F TGGA YAWAAGA GIRL GUIES WA RWANDA, UGANDA NA MADAGASCAR | RobertOkanda

Friday, July 21, 2017

TGGA YAWAAGA GIRL GUIES WA RWANDA, UGANDA NA MADAGASCAR

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Anna Abdallah akimkabidhi  zawadi Girl Guides kutoka Uganda, Rachel Baganyire wakati wa hafla ya kuwaaga Girl Guides kutoka Rwanda, Uganda na Madagascar kwenye Hoteli ya Courtyard Protea, Seaview, Dar es Salaam. Girl Guides hao walikuwa nchini kwa muda wa miezi 6 kwa programu ya kubadilisha uzoefu katika masuala ya utamaduni, maadili na uongozi. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Anna Abdallah akimkabidhi  zawadi Girl Guides kutoka Madagascar, Andriambolamanana Vahatrimama wakati wa hafla ya kuwaaga Girl Guides kutoka Rwanda, Uganda na Madagascar kwenye Hoteli ya Courtyard Protea, Seaview, Dar es Salaam. Girl Guides hao walikuwa nchini kwa muda wa miezi 6 kwa programu ya kubadilisha uzoefu katika masuala ya utamaduni na uongozi.

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Anna Abdallah akimkabidhi  zawadi Girl Guides kutoka Rwanda, Michelline Uwiringiyimana wakati wa hafla ya kuwaaga Girl Guides kutoka Rwanda, Uganda na Madagascar kwenye Hoteli ya Courtyard Protea, Seaview, Dar es Salaam. Girl Guides hao walikuwa nchini kwa muda wa miezi 6 kwa programu ya kubadilisha uzoefu katika masuala ya utamaduni na uongozi.

 Vingozi wa TGGA wakiwa katika picha ya pamoja Girl Guides wanaoagwa

Girl Guides waliokuwa katika mafunzo ya uongozi, maadili na utamadun walioagwa; Wasichana hao ni; Michelline Uwiringiyimana (Rwanda), kulia, Recheal Baganyire (Uganda),kushoto, na Andriambolamanana Vahatrimama.

Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TGGA, Grace Makenya akizungumza wakati wa hafla hiyo.

 Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba akizungumza wakati wa kuanza kwa hafla hiyo ambapo alianza kwa kuwatambulisha viongozi wa TGGA. Kulia ni Kamishna wa TGGA Makao Makuu, Rose Majuva.

 Kiongozi wa Girl Guides Mkoa wa Dar es Salaam, Ruth akitambulishwa wakati wa hafla hiyo..

Dereva wa TGGA, Juma akitambulishwa

Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi (wa pili kushoto) akiwa katika hafla hiyo

Recheal Baganyire Girl Guides kutoka Uganda

Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TGGA, Zakia Meghji akizungumza na Recheal Baganyire Girl Guides kutoka Uganda

Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi akizungumza wakati wa hafla hiyo

Mwenyekiti wa Taifa wa TGGA, Martha Qorro akitoa nasaha kwa Guides wakati wa hafla hiyo

Andriambolamanana Vahatrimama.

Michelline Uwiringiyimana (Rwanda)

Michelline Uwiringiyimana (Rwanda), akitoa shukrani kwa TGGA kwa kuwalea kwa muda wote wa miezi sita na kwamba wamejifunza mambo mengi watakayokwenda kufundisha kwao.

Mkufunzi wa TGGA Makao Makuu akizungumza alipotambulishwa

Kamishna Mkuu wa TGGA Makao Makuu, Rose Majuva akizungumza alipotambulishwa

Kiongozi wa Girl Guides TGGA Makao Makuu, Valentina (katikati) akijadiliana jambo na Michelline Uwiringiyimana (Rwanda) pamoja na Andriambolamanana Vahatrimama.

Kiongozi wa TGGA Makao Makuu, Rehema Kijazi (kulia) akiwa na Mhasibu wa chama hicho

Sasa ni wakati wa misosi

Ni misosi kwa kwenda mbeleAnna Abdallah akitoa nasaha kwa Girl Guides wanaoagwa kutumia vizuri mafunzo waliyoyapata nchini na kwenda kufundisha wenzao katika nchi zao.

Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TGGA, Grace Makenya naye akitoa nasaha zake

Girl Guides wanaoagwa wakiwa katika picha ya pmoja na viongozi wa TGGA

Kamishna Mkuu wa TGGA, Hangi akiwa katika picha na Girl Guides wanaoagwa

0 comments:

Post a Comment