VIGOGO WA IPTL HABINDER SETH NA RUGEMALIRA WAONGEZEWA MASHTAKA SITA YA UTAKATISHAJI FEDHA

Na Karama Kenyunko. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewasomea upya mashtaka, washtakiwa Harbinder Singh Seth na James Burcha...

Na Karama Kenyunko.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewasomea upya mashtaka, washtakiwa Harbinder Singh Seth na James Burchard  Rugemarila kwa kuwaongezea mashtaka na kufanya idadi yao kufikia 12.

Mapema mwezi uliopita, washtakiwa hao walipandishwa kizimbani hapo baada ya kusomewa mashtaka sita kabla ya leo kuwa 12.
Katika mashtaka hayo ambayo ni ya uhujumu uchumi yapo pia matano ya utakatishaji wa fedha na kuisababishia Serikali hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

Mashtaka hayo ni, kula njama, kujihusisha na mtandao wa uhalifu , kughushi,  kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu kuisababishia Serikali Hasara na kutakatisha fedha.

Washtakiwa wamesomewa mshtaka yao mapya na wakili wa Serikali, Shedrack Kimaro mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Katika shtaka la kwanza inadaiwa, Rugemarila Mkurugenzi wa VIP na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL na Sethi ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa PAP, kati ya Oktoba 18 ,2011 na Machi 19, 2014 jijini Dar es Salaam walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Imedaiwa kuwa, Oktoba 18,2011 na Machi 19,2014 washtakiwa hao wakishirikiana na watumishi wa umma walitekeleza mtandao huo wa uhalifu kwa lengo la kujipatia faida.

 Aidha katika shtaka la tatu linalomkabili  Sethi peke yake imedaiwa, Oktoba 10,2011 katika mtaa wa Ohio Ilala, akiwa na nia ya ulaghai alighushi fomu namba 14 a ya usajili wa makampuni  na kuonyesha yeye ni Mtanzania anayeishi Kitalu namba 887 Mtaa wa Mrikau Masaki wakati akijua ni uongo.

Seth pia anadaiwa kutoa nyaraka ya kughushi ambayo ni fomu namba 14 a ya usajili wa kampuni kwa ofisa msajiri wa kampuni, Seka Kasera kwa njia ya kuonesha kwamba yeye ni Mtanzania na Mkazi wa Mtaa wa Mrikau.

Imeendelea kudaiwa kuwa, Novemba 28/29, 2011 na Januari 23,2014 katika Makao Makuu Benki ya Stanbic Kinondoni  na Benki ya Mkombozi tawi St Joseph kwa ulaghai washtakiwa hao walijipatia kutoka Benki Kuu ya (BOT), walijipatia USD 22,198,544.60 na Tsh 309, 461,300,158.27.   

Aidha wanadaiwa kuisababisha hasara, serikali ya kiasi hicho cha fedha.

Katika shtaka la saba, inadaiwa kati Novemba 29,2013 na Januari 23, 2014 maeneo tofauti Dar es Salaam kwa pamoja walitakatisha fedha kwa kuchukua fedha kutoka BoT USD 22,198,544.60 na Tsh 309,461,300.27 wakati wakijua fedha hizo zao la kujihusisha na genge la uhalifu.

Sethi peke yake anadaiwa pia kuwa Novemba 29,2013 katika tawi la kati la Benki ya Stanbic Tanzania wilaya ya Kinondoni,  alitakatisha fedha kwa kuchukua BoT USD 22,198,544.60 wakati akijua fedha hizo zimetokana na zao la kujihusisha na genge la uhalifu.
Aidha Seth anadaiwa kutakatisha shilingi 309,461,300,158.27 kutoka BoT wakati akijua fedha hizo zimetokana na zao la kujihusisha na genge la uhalifu.

Katika shtaka la kumi, inadaiwa Januari 23, 2014 katika Benki ya Mkombozi tawi la St Joseph Cathedral, Rugemarila  alitakatisha, Sh 73,573, 500,000 kutoka kwa Seth wakati akijua fedha hizo zimetokana na zao la kujihusisha na genge la uhalifu.
Kwa upande wa shtaka la 11, Kimaro alidai kuwa Januari 23,2014 katika benki ya Mkombozi tawi la St Joseph Cathedral, Rugemarila alitakatisha fedha USD 22,000,000 kutoka kwa Seth wakati akijua fedha hizo ni zao la uhalifu.
Shtaka la 12, Seth anadaiwa kuwa Januari 28,2014 katika tawi la kati la Benki ya Stanbic wilaya ya Kinondoni alihamisha Rand (zar 1,305,800 kwenda kwenye akaunti namba 022655123 katika Standard bank Land Rover Sandton Johannesburg wakati akijua katika kipindi anahamisha fedha hizo zimetokana na zao la kujihusha na genge la uhalifu.
Washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote kwa sababu mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na washtakiwa wamerudishwa rumande kwa kuwa mashtaka ya utakatishaji wa fedha hayana dhamana.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo itatajwa tena Julai 14,2017.
 
 Mtuhumiwa James Burchard Rugemarila akielekea kupanda gari kurejeshwa mahabusu.
 
Mtuhumiwa Harbinder  Singh Sethi apanda gari la magereza kurejeshwa mahabusu.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: VIGOGO WA IPTL HABINDER SETH NA RUGEMALIRA WAONGEZEWA MASHTAKA SITA YA UTAKATISHAJI FEDHA
VIGOGO WA IPTL HABINDER SETH NA RUGEMALIRA WAONGEZEWA MASHTAKA SITA YA UTAKATISHAJI FEDHA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhlWXy18jEUZ7l-OWPCyvJbJ7NoRlBL3VS8mv3UmiLojxG5fCemOgPxTGdFiUUf4iKEbo7asjUTGgeOLNTIW3STtss21t3Eg1qoC9d3KFouebSb6K4aP4eeCQFFg9GfljwnMIQOp5EqTDA/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhlWXy18jEUZ7l-OWPCyvJbJ7NoRlBL3VS8mv3UmiLojxG5fCemOgPxTGdFiUUf4iKEbo7asjUTGgeOLNTIW3STtss21t3Eg1qoC9d3KFouebSb6K4aP4eeCQFFg9GfljwnMIQOp5EqTDA/s72-c/1.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/vigogo-wa-iptl-habinder-seth-na.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/vigogo-wa-iptl-habinder-seth-na.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy