UFAFANUZI KUHUSU KAMPUNI YA MANTRA TANZANIA KUSITISHA UCHIMBAJI WA MADINI YA URANI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA NISHATI NA MADINI Telegrams “NISHATI”                        Barabara ya Kikuyu, Simu: +02...

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
Telegrams “NISHATI”                       Barabara ya Kikuyu,nembo
Simu: +0262322018                             S.L. P. 422,
Nukushi:                                          40474 DODOMA.
Barua pepe: info@mem.go.tz
TAARIFA KWA UMMA
UFAFANUZI KUHUSU KAMPUNI YA MANTRA TANZANIA KUSITISHA UCHIMBAJI WA MADINI YA URANI
Tarehe 9 Julai, 2017, magazeti ya The Guardian na The Citizen yaliandika habari  kuhusu Kampuni ya MANTRA Tanzania kusitisha (Suspension) uchimbaji wa Madini ya Urani (Uranium) kwenye leseni yao iliyoko eneo la Mto Mkuju sababu zikiwa ni
kuporomoka kwa bei ya Urani katika Soko la Dunia pamoja na mabadiliko katika Sheria ya Madini.

Ieleweke kuwa, Kampuni ya Mantra Tanzania inayo leseni ya Uchimbaji Mkubwa wa Madini (Special Mining Licence) SML NO. 489/2013 yenye eneo la ukubwa wa kilometa za mraba 197.94 iliyotolewa tarehe 05/04/2013 na kabla ya Kampuni hiyo kuomba leseni ya uchimbaji madini ilifanya upembuzi yakinifu (feasibility study) na kuthibitisha kuwa kwa bei ya Urani ya wakati huo ambayo ilikuwa ni Dola za Marekani 65 kwa Ratili moja (US$ 65/Pound) hivyo mradi huo ungezalisha madini kwa faida.  

Hata hivyo, bei ya Urani duniani ilianza kuporomoka na kufikia Dola 18.5 kwa ratili mwanzoni mwa mwaka 2017 na kwa sasa bei ni Dola 23 kwa ratili moja. Kufuatia kuporomoka huko kwa bei, Kampuni ilikokotoa gharama na kuonekana kuwa haiwezi kuzalisha urani kwa faida.  

Tarehe 14/12/2016, Kampuni ilimuandikia Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini ikiomba Waziri mwenye dhamana na Madini atoe ridhaa (consent) ili wasitishe uchimbaji kwa muda wa miaka mitano kwa ajili ya kuangalia kama bei inaweza kupanda ndipo waanze uchimbaji.  Wizara kwa kupitia Wataalam wake ilikokotoa gharama na kujiridhisha kwamba kwa bei ya Dola 18.5 kwa ratili mradi hauwezi kuendeshwa kwa faida.  

Hivyo, Wizara iliwasilisha maombi ya Kampuni kwenye Bodi ya Ushauri ya Madini ambayo ilikaa tarehe 19/04/2017 ili kujadili maombi hayo na kisha kumshauri  Waziri mwenye dhamana kwa mujibu kifungu Na. 69 – (3) cha Sheria ya Madini ya mwaka 2010 kwani   Waziri wa Nishati na Madini ndiye mwenye mamlaka ya kutoa ridhaa ya maombi husika.

Tunapenda kuutaarifu Umma kuwa, utekelezaji wa ombi la kampuni ya Mantra la kusitisha uchimbaji wa madini ya urani  kwa muda bado halijakamilika hadi hapo ridhaa itakapotolewa na Waziri mwenye dhamana.

Kuhusu madai ya kuwa Ombi la usitishaji wa uchimbaji limetokana na mabadiliko katika Sheria ya Madini ni upotoshaji kwani sababu za kuomba usitishaji huo ni za kiuchumi zilizotokana na kushuka kwa bei ya Urani kwenye soko la dunia.
Imetolewa na:-
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Nishati na Madini
Julai 12, 2017

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: UFAFANUZI KUHUSU KAMPUNI YA MANTRA TANZANIA KUSITISHA UCHIMBAJI WA MADINI YA URANI
UFAFANUZI KUHUSU KAMPUNI YA MANTRA TANZANIA KUSITISHA UCHIMBAJI WA MADINI YA URANI
https://lh6.googleusercontent.com/DakUOzZZQZDmmdCcvbazD8SfsyZqS2hahtd06o1Pg9R9BxRQiYWpKuYxowt3l1jJPQ7aKADbpB_g_FnbJ6wtmT1SRioEshg0rMLTuV8myZnexkaM7YIBrWs2_Zn3ztvr7jlmx5mYk5hEGwgchA
https://lh6.googleusercontent.com/DakUOzZZQZDmmdCcvbazD8SfsyZqS2hahtd06o1Pg9R9BxRQiYWpKuYxowt3l1jJPQ7aKADbpB_g_FnbJ6wtmT1SRioEshg0rMLTuV8myZnexkaM7YIBrWs2_Zn3ztvr7jlmx5mYk5hEGwgchA=s72-c
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/ufafanuzi-kuhusu-kampuni-ya-mantra.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/ufafanuzi-kuhusu-kampuni-ya-mantra.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy