Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la kutoa huduma za Elimu ya afya Nchini Marekani Bi. Asha Mustafa Nyang’anyi akizungumza na wandis...
Mkurugenzi
mtendaji wa Shirika la kutoa huduma za Elimu ya afya Nchini Marekani
Bi. Asha Mustafa Nyang’anyi akizungumza na wandishi wa habari kuhusu
ujio wao hapa Zanzibar.
Bwana.
Amiri Muhammed Amiri akimuonesha fangas Daktari bingwa wa ngozi
Mamotheo alipokuwa akitoa matibabu katika hospitali ya Mnazi mmoja Mjini
Zanzibar.
Baba
wa mtoto Abdulmajid akiwaonesha madaktari bingwa wa maradhi ya ngozi
namna mwanawe alivyodhurika kwa kufanya mabaka mwilini katika hospitali
ya Mnazimmoja mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga.
Na Mwashungi Tahir-Maelezo Zanzibar 03-07-2017
Wananchi
wa Tanzania wanaoishi Marekani wanadiaspora wakishirikiana na Madaktari
bingwa wapo nchini kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu ya maradhi
mbalimbali yanayowasumbua wananchi.
Zoezi la kutoa huduma hizo za matibabu bure linafanyika kwa muda wa siku tatu katika Hospitali ya Mnazi mmoja.
Akizungumza
na waandishi wa habari huko katika kitengo cha maradhi ya ngozi kwenye
hospitali kuu ya Mnazi mmoja, Mwanadiaspora Idi Seif Sandaly amesema
wameamua kuja nchini hapa kutoa huduma hizo ili kuwasaidia wananchi
wenye matatizo mbalimbali.
“Tumekuja
Zanzibar kwa lengo la kuwasaidia wananchi ambao wana maradhi mbali
mbali na kuwapatia matibabu kwa kupitia jumuiya yetu ya marekani Health
Education Development kwa kutibu maradhi ya ngozi , sukari na pressure
pamoja na maradhi ya akinamama.” Amesema Mwanadiaspora huyo.
Sandaly
amesema wapo kwa muda wa siku tatu na wamekuja na dawa za kutibia
maradhi hayo ambapo dawa hizo wanazitoa bure bila ya gharama zozote kwa
wananchi.
Amesema
katika matibabu yao wanatarajia kutoa huduma kwa zaidi ya Wananchi
3,000 watakaofika katika Hospital hiyo ya Mnazi mmoja.
Akifafanua
kuhusu gharama za Dawa hizo ambazo wamekuja nazo kutoka Marekani
amesema zaidi ya Dola Million moja za Marekeni zimetumika kwa ajili ya
kununulia Dawa hizo.
Hata
hivyo ameongeza kuwa Nusu za Dawa hizo zitatumika Zanzibar na Nusu yake
zitapelekwa Mkoa wa Bukoba kwa lengo la kusaidia matibabu mkoani huko
Nae
Daktari wa maradhi ya Ngozi kutoka Marekeni Dkt Mamotheo Lepheana
amesema amefarijika kuona wananchi wamejitokeza kwa wingi hasa wa
maradhi ya ngozi.
Sambamba
na hayo mgonjwa aliyepata matibabu hayo ya ngozi Masika Juma Mussa
mkaazi wa Mwera amesema ameshukuru kupatiwa huduma hiyo na kuiomba
serikali iendeleze kuleta wataalam kama hao wanaotaka kusaidia jamii .
Kwa
upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo la kutoa huduma za Elimu
ya afya Asha Mustafa Nyang’anyi amesema ameamua kuja Zanzibar kwa
sababu wananchi wa hapa ni wakarimu na wanaojali kusaidiwa.
COMMENTS