TUNDU LISSU AKAMATWA JNIA AKIJINDAA KWA SAFARI YA KIGALI

Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu . Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) tumepokea taarifa z...




Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu .


Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) tumepokea taarifa za kukamatwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Chama chetu na Mbunge wa Singida Mashariki ambaye pia ni Rais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS) Kwa masikitiko makubwa.


Tabia hii ya ubabe na uonevu ya Polisi inaonekana kuota mizizi na kutaka kufanywa kuwa utamaduni na utaratibu wa Jeshi la Polisi kujiamulia kumkamata kiongozi yeyote wa CHADEMA pale atakapoikosoa Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Magufuli.


Utamaduni huu ni wa kidikteta, kibabe na unaokiuka misingi ya Utawala Bora na haki ya kutoa maoni kwa mujibu wa Katiba.


Moja ya misingi mikuu ya taifa la kidemokrasia ni kuwa na Uhuru wa kujieleza na kutoa maoni au mawazo tofauti na hili ni lazima Serikali ikubali kukosolewa na kusikia upande mwingine una fikra gani juu ya mambo yanayotekelezwa na Serikali.


BAVICHA tumewahi kusema ubabe huu na uonevu huu unaivimbisha nchi, unaitikisa nchi, Rais Magufuli amejivika joho la ubabe na uonevu na kuvunja Katiba ya nchi na kukiuka misingi ya utawala bora.


Tunarudia kumtaka Rais Magufuli kukubali kusikia kutoka kwa watu wasiokuwa wa Chama chake hususani CHADEMA.


Tunalitaka Jeshi la Polisi kufuata misingi ya kuanzishwa kwake, lisimamie uwepo wake ambao ni kulinda raia na Mali zao. Hiki ambacho Jeshi hili linafanya ni kinyume cha sheria ya Jeshi la Polisi nchini (PGO) na hivyo tunamtaka IGP Sirro kuwaelekeza watendaji wake kutimiza wajibu wao na sio kusubiri kuwakamata viongozi wa CHADEMA.


Itafika hatua tutashindwa kuendelea kuvumilia ubabe huu tutalazimika kujitetea kwa mujibu wa misingi ya Tamko la haki za Binadamu


Polisi wenye ndimi mbili ni hatari Kwa Taifa Kwani Jana RPC Dodoma alisema Polisi hawana sababu ya Kumkamata na Leo Polisi Dar es Salaam wanamkamata, Jeshi linapoteza heshima yake ya kuaminika Kwa wananchi. Tunawataka waseme ukweli kwani sheria za Dodoma na Dar ziko tofauti ?. Wanatufundisha kuwa hawaaminiki!
Tunawataka watanzania wote hususani Vijana kusimama upande wa Haki, tusikubali misingi ya Taifa letu kutikiswa.


Hakika tutashinda.


_________________
Julius Mwita
Katibu Mkuu - BAVICHA.
 

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TUNDU LISSU AKAMATWA JNIA AKIJINDAA KWA SAFARI YA KIGALI
TUNDU LISSU AKAMATWA JNIA AKIJINDAA KWA SAFARI YA KIGALI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjabovFA6c-a0lMgQiBtc6vu889rCd7H2NHC4vDdSZjyPE_c_w2r7vgUCyFJOtT90OrCI_pdFbVD-kTWMwNITLO3rn4aiDGW2EHt8LY4SqeO_u_OFwmmdrATBhkIlZXG6bLA87kghqfL4Au/s640/IMG-20170720-WA0138.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjabovFA6c-a0lMgQiBtc6vu889rCd7H2NHC4vDdSZjyPE_c_w2r7vgUCyFJOtT90OrCI_pdFbVD-kTWMwNITLO3rn4aiDGW2EHt8LY4SqeO_u_OFwmmdrATBhkIlZXG6bLA87kghqfL4Au/s72-c/IMG-20170720-WA0138.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/tundu-lissu-akamatwa-jnia-akijandaa-kwa.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/tundu-lissu-akamatwa-jnia-akijandaa-kwa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy