WAZIRI wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amewaasa watumishi wa mahakama kushughulikia vitendo vya rushwa kwani vin...
WAZIRI
wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amewaasa watumishi wa
mahakama kushughulikia vitendo vya rushwa kwani vinaipatia mahakama
taswira hasi na kuzitaka tume za mahakama na maadili kuchunguza vitendo
vya ukiukwaji wa maadili na kuchukua hatua stahiki.
Waziri
Kabudi, amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na
watumishi wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani juu ya mustakabali wa
taasisi hiyo, ikiwa ni mara yake ya kwanza kufanya ziara tangu
alipoteuliwa kuwa Waziri.
Amesema,
majaji na mahakimu mara nyingi, wamekuwa wakihusishwa na vitendo vya
rushwa hivyo, na kuchangia kuwepo kwa kutokuwa na imani kwa wananchi
wanaokuwa na shida, mbali mbali katika taasisi hizo, hasa wale wenye
kesi.
‘’Pamoja
na mabadiliko makubwa katika mahakama bado kumekuwa na changamoto ya
uadilifu hususan vitendo vya rushwa na uwajibikaji ambavyo vimeleta
taswira hasi kwa wananchi wanaotafuta haki na kusababisha ushiriki
mdogo,’’alisema Profesa Kabudi.
Ameongeza,
watendaji wanapaswa kubuni mbinu mbali mbali za kuweza kubadili taswira
hiyo kwa kuwachukulia hatua za kinidhamu wanaokiuka maadili na kusogeza
huduma kwa wananchi.Kwa
mujibu wa Profesa Kabudi, mahakama inanafasi kubwa ya kuchangia
maendeleo ya nchi na kwamba jambo wanalopaswa kufanya ni kuimarisha
utendaji kazi na kutokomeza rushwa.
Kwa
upande wake, Kaimu Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma alisema kuwa
wataendelea kutumia sheria kwa ajili ya kuwainua wananchi wengi kwa
lengo la kukuza uchumi.
Profesa
Juma alisema majaji na mahakimu ni sehemu ya jamii ambao wanapaswa
kushiriki kustawisha wanaqnchi ili kutokomeza umasikini.
Akiwasilisha
ripoti kuhusu mahakama, Mtendaji Mkuu wa mahakama, Hussein Katanga
alisema kuwa idadi ya majaji imeshuka kutoka 100 hadi 80 huku uhitaji
wake ukiwa ni kati ya 100 hadi 120.
Katanga
alisema majaji 20 wameacha kazi kwa sababu mbalimbali ikiwemo kustaafu
na kwamba uhitaji huo unachangia kasi ya kuongezeka kwa ufunguaji
mashauri.
COMMENTS