TRA YAVIPIGA 'STOP' KUTOA HUDUMA VITUO VYA MAFUTA VISIVYOTUMIA MASHINE ZA KIELEKTRONIKI DAR ES SALAAM

Na Robert Okanda Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imevipiga stop kutoa huduma ya kuuza mafuta vituo kadhaa jijini Dar es Salaam kwa k...






Na Robert Okanda

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imevipiga stop kutoa huduma ya kuuza mafuta vituo kadhaa jijini Dar es Salaam kwa kosa la kutoa huduma hiyo pasipo kutumia mashine maalum zilizounganishwa na pampu za nishati wanazouza kwa wateja kinyume na agizo la serikali jijini Dar es Salaam leo.

Kamishna Mkuu wa TRA Charles Kichere aliambatana na maafisa waandamizi kuendesha zoezi hilo kwa baadhi ya vituo ilhali Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango alisimamia zoezi hilo kwa upande Kigamboni na kukemea vikali wale wafanyabiashara wemye tabia ya kukwepa mapato ya serikali kwa kutozingatia agizo la serikali ifikapo Tarehe 30 Agosti Mwaka jana wawe wameshafunga mashine hizo kwenye pampu za kutoa huduma hiyo ili watoapo huduma na kurudisha mikonga ya pampu hizo risiti ya huduma itolewe moja kwa moja kwenye mashine hizo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa zoezi la kufungia vituo mbalimbali, Kamishna Kichere amesema kuwa zoezi hilo ni la nchi nzima na kwa yeyote atakayeshindwa kutii sheria kwa bila shuruti alazamishwa kutii sheria hiyo kwani vituo vyote vinatakiwa kutoa huduma bila kuwepa kulipa kodi.


"Tuliwapa muda wafunge mashine hizo lakini mpaka sasa hawajatekeleza agizo hilo hivyo hatuna budi kuvifunga hivyo vituo mpaka pale watakapotekeleza matakwa ya serikali," amesema Kamshna Kichere. Tumebaini baadhi yao wamefunga mashine hizo kwa baadhi ya pampu ilhali nyingine hawajazifunga hivyo kuendelea kutudanganya kwa kuamini kwamba wamezingatia sheria wakati kiuhalisia wanaedelea kukwepa kulipa kodi.

Naye Kamishna wa Mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Elijah Mwandumbya amesema wafanyabiashara hawana budi kuzingatia sheria za nchi na kutoa huduma kwa kutumia mashine hizo kwani mpaka sasa hakuna malalamiko yaliyotolewa na wafanyabiashara wachache waadilifu wanaoutumia mashine hizo.

Ameongeza kuwa sheria kali zitachukuliwa dhidi ya wafanyabiashara wote ambao vituo vyao vya mafuta vimefungwa na wasithubutu kutoa huduma bila kutimiza masharti ya kuunganisha huduma hizo na pampu za vituo vya pia wawashirikishe TRA ili waruhusiwe kuendelea kutoa huduma hiyo. 


Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere akizungnumza na waandishi wa habari baada ya kikifungia kituo cha Kobili kando ya brabara ya Sam Nujoma Sinza jijini Dar es Salaam leo wakati wa operesheni ya kukagua na kuvifungia kutoa huduma vituo vya mafuta visovyounganishwa na mashine maalum za kielektroniki. Pamoja naye 



Wafanyakazi wa Kampuni ya Yono Auction Mart Limited wakifunga kituo cha Lake Oil Mambibo kando ya Baraara  ya Mabibo Dar es Salaam leo baada ya kukutwa na na kosa la kutotumia mashine za kielekroniki kwa mujibu wa sheria Dar leo.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere akimhoji na kumwagiza ampatie huduma ya mafuta mwendesha bodaboda aliyomnunulia wakati akitafiti kama pampu za kituo cha Lake Oil kilichopo Mambibo kando ya barabara ya Morogoro Dar es Salaam leo kujiridhisha kama imeunganishwa na machine ya kielekroniki. Hata hivyo alipojaribu kwa pampu nyingine kutuoni hapo alibaini baadhi ya pampu hazijaunganishwa na mashine na kuamuru kituo kifungwe mpaka watakapo hapo watakaunganisha huduma zao na mashine hizo.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere akimkabidhi mwendesha bodaboda aliyomnunulia wakati akitafiti kama pampu za kituo cha Lake Oil kilichopo Mambibo kando ya barabara ya Morogoro Dar es Salaam leo kujiridhisha kama imeunganishwa na machine ya kielekroniki. Hata hivyo alipojaribu kwa pampu nyingine kutuoni hapo alibaini baadhi ya pampu hazijaunganishwa na mashine na kuamuru kituo kifungwe mpaka watakapo hapo watakaunganisha huduma zao na mashine hizo.


Wafanyakazi wa Kampuni ya Yono Auction Mart Limited wakifunga moja ya vituo vilivyobainika kutoa huduma pasipo kuubnganishwa na mashine za kielekroniki Dar leo.


Wafanyakazi wa Kampuni ya Yono Auction Mart Limited wakifunga moja ya vituo vilivyobainika kutoa huduma pasipo kuubnganishwa na mashine za kielekroniki Dar leo.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere akizungumza na msimamizi wa Kituo cha Oil Com kilichopo Urafiki Kando ya Barabara ya Morogoro Dar es Salaam leo baada ya kukuta pampu za kituo hicho kikiwa kinatoa huduma wakati pampu hizo hazijaunganishwa na mashine za maalum za kielektroniki.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TRA YAVIPIGA 'STOP' KUTOA HUDUMA VITUO VYA MAFUTA VISIVYOTUMIA MASHINE ZA KIELEKTRONIKI DAR ES SALAAM
TRA YAVIPIGA 'STOP' KUTOA HUDUMA VITUO VYA MAFUTA VISIVYOTUMIA MASHINE ZA KIELEKTRONIKI DAR ES SALAAM
https://i.ytimg.com/vi/XnOURENGAPo/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/XnOURENGAPo/default.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/tra-yavipiga-stop-kutoa-huduma-vituo.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/tra-yavipiga-stop-kutoa-huduma-vituo.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy