RC SHINYANGA AKUTANA NA WAWEKEZAJI NA WAFANYABIASHARA WA MKOA WA SHINYANGA

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack amekutana na wawekezaji na wafanyabiashara wa mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kufahamiana na ku...





Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack amekutana na wawekezaji na wafanyabiashara wa mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kufahamiana na kujadili mambo kadha wa kadha ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika mkoa wa Shinyanga Julai 20,2017.



Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga na kukutanisha wawekezaji na wafanyabiashara kutoka wilaya zote za mkoa wa Shinyanga. 

Akizungumza katika kikao hicho,Telack alisema huu ni mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa miaka mitano 2016/2017 – 2020/2021 wenye dhima ya kujenga uchumi wa viwanda ili kuchochea mageuzi ya maendeleo ya watu 

“Ili kutimiza malengo ya mpango huu lazima serikali ifanye kazi kwa ushirikiano wa karibu na sekta binafsi na nyinyi ni sehemu ya sekta binafsi na ili kudumisha ushirikiano huo serikali imeanzisha mabaraza ya biashara katika ngazi ya taifa, mikoa na wilaya”, alieleza Telack.


Aidha alisema uwekezaji ni moja ya shughuli zinazochochea kasi ya ukuaji wa uchumi wa mkoa wa Shinyanga na taifa kwa ujumla ambapo hadi sasa mkoa huo una jumla ya viwanda 81,ambapo viwanda vikubwa ni 18,viwanda vya kati 9 na vidogo 54.
Mwandishi wetu Kadama Malunde ametuletea picha 32 za matukio wakati wa kikao hicho,Tazama hapa chini


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akitoa hotuba yake wakati wa kikao chake pamoja na wawekezaji na wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga Alhamis Julai 20,2017.




Wafanyabiashara,wawekezaji na wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwa ukumbini



Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akizungumza katika kikao hicho ambapo aliwahamasisha wafanyabiashara kushirikiana na kupeana fursa mbalimbali



Kaimu Mwenyekiti wa wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga Jackton Koy akizungumza katika kikao hicho.



Kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga Jackton Koy,katikati ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akifuatiwa na katibu tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela.




Kikao kinaendelea




Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akichangia hoja katika kikao hicho



Wawekezaji na wafanyabiashara wakiwa katika kikao.




Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba akichangia hoja ukumbini



Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Said Pamui akizungumza katika kikao hicho



Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Muliro Jumanne Muliro aliyehamishiwa mkoa wa Kinondoni akizungumza ukumbini.




Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mada katika Kikao hicho.

Mkurugenzi wa SHUWASA Mhandisi Sylivester Mahole akichangia hoja ukumbini.



Meneja wa Ustawi wa Jamii na Kampuni ya Acacia Bulyanhulu, Elias Kasitila akizungumza katika kikao hicho.



Meneja wa Ustawi wa Jamii na Kampuni ya Acacia Bulyanhulu, Elias Kasitila akichangia hoja ukumbini.




Wafanyabiashara na wawekezaji wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini.



Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mada katika Kikao hicho.




Mkurugenzi wa Hasmukh Group, Kishan Hasmukh akichangia hoja wakati wa kikao hicho.



Meneja wa Ustawi wa Jamii na Kampuni ya Acacia Bulyanhulu,Elias Kasitila (kushoto) na Meneja Uendelevu mgodi wa Buzwagi George Mkanza wakiwa katika kikao hicho




Wawekezaji wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini.




Kikao kinaendelea




Kikao kinaendelea.




Wadau wakiwa ukumbini




Mwekezaji Gilitu Nila Makula akizungumza ukumbini.




Mkurugenzi wa Soud Group,Hilal Soud akichangia hoja wakati wa kikao hicho







Katibu wa Wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga Macelina Lauo akizungumza wakati wa kikao hicho.

 Meneja Uendelevu mgodi wa Buzwagi George Mkanza  akifuatilia kwa umakini kilichokuwa kinaendelea ukumbini.






Tunafuatilia kinachoendelea....





Mwenyekiti wa waendesha bodaboda manispaa ya Shinyanga Wenceslaus Modest akichangia hoja



Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mada katika Kikao hicho.


(Picha zote Kadama Malunde - Malunde1 blog)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RC SHINYANGA AKUTANA NA WAWEKEZAJI NA WAFANYABIASHARA WA MKOA WA SHINYANGA
RC SHINYANGA AKUTANA NA WAWEKEZAJI NA WAFANYABIASHARA WA MKOA WA SHINYANGA
https://3.bp.blogspot.com/-Dh9VeBqSryU/WXCMiu2aUVI/AAAAAAAAQtA/7_pVbjw_ITIKdlBc0YJkNpPAJlGpM40QgCLcBGAs/s640/UF3A1213.JPG
https://3.bp.blogspot.com/-Dh9VeBqSryU/WXCMiu2aUVI/AAAAAAAAQtA/7_pVbjw_ITIKdlBc0YJkNpPAJlGpM40QgCLcBGAs/s72-c/UF3A1213.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/rc-shinyanga-akutana-na-wawekezaji-na.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/rc-shinyanga-akutana-na-wawekezaji-na.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy