.Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Anne Makinda akikabidhi kadi za bima ya afya kwa watoto chini ya miaka 18 kwa wan...
.Spika
Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Anne Makinda akikabidhi kadi za
bima ya afya kwa watoto chini ya miaka 18 kwa wanachama wapya katika
maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya sabasaba
jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, ,Anne Makinda amesema
wakuu wa shule binafsi wanachukua fedha za huduma ya matibabu ya afya
kwa wanafunzi lakini wanafunzi hao wamekuwa hawapati huduma
wanazostahili na kulingana na kiasi walicholipia.
Wakuu wa Shule binafsi wamekuwa wakilipisha wanafunzi fedha za
huduma ya matibabu ikiwa ni njia moja ya maelezo kujiunga (joining
instruction) ila inapotokea mtoto anaumwa humrudisha kwa wazazi wake.
Mwenyekiti huyo ameyasema hayo wakati alipotembelea banda la NHIF
katika Maonesho ya biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya sabasaba
jijini Dar es Salaam, amesema mwanafunzi akilipia bima ya afya lazima
atumie na sio kubaki mzigo kwa mzazi wakati alishalipia fedha ya
matibabu hiyo.
Amesema kuwa wakuu wa shule wanatakiwa kujiunga na mfuko wa taifa
ya wa bima ya Afya NHIF ili kuweza kuwahudumia wanafunzi katika kupata
matibabu.
Anne Makinda amesema kuwa katika maonesho ya sabasaba wamesajili
bima za afya kwa watoto 1600 na kuongeza kuwa wananchi wamekuwa na
mwitikio mkubwa katika kupata bima za afya.
Amesema kuwa wameboresha bima ya afya katika mfuko wa afya ya
jamii katika halmashari kwa kila aliyepata bima kutibiwa mkoa mzima
tofauti na hapo nyuma kutibiwa katika Wilaya husika.
Aidha amesema kuwa wataendelea kutoa huduma za bima za afya ikiwa
ni pamoja na serikali kuweka mpango wa kila mtu kuwa na bima ya afya.
.Spika
Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, , Anne Makinda akizungumza na
waandishi wa habari mara baada ya kutembelea banda la NHIF katika
maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya sabasaba
jijini Dar es Salaam.
Spika
Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Anne Makinda akipata maelezo
kutoka Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti , Angela Mziray katika
banda la NHIF katika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa katika
viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Spika
Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Anne Makinda akipata maelezo
kutoka kwa Meneja Wanachama wa NHIF, Ellentruda Mbogoro katika banda la
NHIF katika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya
sabasaba jijini Dar es Salaam.
Sheik
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum akipata maelezo kutoka
kwa Meneja Wanachama wa NHIF, Ellentruda Mbogoro katika banda la NHIF
katika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya
sabasaba jijini Dar es Salaam.
Spika
Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Anne Makinda akipata maelezo
kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Rose Mdami wakati alipotembelea banda la
NIDA katika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya
sabasaba jijini Dar es Salaam.
Spika
Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Anne Makinda akipata maelezo
kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ,
Sebera Fulgence katika banda la Mfuko huokatika maonesho ya 41 ya
biashara ya kimataifa katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
COMMENTS