WAKANDARASI WA KITANZANIA KUWEZESHA ILI KUFANIKISHA TANZANIA YA VIWANDA

Kampuni ya Mantrac Tanzania imezindua mpango maalum wa kukodisha na kumiliki mitambo kwa kulipa kidogo kidogo ili kuwarahisishia wa...


Kampuni ya Mantrac Tanzania imezindua mpango maalum wa kukodisha na kumiliki mitambo kwa kulipa kidogo kidogo ili kuwarahisishia wateja mzigo wa kulipa fedha kununua mtambo kwa mara moja.

Hii inamaanisha kuwa wafanyabiashara na wakandarasi wataweza kukodisha mitambo kutoka katika kampuni ya Mantrac Tanzania kwa bei nafuu na kuanzia miezi sita na kuendelea anakuwa mmiliki kamili wa mtambo huo.Hayo yamesemwa na mkuu wa kitengo cha mipango na masoko Bw Valence Pantaleo. 

Alisema katika kipindi chote cha kukodisha, kampuni ya Mantrac Tanzania inagharamia matengenezo ya mtambo huo kadiri ya mwongozo wa kampuni ya CAT.Mpango wa kukodisha na kumiliki ni maalum ambao unamwezesha mkandarasi au mfanyabiashara kupata manufaa lukuki ya kutumia mitambo inayotumia tekinolojia ya kisasa kabisa ya kampuni ya CAT bila ya kununua mtambo huo mwanzo wa mradi.

Mpango huu unatoa unafuu mkubwa sana na huweza kupunguza sana gharama za uendeshaji kwa mkandarasi au mfanyabiashara.Kampuni ya Mantrac Tanzania inamhakikishia mteja mitambo na tekinolojia madhubuti ya Catepillar yenye historia pana ya kutengeneza na kuuza mitambo ya kisasa inayotumia katika miradi mikubwa ya kujenga miundombinu.
Miradi hii mikubwa ya miundombinu ni pamoja na ujenzi wa barabara, reli, majengo, madaraja, kwenye madini na kilimo.

Bidhaa zinazouzwa na kampuni ya Mantrac Tanzania zinapatikana katika matawi mbalimbali nchini kama vile Dar es Salaam, Mtwara, Mwanza, Mbeya, na Kilimanjaro.Bw Pantaleo alisema baada ya kupata mafanikio makubwa katika biashara kati ya kampuni ya Mantrac Tanzania na wateja kwenye  mitambo mipya, iliyotumika na kukodisha mitambo, sasa kampuni imeamua kuleta mpango huu wa kukodisha na kumiliki ambapo mteja atalipa kidogo kidogo hadi pale atakapomiliki mtambo wake.

Alisema kamupuni ina mitambo mingi inayofikia zaidi ya dola za kimarekani milioni 15 kwa ajili ya kutekeleza mpango huu mpya wa kukodisha na kumiliki.Kampuni ya Mantrac Tanzania ndio pekee yenye kibali cha kusambaza na kuuza mitambo mbalimbali inayotengenezwa na kampuni ya CAT hapa nchini Tanzania.

Kampuni pia ina vituo maalum vya huduma kwa ajili ya matengenezo ya mitambo, ina wataalamu wa hali ya juu na vifaa vyenye viwango vya kimataifa ambavyo hutumika katika kuchunguza tatizo na kutengeneza ubovu unaojitokeza katika mitambo.Katika mpango huu, vigezo na masharti vitazingatiwa.
Meneja Masoko wa Mantrac  Bw Valence Pantaleo.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAKANDARASI WA KITANZANIA KUWEZESHA ILI KUFANIKISHA TANZANIA YA VIWANDA
WAKANDARASI WA KITANZANIA KUWEZESHA ILI KUFANIKISHA TANZANIA YA VIWANDA
https://4.bp.blogspot.com/-Xm3i3VEgWEI/WWNR7FJjCeI/AAAAAAAAMC4/_ACWvqyLuzQt83ueQnW-OkI-A9D6uSFwACLcBGAs/s640/bed85560-8e1f-434a-aaf5-e492fb66a97d.jpg
https://4.bp.blogspot.com/-Xm3i3VEgWEI/WWNR7FJjCeI/AAAAAAAAMC4/_ACWvqyLuzQt83ueQnW-OkI-A9D6uSFwACLcBGAs/s72-c/bed85560-8e1f-434a-aaf5-e492fb66a97d.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/wakandarasi-wa-kitanzania-kuwezesha-ili.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/wakandarasi-wa-kitanzania-kuwezesha-ili.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy