SERIKALI KUIMARISHA UWANJA WA NDEGE WA MPANDA

SERIKALI imemuagiza Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda kuwasiliana na Kampuni ya Uendelezaji Uwanja wa Ndege wa   Kilimanjar...


SERIKALI imemuagiza Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda kuwasiliana na Kampuni ya Uendelezaji Uwanja wa Ndege wa  Kilimanjaro (KADCO) ili kupata gari la Zimamoto ili ndege za Shirika la ndege Tanzania (ATCL) ziweze kuanzisha safari zake katika Mkoa wa Katavi.
Akizungumza mara baada ya kukagua uwanja huo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani amesema kwa muda sasa kiwanja hicho kimekuwa kikitumiwa  na ndege chache za Shirika la kuhudumia wakimbizi (UNHCR), hivyo ni wakati sasa kutumika na ndege zetu ili kuboresha huduma za usafiri wa anga Mkoani hapa.
“Kamilisheni  mazungumzo na KADCO ili kupata gari la Zimamoto lenye ujazo wa Lita 4,000 litakalokuwa na uwezo wa kukabiliana na majanga ya moto endapo yatatokea, kutakapokuwa na gari hilo uwanjani hapa tutaanzisha safari za ndege za Shirika letu wakati ndege yetu ta tatu itakapowasili,” amesema Eng. Ngonyani.
Aidha, amemtaka meneja wa Uwanja huo wa ndege kuhakikisha anaingiza uwanja huo katika mpango maalum kwa ajili ya ujenzi wa taa kiwanjani hapo ili uwanja huo uweze kutumika kwa mchana na usiku.
Eng. Ngonyani ameongeza kuwa azima ya Serikali ni kuhakikisha usafiri wa anga nchini unaimarika  kwa kutumia ATCL na mashirika mengine yalipo nchini hivyo kama Serikali imejipanga kuendelea kuboresha miundombinu ya viwanja ili viwe katika viwango vinavyokubalika.
Kwa upande wake Meneja wa Uwanja huo Seneth Lyatuu amemuhakikishia Eng. Ngonyani kuwa changamoto ya kuwa na Gari la zimamoto itatatuliwa mapema ili wakazi wa Mpanda waweze kunufaika na huduma za ATCL na hivyo kuwapa unafuu watumiaji wa  usafiri wa anga.
“Kuanza kwa safari za ATCL hapa Mpanda kutawapunguzia gharama wananchi ambao kwa sasa hulazimika kwenda Mwanza au Mbeya ili kupata ndege ya kwenda Dar es Salaam na gharama huwa kubwa,” amesisitiza Lyatuu.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Bw. Saleh Mhando  amesema kutalete tija na kutafungua fursa ya utalii wa ndani na nnje ya nchi hasa kwa kuwepo na Mbuga ya Katavi ambayo ina vivutio vingi.
Katika hatua nyingine Eng. Ngonyani amelipongeza Shirika la Reli Tanzania (TRL) kwa kutekeleza agizo la Serikali la kutumia Mfumo wa kielektroniki katika kudhibiti mapato ambapo shirika hilo limeanza kukatisha tiketi kwa njia hiyo katika stesheni za Mpanda na Tabora.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani(Kulia) akikagua Mfumo wa ukatishaji tiketi kwa njia ya kielekroniki katika Stesheni ya Mpanda Mkoani Katavi. Katikati ni Meneja Mradi wa kampuni ya Makgroup Ltd Bw. Joseph Mrosso.


Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kampuni ya Reli Tanzania, Kanda ya Tabora Bw. Frederick Masangwa(Katikati), wakati alipokagua huduma za usafiri wa Reli Mkoani Katavi.


Meneja wa Msimamizi wa Bandari ya Kigoma Bw. Morris Mchindiuza (aliyenyoosha mkono) akimwonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Wa pili kulia) eneo itakapojengwa bandari ya Kalema iliyopo Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi.Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Wa pili) akitoka kukagua kingo za bandari ya Kalema iliyopo Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: SERIKALI KUIMARISHA UWANJA WA NDEGE WA MPANDA
SERIKALI KUIMARISHA UWANJA WA NDEGE WA MPANDA
https://2.bp.blogspot.com/-Mov5QP982Y0/WWJ6sO751YI/AAAAAAAA37w/jtytqFwgvnkM9W3e9JII2e57jILtpDGmgCLcBGAs/s640/1%25282%2529.JPG
https://2.bp.blogspot.com/-Mov5QP982Y0/WWJ6sO751YI/AAAAAAAA37w/jtytqFwgvnkM9W3e9JII2e57jILtpDGmgCLcBGAs/s72-c/1%25282%2529.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/serikali-kuimarisha-uwanja-wa-ndege-wa.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/serikali-kuimarisha-uwanja-wa-ndege-wa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy