILO KUFANYIKA BUNGENI DODOMA 2018
WAZIRI DKT. MWAKYEMBE AWA MGENI RASMI FAINALI ZA SHINDANO LA BONGO STYLE, AKARIBISHA SHINDANO HILO KUFANYIKA BUNGENI DODOMA 2018
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgnfQjvPG7oxxiOQZg8b8a492Df7DBecmUfGo9NhE6MyTJUQJybNBKi_BZifvvKFQ_Hl96KRGKk8vKbGC9c8-yzLp9SoCpJtdJGSE8mnkVg3orErRPl_OUvjr22cA7KFI88-C8jctGm_WXz/s640/22.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgnfQjvPG7oxxiOQZg8b8a492Df7DBecmUfGo9NhE6MyTJUQJybNBKi_BZifvvKFQ_Hl96KRGKk8vKbGC9c8-yzLp9SoCpJtdJGSE8mnkVg3orErRPl_OUvjr22cA7KFI88-C8jctGm_WXz/s72-c/22.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/waziri-dkt-mwakyembe-awa-mgeni-rasmi.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/waziri-dkt-mwakyembe-awa-mgeni-rasmi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy