MKUTANO WA KIMATAIFA WA SHUKRANI KUFANYIKA KESHO UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ES SALAAM

Muhubiri wa Kimataifa Dk.Nicku Kyungu akihubiri katika kongamano la siku mbili la viongozi wa dini lilifanyika Kanisa la Naoith Pentekos...Muhubiri wa Kimataifa Dk.Nicku Kyungu akihubiri katika kongamano la siku mbili la viongozi wa dini lilifanyika Kanisa la Naoith Pentekoste Church Makuburi jijini Dar es Salaam leo kwa Askofu Dk. David Mwasota. Kongamano hilo linakwenda sanjari na mkutano wa kitaifa wa shukrani wa kuliombea taifa na Rais Dk.John Magufuli utakaofanyika kesho Uwanja wa Uhuru.


Mtumishi wa Mungu Askofu Mwaka kutoka nchini Zambia akihubiri katika kongamano hilo.
Askofu Timoth Joseph kutoka nchini Nigeria akihubiri  na kufundisha neno la mungu katika kongamano hilo.
Maaskofu na watumishi wa mungu wakiwa meza kuu wakati wa kongamano hilo.
Maombi yakifanyika.
Mchungaji Dk. William Kopwe wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania , kutoka Dodoma akiwa katika kongamano hilo na mkewe.
Viongozi wa dini maaskofu na wachungaji wakiwa kwenye kongamano hilo.
Maombi yakiendelea.
Kongamano likiendelea.
Taswira ya kongamano hilo.
Mwonekano  katika kongamano.
Watumishi wa mungu wakiwa katika maombi.
Utulivu katika kongamano hilo.


Na Dotto Mwaibale

KESHO Jumamosi maaskofu mbalimbali, viongozi wa serikali na taasisi na viongozi wa dini na wananchi watakutana Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maombi ya kitaifa ya shukrani ya kuiombea nchi na Rais Dk.John Magufuli.

Maombi hayo ya kihistoria yameandaliwa na viongozi wa dini kutoka madhehebu mbalimbali ya Huduma Tanzania na Taasisi ya I Go Africa For Jesus.

Katika maombi hayo yatakayofanyika kesho watumishi wa mungu kutoka ndani na nje ya Tanzania wakiwepo maaskofu watahudhuria.

Lengo kubwa la maombi hayo ni kuiombea nchi amani na  kumuunga mkono rais Dk.Magufuli ambaye amekuwa akiomba watanzania wamuombee mara kwa mara.

Kabla ya maombi hayo kwa jana na leo lilifanyika kongamano la viongozi wa dini ambapo watumishi wa mungu mbalimbali waliweza kufundisha mambo ya kiroho na somo la uaminifu na utunzaji wa fedha.

Muhubiri wa kimataifa 'Mama Afrika' Dk. Nicku Kyungu ameomba wananchi, viongozi wa dini kufika kuhudhuria maombi hayo bila kujali dini ya mtu kwani ni ya muhimu kwa nchi.

Alisema maombi hayo yanatoa fursa kwa kila mwananchi ya kuliombea taifa na kuwa yataanza saa tatu asubuhi hadi mchana ambapo kwaya mbalimbali zitakuwa zikitoa burudani ya nyimbo za kumtukuza mungu.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)


COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MKUTANO WA KIMATAIFA WA SHUKRANI KUFANYIKA KESHO UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ES SALAAM
MKUTANO WA KIMATAIFA WA SHUKRANI KUFANYIKA KESHO UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ES SALAAM
https://2.bp.blogspot.com/-fZtqIoTgqxY/WWifXtqzfdI/AAAAAAAAbQ4/R3SuBMfhXGoHCLvWRJaxBuw8dVGRVuWlQCEwYBhgL/s640/1.JPG
https://2.bp.blogspot.com/-fZtqIoTgqxY/WWifXtqzfdI/AAAAAAAAbQ4/R3SuBMfhXGoHCLvWRJaxBuw8dVGRVuWlQCEwYBhgL/s72-c/1.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/mkutano-wa-kimataifa-wa-shukrani.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/mkutano-wa-kimataifa-wa-shukrani.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy