NDOA ZA KIHISTORIA KUFUNGWA SIKU MOJA NDANI YA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA

Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya waliookoka katika kanisa hilo huku tayari wakiwa wanaishi na wenza wao kama mme na mke bila kufunga n...


Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya waliookoka katika kanisa hilo huku tayari wakiwa wanaishi na wenza wao kama mme na mke bila kufunga ndoa takatifu, wamepata fursa ya kufungishwa rasmi ndoa takatifu.

Mchungaji wa kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola amesema si vyema waliookoa kuishi kama mme na mke huku wakiwa hawajafunga ndoa takatifu madhabahuni mwa Bwana hivyo jumapili ijayo Julai 16,2017 zitafungwa ndoa za pamoja zaidi ya tisa kwa waumini waliookoka huku tayari wako kwenye ndoa bubu.

"Usikae na mme au mke bila kufunga ndoa, maana ndoa bubu itakukotea puani. Acha kuvaa mapete ya ajabu ajabu bila kufunga ndoa. Unakuta lipete lina kichwa cha nyoka, jiulize hilo lipete umepewa na nani? Huenda ndiyo maana unaandamwa na mapepo". Alisisitiza Dkt.Mchungaji Kulola.

Baadhi ya wanaotarajiwa kufunga ndoa siku hiyo, wamefurahishwa na fursa waliyoipata huku wakisema aina hiyo ya ndoa ni nzuri kwa kuwa hawatatumia gharama kubwa kwani baada ya kufunga ndoa, watapata chakula cha pamoja kanisani hapo na baadaye kurejea nyumbani.

Tukio hilo la kihistoria litaanza saa nane kamili mchana katika kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Jijini Mwanza na watu wote wanakaribishwa kulishuhudia ambapo baada ya ndoa hizo kufungwa, itafanyika tafrija fupi kanisani hapo ambapo watu watakula na kunywa pamoja na wanandoa hao.

Mwenyekiti wa kamati ya harusi (kushoto) na katibu wake.[/caption]

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: NDOA ZA KIHISTORIA KUFUNGWA SIKU MOJA NDANI YA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA
NDOA ZA KIHISTORIA KUFUNGWA SIKU MOJA NDANI YA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA
http://www.bmghabari.com/wp-content/uploads/2017/07/EAGT-1024x768.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/ndoa-za-kihistoria-kufungwa-siku-moja.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/ndoa-za-kihistoria-kufungwa-siku-moja.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy