F WANANCHI WATAKIWA KUTUMIA NISHATI YA BIOGAS ILI KURAHISISHA MAISHA | RobertOkanda

Tuesday, July 18, 2017

WANANCHI WATAKIWA KUTUMIA NISHATI YA BIOGAS ILI KURAHISISHA MAISHA


Mkufunzi wa semina ya wadau mbalimbali wanaotumia Teknologia ya biogas, pamoja na wamiliki wa mitambo hiyo pamoja na mafundi Rowah Spear akiendelea kutoa elimu katika semina iliyofanyika jijini Arusha leo.
Mratibu wa Ubunifu  kutoka ECHO, Harold Msanya akifafanua jambo mbele ya wakufunzi hao.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifanya kazi kwa majadiliano katika makundi.


Mkufunzi wa semina ya wadau mbalimbali wanaotumia Teknologia ya biogas ndugu Rowah Spear akiwa anawaelekeza baadhi ya wadau waliouthuria semina jinsi biogas inaweza kufanya kazi
Wadau wakifutilia mada.


Mkurugenzi wa ECHO   Erwin Kinsey akiwa anaonyesha wakulima na wadau walioshiriki semina hiyo mmea aina ya gugukaroti ambalo ,alisema kuwa gugu ilo kwa asilimia 90% huku asilimia 10% ni gugu ambalo linaweza kutumika kutengeneza biogas.

Wadau wakifanya majadiliano katika makundi yao ikiwa ni sehemu ya kujifunza njia mbalimbali  na matumizi ya biogas
(Habari picha na Woinde Shizza, Arusha)


Wananchi wametakiwa kutumia Gesi Bayogesi
kwani  inapunguza gharama za watumiaji wa vyanzo vingine vya nishati  pia gesi hii inasaida kutunza mazingira.Hayo yamebainishwa leo na Mratibu wa Ubunifu  kutoka ECHO  Harold Msanya wakati akitoa mada katika semina ya wadau mbalimbali wanaotumia Teknologia ya biogas, wamiliki wa mitambo hiyo pamoja na mafundi wanaofunga na kutengeneza mitambo hiyo.


 Alisema kuwa gharama za nishati ya umeme na gesi asilia ni ghali sana hasa kwa mtumiaji
atakayedhamiria kutumia jiko la umeme au jiko la gesi lakini kwa gesi hii ya samadi mtumiaji  au mabaki ya nyasi aina mbalimbali zitamgharimu muda wake tu kujaza samadi na maji kila siku na atakuwa hana malipo ya pesa kila mwezi kama itakavyomlazimu kulipia umeme na gesi asilia kila mwezi, na hata kuni ambazo watumiaji wengine hununua

Alibainisha kuwa njia hii imeweza kuwasaidia na kuwapa faida baadhi ya wananchi ambao wameanza kutumia teknoligia hii na pia wengi wao
wameshanufaika na huduma hii.

 Aidha Bayogesi ambayo aghalabu hutokana na
kinyesi cha wanyama, masalia ya mimea na kinyesi cha binadamu inaweza kuzalishwa na kutumika kupikia na hata matumizi mengine kama vile kuendeshea mitambo mbalimbali.


“ Matumizi ya gesi hii kwa mtu ambaye ana mifugo kama vile nguruwe, ng’ombe yanaweza kusaidia
kuondokana na gharama za kununua nishati ya kuni, mkaa, umeme na hata gesi asilia inayochimbwa ardhini.”alisema  Msanya

Kwa upande wake mkufunzi wa Mkufunzi wa semina ya wadau mbalimbali wanaotumia
Teknologia ya biogas pamoja na wamiliki wa mitambo hiyo pamoja na mafundi
Rowah Spear alisemak uwa ni wajibu wa kila mtanzania kuwakikisha anakuwa na
mtambo huo kwani mtambo huo unapunguza gharama 
kubwa ambazo awali walikuwa wanatumia na pia pale mwananchi anapotumia
mtambo huu anakuwa rafiki wa mazingira kwani kwanza kabisa akati miti ovyo na
pili  yale majani, vyakula na uchafu
uchafu wa aina wowote anaweza kuukusanya na kuingiza katika mashina na
ikamsaidia kupatikana kwa Biogas
Pia alisema kuwa mbali na kupata nishati yakupikia tu pia uchafu ambao unakuwa

umetokana na mabaki haya unaweza kufanywa kama mbolea kwa mazao mbalimbali
tunayoyalima hivyo ni vyema kila mwananchi kuhakikisha nyumbani kwake anamtambo
huu


0 comments:

Post a Comment