Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto)akisalimiana na Mjumbe wa “The Elders” Taasisi inayoshughulika na Amani, Haki...
Spika wa
Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto)akisalimiana na Mjumbe wa “The
Elders” Taasisi inayoshughulika na Amani, Haki za Binadamu na Huduma za
Afya, Ndg. Graca Machel (kulia) katika tukio lililofanyika leo katika
viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job
Ndugai (kushoto)akisalimiana na Rais Mstaafu wa Ireland (kulia) ambae
pia ni Mjumbe wa “The Elders” Taasisi inayoshughulika na Amani, Haki za
Binadamu na Huduma za Afya, Mhe. Mary Robinson katika tukio
lililofanyika leo katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job
Ndugai (kulia)akizungumza wakati ugeni kutoka “The Elders” Taasisi
inayoshughulika na Amani, Haki za Binadamu na Huduma za Afya
ilipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, katikati ni Rais Mstaafu
wa Ireland ambae pia ni Mjumbe kutoka Taasisi hiyo Mhe. Mary Robinson na
kushoto ni Mjumbe wa Taasisi hiyo Ndg. Graca Michel
……………………………………………………………………….
SPIKA wa Bunge, Mheshimiwa Job
Ndugai amesema Bunge litaendelea kuungana mkono jitihada za Serikali za
kuboresha afya ya jamii ikiwemo uzazi salama, afya ya mama na mtoto na
afya ya wazee.
Spika alitoa kauli hiyo Ofisini
kwake Mjini Dodoma alipotembelewa na Rais Mstaafu wa Ireland Mheshimiwa
Mary Robnson na Mama Graca Machel pamoja na ujumbe wao kutoka Taasisi ya
‘The Elderes’ ya Uingereza inayoshughulikia masuala ya Amani, Haki za
Binadamu na Huduma za Afya.
Alisema siku zote Bunge limekuwa
likipigania masuala mbalimbali yahusuyo afya ya jamii na kwamba ipo
kamati maalamu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ambayo
inashughulikia masuala mbalimbali ikiwemo Huduma za Afya.
Alisema pia wapo wabunge mmoja
mmoja ambao huyasemea masuala ya afya ya jamii na kwamba wamekuwa
wakiuliza maswali mbalimbali kwa mawaziri na kujibiwa.
Kwa upande wake, Mama Machel
alisema wanatambua mchango wa Tanzania katika kuboresha huduma za afya
na kuishauri iendelee kufanya vizuri zaidi kwa kuongeza kipaumbele ka
kile kilichowekwa katika elimu kwa kutoa elimu bure hadi kidato cha
nne kifanyike hivyo hivyo katika sekta ya afya.
Alisisitiza pia Wabunge
kuhakikisha wanatenga bajeti ya kutosha katika sekta ya afya pamoja
nakupitisha sheria zitakazosaidia kuobresha sekta hiyo.
Naye Mheshimiwa Robson alisema
anatambua nguvu ya Bunge katika kuhakikisha afya ya jamii inaboreshwa na
kusifu juhudi za Tanzania za kuboresha elimu na sekta ya afya pia.
Mheshimiwa Robson na Mama Machel
ni wajumbe wa Taasisi ya ‘The Elderes’ ya Uingereza inayoshughulikia
masuala ya amani, haki za binadamu na huduma za afya.
COMMENTS